Posts

Showing posts from January, 2015

Sehemu ya pili:Sababu 14 kwanini biashara yako inahitaji kuwa na nembo na vingine vya kutafutia masoko

Pia ningefurahi kupata mrejesho wako (feedback) juu ya uzi ninazotoa  ili nijue pia kama jamii na mlengwa ninaemtegemea amepata elimu unaohitajika,kwa kuacha komenti yako hapo chini kwenye sehemu ya Comment, Asante. 8. Kueleza jina la kampuni yako Unapotengeneza nembo au unapotoa flyers na bidhaa nyingine inayokutambulisha kwenye soko  hapo ni kuliweka jina la biashara au kampuni yako katika vichwa va wateja wako watarajiwa,ambapo ili mteja akutafute ni lazima awe anakukumbuka au anajina lako ndio anaweza kukutafuta mfano: Unaposikia bidhaa za Azam tayari unakumbuka na SSB Company ( Bakhresa). 9. Kutunza jina la kampuni yako kwa mteja Mteja mara zote anahitaji kitu cha kumkumbusha ili aweze kukukumbuka hivyo kwa kutoa vitu kama business card, flyer na vingine vya namna hiyo hapo unakuwa unatunza jina lako kwa mtu unaemtegemea na kwa yule uliempata na siri za kufanikiwa katika biashara ni kumfanya mteja akukumbuke kila anapofikiria huduma yako na huduma za pembeni yako.

Sababu 14 kwanini biashara yako inahitaji kuwa na nembo na vingine vya kutafutia masoko.

Image
Nimepokea maswali mengi kuhusiana na umuhimu wa kuwa na vitu kama Nembo, Flaya,Tovuti,Broshua na vingine vingi logo/Nembo poster Flyer/Flaya      Leo nitatoa sababu chahche kwanini biashara yako inahitaji hivyo vyote ili ifanikiwe kibiashara. Ukiviangalia vyote kwa juu juu unaweza kuviona sio vya muhimu sana Mfano: Kampuni kuwa na logo wakati hakuna mtu anaekuja kuulizia logo wala hakuna mtu anaekuja kununua logo hivyo ni kitu ambacho unatengeneza kwa gharama na kinaendelea kuwa chako. Vivyo hivyo kwa vingine unatengeneza broshua kwa gharama kubwa lakini unasambaza bure kwa watu na unaweza kumpa mtu hapo hapo akakitupa ,ukiangalia kwa macho ya fedha zangu nimeziweka hapa kipewe heshima hauwezi kuona ninachokimaanisha. Kila biashara inahitaji kuonekana na pia inahitaji kukua bila kukua na kuonekana haiwezi kufanikiwa hivyo kutengeneza Nembo yako ni kujipa muonekano katika soko na kutengeneza vitu kama Flaya,Broshua,Poster hiyo ni kukuza biashara hivyo ili bias

Majibu ya Maswali 12 yahusuyo Branding

Kabla ya kuingia moja kwa moja katika somo la branding nimeonelea nitoe kwanza uzi wenye maswali na majibu kuhusu branding ili hata kwa yule ambae haijui na anahayo maswali ya msingi anaweza kuelewa na kupata picha ya kitu ambacho ninataka kuanza kukitolea ufafanuzi. Branding inahitajika kwa kila biashara na kila kitu kwa sababu hata wewe pia ni brand. chini ni maswali na majibu kuhusu Branding Brand ni nini? Ans: Brand kwa maana moja tunaweza kusema ni muonekano wa biashara yako, branding ni muonekano wako kuhusu biashara yako  na jinsi gani biashara yako inajitofautisha na washindani wenzako, Kazi za Brand . Brand  hutambulisha muonekano ,ubora  wa kuaminika kwa watu, huku bidhaa za generic (kawaida)  hazijulikani  na haziaminiki ,hata hivyo brand ni ghali na inahitaji mipango ya muda mrefu Brand hutofautisha bidhaa na hufanya bidhaa kutambulika mapema Brand inaruhusu mtumiaji kutengeneza maamuzi na matumizi ya bidhaa Brand hutengeneza thamani halisi

Salamu za Mwaka mpya

Natoa Shukrani zangu za dhati kwa Muumba wa mbingu na nchi kwa kusimamia na kuniwezesha kufika mwaka 2015 najua yote ni mapenzi yake ni wengi walitamani lakini hawajaifikia siku ya leo pia niwashukuru wote walionitumia salamu za heri ya mwaka, nami kwa mapenzi ya dhati nakutakia heri ya kuufikia mwaka 2015. nakutakia uwe ni mwaka wa mafanikio na kufikia malengo yako. Mwaka 2014 umekuwa ni mwaka wa mafanikio na changamoto pia kwa kila mtu hivyo nimeelezea kwa undani na kwa ufupi kuhusu biashara na ujasiriamali, mwaka huu nitajikita zaidi kwenye jinsi ya kuifanya biashara yako ifanikiwe au njia za kuikuza biashara yako unapoanza au unapoendelea na biashara yako. Branding ni neno ambalo nimeishakulitaja sana katika matoleo yangu na kwa mwaka huu nataka kila msomaji wangu na wote wanaonifuatilia wafanye brand ya biashara zao.  Brand ni neno la kiingereza lenye maana isiyokuwa na uwezo wa kushibishwa kama lilivyo kwa lugha ya kiswahili ambapo unaweza kuiita Brand kama chapa lakini k