Posts

Showing posts from November, 2014

Mabadiliko ya lazima kwa wafanyabiashara na wajasiriamali Tanzania

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa mwenendo wa biashara unavyoenda hapa nchini basi utakuwa umeshagundua kuna mabadiliko makubwa yanayoendelea ndani ya nchi hii, na sababu kubwa ya mabadiliko hayo ni kutokana na Tanzania imekuwa ikifanya biashara kienyeji kwa muda mrefu na sasa imeonekana  katika ramani ya dunia wawekezaji na makampuni mengi ya kigeni yanakuja kufungua matawi na kuanzishwa hapa nchini hivyo serikali yetu imeona ni bora ianze kuwatengeneza wafanyabiashara mapema kabla haijajaa wawekezaji mfano: Serikali haikuwazoesha wafanyabiashara kulipa kodi kwa EFD lakini imegundua kuna fedha nyingi zinapotea iwapo hawatatumia EFD ndio maana wakaamua kuwabana lakini kwa kuwa hawakuzoeshwa leo hii hadi Wahindi na Wachina ikiwa ni mgomo wa kufunga maduka nao wamo japokuwa kwao mtindo huu unatumika kitambo na biashara ni ushuru, lakini huku nao wako mstari wa mbele kufunga maduka. Baadhi ya mabadiliko haya yanatokea kwa kutangazwa na mengine hayatangazwi Mfano: Serikali iliona wimbi kubwa