Posts

Showing posts from June, 2019

Aina za malengo na mipango

Image
Aina za Malengo na mipango Katika maisha ya kila siku kila mtu hutengeneza malengo na mipango ya kufikia kilele fulani,lakini kutokana na kutokuwa na aina kamili ama sahihi za malengo na mipango watu wengi hujikuta malengo na mipango yao inafeli kwa sababu hujiandaa kwa vitu vichache kuliko uhalisia wenyewe. asilimia kubwa ya watu hutengeneza mipango bila malengo na matokeo yake ile mipango hufeli sababu hakuna malengo kamili,katika maisha ya kila siku kuna mipango ya aina 2 (mbili) na katika malengo kuna malengo ya aina 7 (saba). hivyo unapofikiria kutengeneza mipango na malengo yako ili ukue na kufikia kile unachokihitaji ni lazima malengo yote yakamilike ndio mipango itafanikiwa kwa ufasaha. Aina za Mipango - hizi sio aina ngeni kabisa kwa watu japo wengi hawajui kuzitumia na kuitofautisha,kuna mipango aina 2,mipango ya muda mrefu na mipango ya muda mfupi,ili ufanikiwe unatakiwa kuwa na mipango ya muda mrefu ambayo itakuwa ndio imebeba lengo kuu kwa vile safari ya ku

Jifunze kupokea matatizo kama changamoto

Image
Jifunze kuwa mjasiriamali mzuri,ukiyabadilisha mazingira na unayoyaita matatizo kuwa changamoto,utaanza kuziona fursa kupitia changamoto yako,badilisha aina ya mawazo yako usiishi ndani ya boksi la uwezo na uelewa wako toka nje ya boksi lako utaona vitu katika hali ya tofauti sana. Mfano mdogo ni masikini siku zote anaomba majaribu ama matatizo yasimpate ili aendelee kusimamia eneo lake,lakini anaefanikiwa anatamani changamoto za kiwango cha juu ili atatue na kupanda kiwango,hali hii inakuja hata kwenye nyumba za ibada wanaojihisi hawana wanawaachia michango wanaohisi wanacho mwisho wa siku aliekuwa nacho anaongezewa na asiekuwa anacho ananyang'anywa. kila kinachopita kwako ni thawabu inategemea na vile unavyokichukulia aidha kitakujenga ama kitakubomoa,chagua kujengwa ili kesho uwe bora zaidi ya jana,hakuna asiekuwa na changamoto ila tofauti ni jinsi ya kuzipokea na kuzifanyia kazi. Elisha Chuma Snr www.elishachuma.blogspot.com