Posts

Showing posts from January, 2017

Wazo la biashara 01

Asilimia 80% ya dawa tunazotumia mahospitalini zinatokana na miti,na asilimia 60 ya magonjwa tunayougua yanatokana na mtindo wa maisha, hivyo ukiwa kama mjasiriamali ama mfanyabiashara unatakiwa uone fursa hapo katikati ya kuugua na miti. Matunda yanatumika sana kama dawa, na chakula ni dawa ndio maana ukikikosea kinakuwa sumu mwilini sasa tupitie fursa hii,ikakufungue na kukupa maono mapya. FURSA: Unaweza  kuuza ujuzi  ama kuwa mshauri wa masuala ya chakula,matunda na miti. JINSI YA KUIFANYA: Kama mtumiaji wa mtandao anza kwa kutafuta na soma kwa makini    matumizi,faida,utengenezwaji,uhifadhi na mfumo wa mwanadamu unavyopokea na unatumia nini kwa matunda ambayo yanapatikana sana eneo lako ama yanayopatikana kwa urahisi ( Mfano kuchanganya tunda lenye ukali na lisilokuwa na ukali unaliua lile tunda lisilokuwa na ukali linakuwa pombe(Nanasi na ndizi).),fuatilia na chakula uandaaji,viungo,upishi na kadha wa kadha hakikisha unatambua kila aina ya chakula tunda na miti kazi ambazo zina

Tunza muda

Tunza sana muda wako, usiutumie muda wako kwa mazoea. Kwenye maisha pesa unaweza kuzitafuta na ukazipata lakini muda ukipita haujirudii tena kila sekunde, kama unafikiria kuwa na mafanikio hebu jiangalie unatumia muda kiasi gani kwa ajili ya uzalishaji katika siku yako. Anza upya badilika sasa...Jali muda #2017 #maishanihayahaya  wakubadilika ni wewe.

Tambua maana halisi ya fedha

Dhana ya  fedha haiko katika ile karatasi unayoishika yenye namba za thamani yake. Fedha yoyote unapoikea unaenda kuitumia hata kama sio moja kwa moja lakini wewe ni mwakilishi tu wa hilo karatasi ndio maana hazina mwenyewe unaishika wewe unaitoa anaishika mwimgine. Kama lile karatasi sio fedha basi fedha halisi iko wapi?...Fedha halisi iko kichwani mwako unapoifikiria na kuishughulikia hadi kuifanikisha hapo ndio unakuwa unafedha ila ukiisha kuishika tu wewe inakuwa sio ya kwako bali mtu mwingine ndio anakuwa anaiwazia na kuishughulikia aipate. Hivyo hakikisha kichwani mwako unatengeneza pesa nyingi bila kuchoka na jitahidi pia kuzishughulikia ukishazipata tu achana na zilizoingia sababu hata ufanyeje dhima ya pesa ni matumizi hivyo utaitumia tu.Ili kuwa katika sehemu nzuri kila siku tengeneza pesa akilini mwako. Ungana nami kwa dondoo na ushauri zaidi kuhusu ujasiriamali na biashara Jumatatu - Ijumaa saa 12:45ash - 1:00asubuhi (Maisha mseto) Redio Times fm 100.5 Kila Alhamisi s