Posts

Showing posts from May, 2023

JENGA MAZOEA YA KUANDIKA MAWAZO YAKO.

Image
Akili zetu zimeumbwa kuwa na maboresho ya mawazo kulingana na msimu ama uhitaji husika, hii imekuwa ni changamoto kwa watu wengi sana wanapofikiria kuanzisha ama kukamilisha malengo yao, wanapoanza wazo linakuwa jingine na wanapoendelea pia wazo linakuwa jingine hii inapelekea kupoteza nguvu katika kusimamia misingi ya wazo la kwanza. Sasa basi jitahidi sana uwe unaandika mawazo yako ili unapoyafanyia kazi uwe na sehemu ya kumbukumbu ambayo utaitumia kwa ajili ya kukuongoza katika yale ambayo unafikiria kuyafanya, kuandika inaweza kuonekana kama ni kitu kidogo sana katika utendaji lakini ni kitu kikubwa sana kisaikolojia na pia hata kimalengo. Nijulishe hapa chini, na wewe ni mtu wa kuandika malengo yako au unakiamini kichwa chako kwamba siku zote utakumbuka na kulisimamia lengo mama. Bado kitabu cha Saikolojia ya mahusiano kinapatikana, ni kitabu maalum kwa ajili ya kuinua na kurudisha uelewa bora wa mahusiano kuanzia yale ya mzazi na mtoto hadi yale ya kimapenzi, saikolojia yake isip