Posts

Showing posts from May, 2016

Mafanikio ya biashara yako na muonekano wake

Mafanikio ya biashara yako yanategemea sana muonekano wako ambao hutengeneza uaminifu,heshima na kumvuta mteja, iwapo muonekano ukiwa tofauti na lengo mteja husita kufanya hivyo vilivyopo hapo juu, kitu kikubwa ambacho kwa sasa kinachukuliwa cha kawaida katika kuipandisha na kuipa muonekano biashara yako ni fani ya Graphics design. fani hii kwa sasa imekuwa ni kama imeingiliwa kila anaetumia kompyuta basi anaweza kuwa graphics designer,hili limepelekea hadi sasa ubora wa muonekano na uhalisia wa kwanza wa biashara unapotea. Nguzo kuu ya Graphics design ni lazima dizaina awe anajua Branding,Maumbo,Mpangilio,fonts na rangi lakini sasa hivi vingi vinapuuzwa na kulifanya soko kuwa la kawaida,Je katika vitambulishi  vyako vyote viko sawa kulingana na maana ya rangi,maumbo,mpangilio na fonts kufuatana na uasili wa biashara yako? Makampuni makubwa husimamia zaidi suala la muonekano wao wanapokupa kazi wanatoa hadi na vipimo muonekano unaotakiwa na vipimo vya rangi ili usibadilishe muonek

Je unafahamu biashara yako inatakiwa iwe na muoneako gani ili iuze?

Serikali ya awamu ya 5 inapeleka mambo kasi na inathamisha katka mifumo tuliyoizoea na kutupeleka katika mifumo mipya, moja kati ya mabadiliko yanayoongelewa sana na yanayohitajika sana ni kukuza pato la taifa na kupandisha thamani ya pesa yetu hii inamaanisha ni kupunguza uagizaji na kuongeza uzalishaji kutokana na hilo serikali inashauri biashara ziongeze kujitangaza na kuuza nje ya mipaka ya Tanzania ili tuongeze kupokea malipo ya Usd kuliko sisi kulipa Usd.  Sasa basi moja kati ya kada zinazoangaliwa katika hili ni kada ya biashara ambapo inapokea urasmishaji na uboreshwaji wa mipango ya kimaendeleo kwa kasi sana hivyo biashara nyingi ambazo hazikuwa zimejipanga sawasawa kwenda na kasi yoyote nyingi zitakufa, lakini katika urasimishaji huu biashara haiongelei sana bidhaa ila inaongelea vitambulishi vya bidhaa, Katika mkutano wa wafanyabiashara kutoka India uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana rai yao ilikuwa ni kuboresha upakiaji na vifungashio vya bidhaa zetu hivyo kinachole ta shi

Itambue kanuni kuu ya pesa

Kila kitu katika dunia hii kina kanuni aidha unaijua au hauijui, unaitambua au hauitambui leo nitaiongelea kanuni kubwa kabisa ya kwanza ya pesa. Kwanza kabisa nikubadilishe mawazo kuhusu upatikanaji na dhana ya mzunguko wa pesa. Kwanza ukubaliane na mimi kwanza kuhusu pesa kwamba, pesa uliyonayo mkononi,mfukoni,benki ama sehemu yoyote ile ambayo unaweza kuitoa kama unavyojiita mmiliki ile pesa sio ya kwako sababu kila pesa unayoishika tayari inasehemu au kazi ya kufanya na kama inasehemu au kazi ya kufanya inamaanisha inabidi ile pesa itoke mkononi mwako, hivyo wewe ni muwakilishi tu umeishika kwa muda huo ili uipeleke kwa mwingine, mfano Ukipewa 10,000 sasa hivi unajihisi kama wewe ni mmiliki wake lakini katika ulimwengu wa fedha wewe umekuwa daraja la mzunguko wake, hivyo kama ni daraja inabidi uipitishe ambapo lazima utaitoa na kumpa mtu mwingine hiyo pesa ambae hata yeye akiisha kuishika inakuwa sio yake tena inabidi akaitoe mfano umeenda kununua unga ukampa 10,000 atakurudishi

Jinsi ya kutengeneza matokeo chanya kupitia business card yako.

Je unaitumiaje fursa ya kujitangaza kupitia Business card yako.japo bzcard ni kikaratasi kidogo kinaweza kukupa matokeo chanya zaidi ya vingine kwanza ni kidogo NA pia ni rahisi kukitunza tofauti na vingine hivyo ukikipa muonekano na maelezo sahihi kina matokeo chanya zaidi.lakini tuangalie hapa chini kwann tunakosea. kwanza Wengi wetu tumefanya business card kama karatasi ya namba tu,Ndio.Kwa nchi zilizoendelea bzcard imebeba namba tu labda na website.lakini kwa huku kwetu hali iko tofauti watu wengi hawakokaribu sana na matumizi ya mtandao zaidi wanatumia mtandao kupitia mitandao ya kijamii,hii inapunguza fursa ya kuitembelea tovuti yako. Pili asilimia kubwa ya watengenezaji na watengenezewaji huhisi bzcard ni bzcard tu haijalishi,lakini iko tofauti hata dizaini za bzcard zinatofautiana kulingana na kada tofauti tofauti,ukikosea kuitengeneza usitegemee kama atakaeiona atakufikiria kupitia kada yako.Mfano biashara ya chakula ikatengeneza bzcard kama za benki utaigusa ile bzcard unap