Posts

Showing posts from January, 2020

Tofauti ya kupenda kati ya mwanamke na mwanamme

Image
Tofauti ya kupenda kati ya mwanamke na mwanamme. Watu wengi kwenye mahusiano huchanganya kipi kinahitajika wapi na kipi kinawekwa wapi,ugomvi na kutokuelewana vinachukua sana nafasi sababu kila mtu hajui anakosea wapi na anajiona yuko sahihi. Iko hivi utambue leo. Mwanaume maisha yake yote hahitaji kupendwa,uhitaji wake mkubwa kwenye mahusiano sio kuonyeshwa anapendwa ama kufanyiwa vitu vya kudhihirisha upendo wako,atavichukulia kawaida wakati wewe umevichukulia pakubwa sana na utalalamika hupendwi,kumbe umemkosea hitaji la mwanaume kwenye mahusiano ni "Heshima" mwanaume anahitaji kuheshimiwa tu,ukimuheshimu kwake ni tafsiri ya unampenda ndio maana ili kumlegeza mwanamme na kukupa unachotaka mwanamke akishusha sauti na akaongea kwa upole,ustaarabu na utii mwanaume hufanya kile mwanamke anachokitaka sababu ameonyesha heshima,hivyo mwanamke usipambane kuonyesha unampenda ila onyesha unamheshimu. Lakini hali iko tofauti pia kwa mwanamke yeye anapenda kwa hisia na kudhahania,

Hatua za kufuata unapofikiria kuanza kufanya biashara yoyote

Watu tumezoea kudanganyana na kutokuelezana ukweli kuhusiana na biashara, tumekuwa watu wa kupeana moyo na kushauriana kila mtu afanye biashara lakini biashara au ujasiriamali sio kitu rahisi kiasi hicho ambacho kinaweza kufanywa na kila mtu. Hivyo usijitumbukize tu katika bishara kwa kufuata mkumbo aidha umeambiwa biashara fulani unaiweza, biashara fulani inalipa au wewe unaweza kufanya biashara fulani na ikakulipa, kila kitu kinaugumu wake na changamoto zake, changamoto za muuza maandazi ni tofauti na changamoto za muuza duka,hata ujuzi wa msusi ni tofauti na wa kinyozi japo wote wapo saluni,hivyo unapoamua kufanya biashara fulani usikurupuke fikiria na tathmini kwanza kwa undani kama inaendana na wewe zifuatazo ni baadhi ya njia au mbinu muongozo za kufuata unapotaka kuanza biashara yako. Wazo la biashara. Kitu cha kwanza unachotakiwa utafute ni wazo la biashara,hii itategemea na eneo pamoja na asili ya kazi yako (kwa muongozo wa jinsi ya k