Posts

Showing posts from February, 2015

Umuhimu wa Broshua katika biashara yako

Broshua haina tofauti sana na Kipeperushi lakini yenyewe inakuwa imedizainiwa na kuprintiwa pande zote na kukunjwa ,lakini kipeperushi chenyewe  hakina kukunjwa na huprintiwa pande moja tu. Broshua hazitolewi kama kipeperushi mara nyingi broshua hugawiwa na mtu wa masoko baada ya kuona mteja amevutiwa na kitu fulani au anahitaji maelezo zaidi ya kitu ambacho maelezo ya kina yapo kwenye broshua hiyo au amevutiwa na kitu fulani, Broshua ni lazima iwe ni nzuri na nadhifu. Sababu za kutoa Broshua ni pamoja na Kufuatilia maelezo zaidi kuhusu mawasiliano ya mauzo Kutoa maelezo ya kina na mengi zaidi kuhusiana na biashara,bidhaa au promosheni Kupata muitikio wa mteja mtarajiwa kwa kuonyesha uwezo,gharama na mategemeo Watu wengi wamekuwa wanaacha kujitangaza au kutengeneza vitu vya kujitangaza kwa vile tu pale mauzo yanapoongezeka ni makosa kusimamisha promosheni kwa ajili tu unapata faida inatakiwa kila siku kuwe na promosheni inayoendelea ndani ya biashara yako na ...

Umuhimu na maana ya Kipeperushi(Flyer) katika biashara yako.

Image
                               Kipeperushi ni karatasi isiyokunjwa iliyodizainiwa vizuri mahsusi kwa ajili  ya kukutangaza,na inatumika kuweka umakini kuhusu tukio,huduma,bidhaa au wazo . Kipeperushi kama kinavyoitwa hutumika kupeperusha habari au tangazo lako na kipeperushi mara nyingi hubeba ujumbe rahisi na mwepesi kufika kwa walengwa,kipeperushi hutumika sana kwenye halaiki ya watu wengi, Vipeperushi havina gharama kubwa na pia ni njia rahisi ya kufikisha ujumbe kwa watu wengi kwa wakati mmoja. Aina hii ya kujitangaza kupitia kipeperushi huitwa tupa mbali, kwa sababu mara nyingi mtu anaepewa kipeperushi mara nyingi anakuwa kwenye mwendo ambapo akisoma anapomaliza wengi  wao huvitupa kwa kuwa ameshakisoma ambapo sehemu atakapo kitupa yeye pia kuna mwingine atakiokota ili aone ni tangazo la nini na yeye atafanya vivyo hiyo akimaliza kusoma hivyo habari inawafikia wengi kwa mtindo wa...

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Image
Logo ni alama au nembo iliyodizainiwa mahsusi kwa ajili ya biashara yako, inayotumika kukutambulisha nje na ndani ya ofisi. Au  Logo ni alama au nembo inayotumika kutambulisha huduma,bidhaa,kampuni au mfumo wowote wa vikundi. Logo au nembo inamaanisha vitu vingi kuhusu biashara yako kulingana na muonekano wake , biashara nyingi sana utambulisho wake hupatikana kwanza kwenye logo,matangazo  mengi hulenga watu kukumbuka lengo na logo ya biashara. Logo ndio kitu ambacho mtu hufikiria anaposikia jina la kampuni au biashara yako. Mfano: Unaposikia jina Cocacola, Azam,TBS,Vodacom,Legacy,Pepsi, kitu cha kwanza kitakachokuja kwenye kichwa chako ni logo ya kampuni kisha ma tangazo uliyokwisha kuyasikia au kuyaona kuhusiana na huduma au bidhaa zao huanza kujirudia kichwani.hivyo                           Hivyo logo ni ya muhimu sana kwa maendeleo au mafanikio ya biashara yako.Chini hapa ni baadhi ya mambo a...