Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.
Logo ni alama au
nembo iliyodizainiwa mahsusi kwa ajili ya biashara yako, inayotumika
kukutambulisha nje na ndani ya ofisi. Au
Logo ni alama au nembo inayotumika kutambulisha huduma,bidhaa,kampuni au
mfumo wowote wa vikundi.
Logo au nembo
inamaanisha vitu vingi kuhusu biashara yako kulingana na muonekano wake ,
biashara nyingi sana utambulisho wake hupatikana kwanza kwenye
logo,matangazo mengi hulenga watu
kukumbuka lengo na logo ya biashara. Logo ndio kitu ambacho mtu hufikiria
anaposikia jina la kampuni au biashara yako.
Mfano: Unaposikia
jina Cocacola, Azam,TBS,Vodacom,Legacy,Pepsi, kitu cha kwanza kitakachokuja
kwenye kichwa chako ni logo ya kampuni kisha matangazo uliyokwisha kuyasikia au
kuyaona kuhusiana na huduma au bidhaa zao huanza kujirudia kichwani.hivyo
Hivyo logo ni ya
muhimu sana kwa maendeleo au mafanikio ya biashara yako.Chini hapa ni baadhi ya
mambo ambayo Logo huwakilisha kwa wakati mmoja pindi inapoonekana.
1.Humpa mteja maana
au tafsiri ya biashara yako japo inaweza kuwa sio sawa na ya kwako
2.Huonyesha
muonekano unaotakiwa
3.hukuongezea hadhi
4.huonyesha utofauti
wako na wengine katika soko
5.Kuwa na muonekano
wa kuvutia
6.Hujipanga yenyewe
kwa makengo flani ya soko.
Sababu kwanini
biashara yako inahitaji logo, kuna sababu nyingi kwanini biashara yako iwe na
logo tena sio logo tu iwe na logo iliyodizainiwa vizuri, baadhi ya sababu za
msingi ni pamoja na
- Ikiwa unafungua biashara mpya
- Ikiwa unatambulisha biashara mpya
- Ikiwa unabadilisha jina la biashara
- Ikiwa asili ya biashara yako imebadilika
- Kubadilisha ili kuendana na soko kama inaonekana ni ya kizamani
- Kutaka kuwarahisishia wateja wako utambuzi wa bidhaa au biashara yako
- Ukiwa unahitaji kutofautisha bidhaa na kampuni
Chapisho lijalo
nitaelezea kwanini biashara yako inatakiwa iwe na Flyers(Vipeperushi)
Bado mnakaribishwa
kujiunga na kundi la Whatsapp Branding kwa kutuma namba yako na jina lako
kwenda namba 0767603699 ili uunganishwe, Asante. Kauli mbiu ya mwaka huu ni
Mabadiliko lazima.
Pia karibu utangaze
nasi na biashara yako ifikie watu wengi zaidi nje na ndani ya nchi kupitia
blogu hii maelezo zaidi kuhusu kutangaza piga simu nama 0767603699.
Comments
Post a Comment