Posts

Showing posts from May, 2014

Mambo yanayorudisha nyuma wajasiriamali/Wafanyabiashara

Kuna mambo mengi ambayo wajasiriamali wengi huyaangalia kama hayana nafasi sana   wanapoanza ujasiriamali lakini baada ya muda na mambo kugeuka ndipo hukumbuka umuhimu wake, na mengi kati ya hayo huwa yanakataliwa na misemo ya mitaani ambayo huwa inaathari za moja kwa moja au vinginevyo kwa mfano maranyingi unapoamua kufanya kitu huwa unafuta mawazo yote ya kufeli ingawa katika hali halisi kufeli kupo katika hilo hilo unalolifanya na wengi huwa wanatumia msemo wa " unapofanya jambo fanya kwa moyo wote usiwaze kufeli sababu utapunguza ari" uwezekano ni ukweli ukiwaza kufeli unapunguza ari ya kulifanya jambo lakini Je unalolifanya linakufeli au halina? Na je ukifikiria kufeli unapunguza ari kwa kuliogopa jambo au kwa kuchukua tahadhari iwapo utafeli? .vivyo hivyo na kwa wajasiriamali wengi pia huwa hawawazi kufeli katika wanachokifanya ni kushinda tu muda wote lakini ukiangalia ukweli ni kwamba hata katika maisha yao ya kawaida mipango yao sio yote inayofanikiwa. Utakuta baada

Vitu ambavyo vinatakiwa vionekane kwenye nembo yako

Iwe ya kipekee Watu wengi wamezoea kuwa wanatengeneza logo kwa kuigilizia ya sehemu fulani au kwa kufuatisha mfumo wa kampuni fulani , wengine hufanya kama logo nyingine kisa tu ni kwa vile imempendezea machoni kwake au ameipenda bila kujali ujumbe utakaotoka baada ya hapo, nembo yako mara zote inatakiwa  iwe ya kipekee na isifanane na nembo yoyote dunia nzima. Hasa katika soko ulilopo, unatakiwa kuifuata maana halisi ya nembo kama nembo ni utambulisho wako iweje uwe unafanana na utambulisho wa mwingine na iwapo umeigilizia kutoka kwa mwenzako inamaanisha tayari yeye brand yake ni kubwa kuliko yako hivyo ukitengeneza nembo inayofanana nayakwake ni kama vile unamsaidia kumkumbushia watu na kumtengenezea nafasi katika vichwa vya wateja wake. Mfano: leo hii ukipita sehemu ukaona nembo inayofanana na ile nembo ya brand ya cocacola utamkumbuka nini brand ya cocacola au brand ya yule aliyeitengeneza . Ukweli ni kwamba utaikumbuka cocacola na unaweza hata kuanza kujiuliza kama wa

Muendelezo wa umuhimu wa Logo katika biashara yako

Image
Kukutambulisha katika soko Logo yako ndio inayokutambulisha katika soko la ushindani ,soko la biashara  na hata kwa wateja hivyo logo yako inatakiwa iwe ambayo ni maalum kweli ili utambulisho wako usije kuwa na muonekano mbaya au usiovutia logo yako ndio ambayo inatathminiwa ndani ya soko mtu anapoiona logo yako ndio anakutambua. Logo ni muongozi wa biashara yako  kwa sababu unapokutana na mteja ananunua kitu kutokana na utambulisho na muendelezo wa logo ya bidhaa unayotengeneza siku sio nyingi nilipokea simu kutoka kwa mtu nisiemfahamu akawa anataka nimtengenezee logo kawaida yangu huwa ni kupata maelezo nikamuuliza ameipatia wapi namba yangu na aina ya logo anayotaka alishangaa kidogo kuona nakuwa na maswali kumzidi lakini alielewa na kitu alichokuja kunijibu ni aliona business card yangu kwa mtu akawa amependa logo yangu ikawa imemvutia kiasi kwamba akawa anataka nayeye  nimtengenezee nyingine lakini iwe jamii ya hiyo ya kwangu, hivyo logo yako ni muongozo wa bi

Logo/Nembo na Biashara yako

Image
Katika matoleo yangu ya nyuma nilielezea vitu vinavyotengeneza biashara yenye afya na moja kati ya vitu hivyo ilikuwa ni nembo (Logo) leo nitaelezea kwa undani kidogo maana yake katika nyanja ya biashara na kwanini biashara inahitaji logo. Logo/Nembo ni nini? Nembo ni alama maalum inayokutambulisha sehemu fulani katika jamii, hiyo ni maana ya nembo kwa ujumla lakini nembo ( logo) maana yake haitofautiani  sana na maana ya hapo juu,logo maana yake ni alama ya utambulisho wako katika biashara ambayo inatengenezwa kwa umakini na utaalamu maalum kwa ajili ya biashara yako. Logo/Nembo inamaana gani kwako Imekuwa kawaida kwa watu kutengeneza nembo mtu anapomiliki biashara basi anajua kitu cha kwanza ni nembo japo hajui inaumuhimu gani katika biashara nilishawahi kukutana na mmiliki wa biashara moja nikamuuliza kwanini ananembo katika biashara yake  majibu yake ilikuwa ni " kama biashara lazima na mimi niwe na logo, na unapomiliki biashara nembo ni lazima

Nukuu za Elisha

Image