Posts

Showing posts from April, 2019

Elisha Chuma : Maana ya mawasiliano

Image
Watu wengi wanapowasiliana mawazo yao ama fikra zao huwapeleka kwenye kujibu kabla ya kuelewa kwanza na ndipo hujitokeza ile dhana uanongea na mtu unahisi anakuelewa halafu baada ya muda ndio anakufata anakwambia "kwa hiyo kumbe pale ulimaanish hivi" hii ni dalili moja wapo kwamba  mtu huyu hakukusikiliza ili akuelewe ila akujibu kwanza,mimi na wewe ni mashahidi wa vitendo hivi mara nyingi na kulingana na mazingira tumejikuta tumesahau kurekebisha tabia hii ambayo imekuwa na madhara makubwa kwa watu wengi. Kwenye usaili sasa hivi kampuni nyingi zinatumia mbinu ya kupima uwezo wa mtu kuelewa kama kigezo moja wapo cha kumuajiri  mtu,maswali utakayoulizwa asilimia kubwa ni ya kukupima kiwango chako cha uelewa hii yote ili kuhakikisha ni mtu sahihi nje ya weledi alionao,unaweza kuwa na ujuzi ama uwezo mkubwa wa kufanya kazi ila kama hautakuwa mtu wa kuwasiliana kwa kuelewa inamaanisha ile dhana ya "team work" inakuwa inapotea sababu hautaweza kufanya kazi vizuri na

Tofauti kati ya ukweli na uhalisia

Ishi kiuhalisia endana na uhalisia wako,huenda ukweli unakuvuta ili usimame mahala ama kuonyesha uwezo lakini uhalisia ndio sehemu pekee unayoweza kuwa na amani na kutengeneza mafanikio yako. Watu wengi wamefeli kwa kuusimamia ukweli kuliko uhalisia mathalani,ukweli ni kwamba unahitaji kula ili uishi uhalisia ni kwamba unahitaji kufanya kazi ili upate hela ya kukuwezesha kununua chakula ili uishi. Wasanii,wafanyabiashara na watu wengi wamefelishwa sana na hiki kitu na bado kinawatafuna wengi kuung'ang'ania ukweli ilhali uhalisia unakataa ndio matokeo yake unaishi maisha yasiyokuwa ya kwako mwisho wa kuishi hivyo ni kufeli. Ishi maish a yako ya uhalisia utapata amani ya moyo na ni rahisi kutengeneza mafanikio na mbinu zake ukiwa kwenye uhalisia kuliko kwenye ukweli wako. #Maishanihayahaya #wakubadilikaniwewe