Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Logo ni alama au nembo iliyodizainiwa mahsusi kwa ajili ya biashara yako, inayotumika kukutambulisha nje na ndani ya ofisi. Au  Logo ni alama au nembo inayotumika kutambulisha huduma,bidhaa,kampuni au mfumo wowote wa vikundi.

Logo au nembo inamaanisha vitu vingi kuhusu biashara yako kulingana na muonekano wake , biashara nyingi sana utambulisho wake hupatikana kwanza kwenye logo,matangazo  mengi hulenga watu kukumbuka lengo na logo ya biashara. Logo ndio kitu ambacho mtu hufikiria anaposikia jina la kampuni au biashara yako.

Mfano: Unaposikia jina Cocacola, Azam,TBS,Vodacom,Legacy,Pepsi, kitu cha kwanza kitakachokuja kwenye kichwa chako ni logo ya kampuni kisha matangazo uliyokwisha kuyasikia au kuyaona kuhusiana na huduma au bidhaa zao huanza kujirudia kichwani.hivyo
                         


Hivyo logo ni ya muhimu sana kwa maendeleo au mafanikio ya biashara yako.Chini hapa ni baadhi ya mambo ambayo Logo huwakilisha kwa wakati mmoja pindi inapoonekana.

1.Humpa mteja maana au tafsiri ya biashara yako japo inaweza kuwa sio sawa na ya kwako
2.Huonyesha muonekano unaotakiwa
3.hukuongezea hadhi
4.huonyesha utofauti wako na wengine katika soko
5.Kuwa na muonekano wa kuvutia
6.Hujipanga yenyewe kwa makengo flani ya soko.

Sababu kwanini biashara yako inahitaji logo, kuna sababu nyingi kwanini biashara yako iwe na logo tena sio logo tu iwe na logo iliyodizainiwa vizuri, baadhi ya sababu za msingi ni pamoja na
  1. Ikiwa unafungua biashara mpya
  2. Ikiwa unatambulisha biashara mpya
  1. Ikiwa unabadilisha jina la biashara
  1. Ikiwa asili ya biashara yako imebadilika
  1. Kubadilisha ili kuendana na soko kama inaonekana ni ya kizamani
  1. Kutaka kuwarahisishia wateja wako utambuzi wa bidhaa au biashara yako
  2. Ukiwa unahitaji kutofautisha bidhaa na kampuni

Chapisho lijalo nitaelezea kwanini biashara yako inatakiwa iwe na Flyers(Vipeperushi)


Bado mnakaribishwa kujiunga na kundi la Whatsapp Branding kwa kutuma namba yako na jina lako kwenda namba 0767603699 ili uunganishwe, Asante. Kauli mbiu ya mwaka huu ni Mabadiliko lazima.


Pia karibu utangaze nasi na biashara yako ifikie watu wengi zaidi nje na ndani ya nchi kupitia blogu hii maelezo zaidi kuhusu kutangaza piga simu nama 0767603699.

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Aina za malengo na mipango