Posts

Showing posts from 2023

TAMBUA : BIASHARA NI RAHISI KUIFANYA KWA KUFIKIRI ZAIDI YA UHALISIA WAKE

Image
Wapo watu wengi waliofeli kwa changamoto ya kuifanya biashara kwa kichwa zaidi ya uhalisia wake, yako mambo mengi ya kufahamu kuhusu biashara lakini la kwanza katika yote ni kutambua uhalisia wa biashara kwa kuwa na taarifa sahihi na sio maelelzo ya kufikirika. UTAFELI VIBAYA kwa kutegemea taarifa za kufikirika. Niambie ulijaribu biashara gani kwa kufikiri na uhalisia wake ukakukataa? Ikiwa unahitaji ushauri ama usimamizi bora wa biashara yako wasiliana nami sasa : 0745 108010 ——————————- Mahusiano ndio msingi mama wa mafanikio yetu kila linalofanyika liko chini ya kiwango sahihi cha mahusiano, unaifahamu Saikolojia ya Mahusiano?, Kama bado tayari nimekuandikia kitabu ambacho kitakuongoza kujenga ufahamu chanya wa nini maana na saikolojia ya mahusiano kwako na kizazi chako. Jipatie leo nakala yako kwa Tshs 20,000/= nakala ngumu na Tshs. 25000/= nakala ya sauti. Kukipata wasiliana nami leo  0745108010 #echumaarifa #ujasiriamali #maisha #daressalaam #elishachuma

JENGA MAZOEA YA KUANDIKA MAWAZO YAKO.

Image
Akili zetu zimeumbwa kuwa na maboresho ya mawazo kulingana na msimu ama uhitaji husika, hii imekuwa ni changamoto kwa watu wengi sana wanapofikiria kuanzisha ama kukamilisha malengo yao, wanapoanza wazo linakuwa jingine na wanapoendelea pia wazo linakuwa jingine hii inapelekea kupoteza nguvu katika kusimamia misingi ya wazo la kwanza. Sasa basi jitahidi sana uwe unaandika mawazo yako ili unapoyafanyia kazi uwe na sehemu ya kumbukumbu ambayo utaitumia kwa ajili ya kukuongoza katika yale ambayo unafikiria kuyafanya, kuandika inaweza kuonekana kama ni kitu kidogo sana katika utendaji lakini ni kitu kikubwa sana kisaikolojia na pia hata kimalengo. Nijulishe hapa chini, na wewe ni mtu wa kuandika malengo yako au unakiamini kichwa chako kwamba siku zote utakumbuka na kulisimamia lengo mama. Bado kitabu cha Saikolojia ya mahusiano kinapatikana, ni kitabu maalum kwa ajili ya kuinua na kurudisha uelewa bora wa mahusiano kuanzia yale ya mzazi na mtoto hadi yale ya kimapenzi, saikolojia yake isip