Posts

Showing posts from June, 2016

Jinsi ya kujitangaza na wapi pa kujitangaza

Utafutaji wa masoko umebadilija sana kipindi cha hivi karibuni kutoka mauzo mengi kwa ushawishi wa mdomo hadi kwenye kujitangaza kupitia mtandao. Asilimia kubwa ya wateja sasa hivi wanapatikana kwenye mtandao na asilimia kubwa ya biashara zinajitangaza kwenye mitandao,hii inachangiwa na ukuaji wa teknolojia na upatikanaji wa taarifa nyingi muhimu kwa urahisi. Njia nyingine inayotumika ni kujitangaza kupitia mteja wako,biashara nyingi sasa hivi ziko kwenye utaratibu wa kutoa kamisheni kwa mteja atakae leta mteja mwingine,kwa sababu marketing ya mteja huwa ya uhakika na ya uzoefu hivyo humvuta mtu zaidi kutumia bidhaa au huduma. Hivyo ukiangalia njia zote mbili hapo juu ni kama zinaua soko la watu wa masoko badala yake linaongeza soko kwa watu wa teknolojia na habari hali imebadilika hii inakuja pia kama changamoto kwa sekta nyingine ya waliomo ndani ya kada ya kutafuta masoko na wanaofikiria kujiunga yafaa kuangalia zaidi mbele na dunia itahitaji nini zaidi kutoka kwako kwa muda gani

Muonekano wa biashara yako na matokeo yake.

Muonekano wa biashara yako na matokeo yake. Hali ya mzunguko na mfumo wa biashara imebadilika sana hapa nchini na hii imechangiwa na kuongezeka kwa makampuni ya kigeni ambayo yamekuwa yakiongeza chachu ya kuendelea kufanya zaidi ya pale wazawa wanapofanya, na tofauti kubwa ambayo inafanya kampuni nyingi na biashara nyingi za nje kufanikiwa ni Branding, asilimia kubwa ya hizo kampuni huingia nchini tayari zikiwa zimeshajibrand hivyo inakuwa rahisi kupata nafasi katika soko la ndani. Kinyume cha hapo asilimia kubwa ya biashara au kampuni zetu wazawa hazijafanya Branding ambayo ndio uti wa mgongo wa biashara, matokeo yake imekuwa hatuwezi kuuza ndani sababu hazina muonekano mzuri na hatuwezi kuuza nje sababu pia hazijafanyiwa branding nzuri. Baada ya serikali kuiona changamoto hiyo ikaanza kusisitiza wafanyabiashara kufanya branding vizuri( kuboresha  utengenezaji na upakiaji wa bidhaa uwe mzuri na wa kuvutia ili bidhaa zetu zipate nafasi hata katika soko la nje kwa wingi). Hivyo maba

Nembo yako inamaanisha nini?

Je wewe ni mfanya biashara au mjasiriamali au mfanyabiashara?umetengenezaje nembo yako? inakidhdi vigezo vya soko lako? Kwanza Logo ni alama au nembo iliyodizainiwa mahsusi kwa ajili ya biashara yako, inayotumika kukutambulisha nje na ndani ya ofisi. Au Logo ni alama au nembo inayotumika kutambulisha huduma,bidhaa,kampuni au mfumo wowote wa vikundi. Kwanini biashara yako inahitaji nembo 1.Humpa mteja maana au tafsiri ya biashara yako japo inaweza kuwa sio sawa na ya kwako 2.Huonyesha muonekano unaotakiwa 3.hukuongezea hadhi 4.huonyesha utofauti wako na wengine katika soko 5.Kuwa na muonekano wa kuvutia 6.Hujipanga yenyewe kwa malengo flani ya soko. Vitu vya kuangalia unapotengeneza logo 1. Iwe ya kipekee 2. Inatakiwa iwasilishe uhalisia wa biashara ,bidhaa au huduma 3. Iwe na uwezo wa kuonekana kwa wateja unaowategemea 4. Iwe na uwezo wa kusimama na kujiimarisha muda hadi muda ( isipitwe na wakati) 5. Iwe na uwezo wa kutumika na kuoneka kwenye kila nyanja ya mawasiliano.