Kabla ya kuanza kufanya marketing jiulize maswali yafuatayo
Marketing kwa maana
moja mimi huwa naiita ni zao la Branding kwenye biashara ambalo linatakiwa
litoke liende kuitangaza brand iliyojitengeneza.Hapa nchini biashara nyingi
zinafanyika kwa mazoea na watu wanafanya bila kuelewa au kuwa na maana halisi
ya kitu wanachokifanya, utakuta mtu ameona kampuni fulani wamefanya kitu fulani
kwa ajili ya bidhaa, biashara au huduma kwa ajili ya kampuni yao, basi na yeye
pia atataka kubadilisha jina tu kwenye hicho kitu kutoka jina la biashara alioiona hadi jina la biashara
yake, ila vingine ataviaacha kama vya mwenzake kwa vile tu amependa jinsi kile kitu kilivyo. Na wengine hufanya hivyo kwa mifano na kujaribu .
Leo nitaelezea
kidogo vitu vya kuzingatia kabla hujaanza kujitangaza au kufanya
marketing,Tutaangalia vitu kama vitano(5) ambavyo unatakiwa kuviangalia kwenye
biashara yako kabla ya kuanza kufanya marketing, vitu hivi mara zote huwa ni
vitu vya kawaida na huonekana ni sio vya muhimu sana lakini nikupe siri ndugu
yangu hakuna kitu ambacho sio cha muhimu hata kama ni kidogo kiasi gani.
- Uko kwenye biashara gani?
Kabla
ya kufanya marketing lazima utambue uko
katika biashara ya aina gani, kuna biashara za aina mbili huduma na bidhaa.Njia
zake za kufanya marketing (kutafuta
masoko) zinatofautiana japo soko ni moja, kila biashara huwa inamtafuta mteja,
mfano wa biashara zinazotoa huduma ni kama Washauri, Mahospitalini, n.k na biashara zinatoa bidhaa ni kama Makampuni
ya vinywaji, Maduka n.k . Hivyo hata
katika mbinu za utafutaji wake wa masoko zinakuwa tofauti, mbali na kutambua
aina ya biashara ni lazima hapo hapo utambue na njia zake za kuingiza na kutoa
pesa
- Malengo yangu ni yapi?
Baada
ya kutambua aina yako ya biashara sasa unakuja hatua ya pili ambayo ni kutambua
malengo, katika biashara malengo ni kitu cha muhimu na asilimia kubwa ya
biashara zinazofanikiwa ni kwa sababu zimesimamia malengo na kuhakikisha
yanafikiwa. Hivyo ni lazima biashara iwe na malengo na sio kampuni peke yake
bali kila kinachofanyika ndani na nje ya biashara ni lazima kiwe na lengo ama
malengo ambayo hayatakiwi kuwa na mwisho unaotofautiana.
- Nnatoa faida gani?
Faida
pia ni kitu kingine kikubwa ambacho kinaongozwa na marketing na mauzo hivyo
kabla ya kuingia katika kutafuta masoko inabidi kwanza utambue unatoa faida
gani kwa biashara unayoifanya na unataka ikupe matokeo gani? na wewe mwenyewe na biashara mnatoa faida gani kwa mtumiaji wa mwisho na iwapo wewe ndio ungekuwa mtumija wa mwisho ungependa bidhaa au huduma itoleweje?.
4 . Nini ni faida nilizonazo
kwenye ushindani?
Kabla
ya kuingia katika ushindani sokoni ni lazima pia uangalie faida za ushindani,
ambapo faida za ushindani ni kwako ni udhaifu wa mshindani ,sio tu kuanzisha
kampeni kwa vile mwenzako ametengeneza kitu kama kile na wewe ufanye kwa
kutegemea matokeo sawia, angalia kwanza unafaida gani za kiushindani na
unazitumia vipi hapo ndio unaweza kufanya kitu ili kikuletee matokeo chanya.
5. Nnaogopa nini?
Kama
mfanyabiashara au biashara lazima kuna vitu ambavyo utakuwa unaviogopa kwenye
soko haijalishi vinaathari kwako au kwenye biashara, vitu hivyo pia vinatakiwa
viwekwe hadharani kwa kuzingatia aina ya biashara na kampeni ya masoko
unayotaka kuifanya hii itakusaidia kutengeneza njia nzuri za kuviepuka au
kutafutia mbinu mbadala ya kuvishinda.
Je unahitaji kujua chochote kuhusu Branding na Marketing? karibu
ReplyDelete