Umuhimu wa Broshua katika biashara yako
Broshua haina
tofauti sana na Kipeperushi lakini yenyewe inakuwa imedizainiwa na kuprintiwa
pande zote na kukunjwa ,lakini kipeperushi chenyewe hakina kukunjwa na huprintiwa pande moja tu.
Broshua hazitolewi
kama kipeperushi mara nyingi broshua hugawiwa na mtu wa masoko baada ya kuona
mteja amevutiwa na kitu fulani au anahitaji maelezo zaidi ya kitu ambacho
maelezo ya kina yapo kwenye broshua hiyo au amevutiwa na kitu fulani, Broshua
ni lazima iwe ni nzuri na nadhifu.
Sababu za kutoa
Broshua ni pamoja na
- Kufuatilia maelezo zaidi kuhusu mawasiliano ya mauzo
- Kutoa maelezo ya kina na mengi zaidi kuhusiana na biashara,bidhaa au promosheni
- Kupata muitikio wa mteja mtarajiwa kwa kuonyesha uwezo,gharama na mategemeo
Watu wengi wamekuwa
wanaacha kujitangaza au kutengeneza vitu vya kujitangaza kwa vile tu pale mauzo
yanapoongezeka ni makosa kusimamisha promosheni kwa ajili tu unapata faida
inatakiwa kila siku kuwe na promosheni inayoendelea ndani ya biashara yako na inatakiwa
iwe inafanyiwa matangazo.
Chapisho lijalo
nitaelezea utangulizi wa Branding
Pia kwa wale
watakaohitaji professional email za branding .co. tz kwa ajili ya biashara
zao,tafadhali wasiliana nami kwa mawasiliano hapo chini
Bado mnakaribishwa
kujiunga na kundi la Whatsapp Branding kwa kuandika namba yako katika sehemu ya comment chini ya uzi huu ili uunganishwe, Asante. Kauli mbiu ya mwaka huu ni
Mabadiliko lazima.
Pia karibu utangaze
nasi na biashara yako ifikie watu wengi zaidi nje na ndani ya nchi kupitia
blogu hii maelezo zaidi kuhusu kutangaza piga simu nama 0713603699.
0654660000
ReplyDelete0654660000
ReplyDelete