Posts

Showing posts from August, 2015

Pitia chapisho hizi zitakusaidia kupata wazo la biashara

Image
Baadhi ya machapisho yahusuyo wazo la biashara kutoka elishachuma blog. 1. jinsi ya kupata wazo la biashara 2. Vitu vya kutambua kabla ya kuwa mjasiriamali au mfanyabiashara 3. Tahadhari kwa wafanyabiashara na wajasiriamali 4. Hatua za kufuata unapofikiria kuanza ujasiriamali 5. Tofauti kati ya mfanyabiashara na mjasiriamali Kujiunga na kundi la whatsapp branding tuma namba na jina lako kwenda namba 0684047323 (Whatsapp sms tu), pia unaweza kunipata kwa ukaribu zaidi kwa kuniandikia email(elishachuma@gmail.com) au like page yangu  Elisha Chuma .

Vitu vitano (5) vitakavyokusaidia kufanikiwa katika eneo lako la biashara.

Image
Leo nataka nikupe siri 5 za vitu ambavyo ni vya kawaida sana tunavyovifanya kila siku katika maisha ya kawaida lakini tunavifanya aidha kwa mazoea au kwa kurithi leo nnakupa mwanga na sababu kadhaa za kwanini unatakiwa kuziwekea mkazo hizo sehemu au vitu hivyo kwa manufaa ya biashara yako, katika Branding hakuna kitu kipya ambacho utakutana nacho ila utakutana na elimu ya jinsi ya kutumia vitu kwa usahihi ili vilete malengo chanya katika biashara yako.Jifunze branding mara nyingi uwezavyo ni msingi au mhimili wa bishara yako. 1. Waza tofauti (Ushindani ndio biashara) Katika vitu vitano (5) ambavyo ukivishika vizuri na kuvifanyia kazi kwa umakini vitakusaidia kufanikiwa katka eneo la biashara yako ni jinsi unavyowaza, mawazo yako ni hazina kubwa katika biashara yako. Unatakiwa kama mfanyabiashara au mjasirimali  uwe na mawazo chanya uone nafasi kwenye changamoto(tatizo) kwenye kila hatua kitu kikubwa kinacho waangusha wengi ni kuchukulia changamoto kama tatizo hivyo hujikuta hata c

Vitu vya kuzingatia unapotaka kuanza au ukiwa mjasiriamali ili ufanikiwe.

Image
Kwanza niwape hongera ambao tayari wameshafanikiwa kupata vitambulisho vya kupigia kura kwa nchi nzima na niwape pole kwa wale ambao bado hawajapata na pia nnawatia moyo kuendelea kuvifuatilia vina maana sana kwa maisha yako naya kizazi chako cha sasa na cha baadae. Baada ya kutoa salamu hizo sasa nirudi kwenye mada kuu leo hapo juu, taifa letu linapoteza sana nguvu kazi ya taifa katika vitu ambavyo havina mafanikio na malengo chanya kwa maisha ya mhusika na taifa na kutokana na kupunguza umakini katika hilo sasa hivi tumejikuta vijana wengi wanamaliza mafunzo ya elimu zao lakini hawana kazi wanabaki kuwa omba omba na wadandiaji wa kazi wasizokuwa na weledi nazo. Leo nitaongelea kwa upande wa wajasiriamali wadogo ambao wanafanya biashara ndogo ndogo kwa minajili ya kupata kipato cha kuendesha maisha yao ya kila siku na wale ambao wanafikira kuingia katika ujasiriamali au biashara. Asilimia kubwa sana ya vijana wanafeli katika biashara na ujasiriamali kwa kukosea baa