Posts

Showing posts from 2013

Aina za washindani katika biashara

Katika kila biashara lazima kuwe na washindani, biashara isiyokuwa na washindani hiyo sio biashara   na katika biashara Ushindani ni wa muhimu kwa ajili ya maendeleo ya biashara yoyote na   moja kati ya faida za washindani ni kuongeza changamoto za ufanisi wa kazi,kuna aina kuu   tatu za washindani Washindani wa moja kwa moja Hawa ni washindani ambao unawafahamu na mnashabihiana biashara,mnafanya biashara ya aina moja,kwa mfano kama biashara yako ni fundi cherehani basi mafundi cherehani   wengine ndio washindani wako wa moja kwa moja. Washindani wasiokuwa wa moja kwa moja Hawa ni washindani ambao wanatengeneza bidhaa au shughuli mbadala ya za kwako, wanatengeneza   aina ya bidhaa ambazo kama mteja asipotumia za kwako basi atatumia za kwao. Mfano: kama wewe ni fundi cherehani washindani wako ambao sio wa moja kwa moja ni wale ambao wanauza nguo madukani za spesho na mitumba hao ni washindani wako pia. Washindani dhahania Hawa ni aina ya washindani ambao

Hatua za kufuata unapofikiria kuanza ujasiriamali

Ujasiriamali sio kitu kidogo kama wengi wanavyofikiria na wengi hufikiria kupokea hasara ni kama vile umefungua duka hujauza vitu hadi muda wake wa kutumika umeisha   ndio unakuwa umepata hasara lakini kwa maana ya ujasiriamali maana iko tofauti kidogo maana ya kukubali hasara kwa upande wa ujasiriamali ni ile hali ya kukubali kutumia nguvu na gharama nyingi kwa ajili ya matokeo ya baadae ,ambapo matokeo hayo yanaweza kuchukua muda mrefu hadi yaonekane. Mjasiriamali ni mfanyabiashara pia na hakuna mfanyabiashara anaefanya biashara kwa hasara kila kinachofanyika katika biashara kinategemewa kulipa hata kama sio sasa, hivyo hata mjasiriamali pia hakubali hasara ila kwa malengo. Hivyo unapoamua kuwa mjasiriamali usikurupuke kwa vile unajiona unaweza kwanza kabla ya yote jitambue   kwanza (tofauti kati ya ujasiriamali na biashara),ukishakuwa na uhakika na hilo   sasa unaweza kuanza kufata hatua zifuatazo,nb: usifanye kwa kuwa unataka kujilazimisha kuwa mjasiriamali fanya kwa kufuata

Hatua za kufuata unapofikiria kuanza kufanya biashara yoyote

Watu tumezoea kudanganyana na kutokuelezana ukweli kuhusiana na biashara, tumekuwa watu wa kupeana moyo na kushauriana kila mtu afanye iashara lakini biashara au ujasiriamali sio kitu rahisi kiasi hicho ambacho kinaweza kufanywa na kila mtu. Hivyo usijitumbukize tu katika bishara kwa kufuata mkumbo aidha umeambiwa biashara fulani unaiweza, biashara fulani inalipa au wewe unaweza kufanya biashara fulani na ikakulipa, kila kitu kinaugumu wake na changamoto zake, changamoto za muuza maandazi ni tofauti na changamoto za muuza duka,hata ujuzi wa msusi ni tofauti na wa kinyozi japo wote wapo saluni,hivyo unapoamua kufanya biashara fulani usikurupuke fikiria na tathmini kwanza kwa undani kama inaendana na wewe zifuatazo ni baadhi ya njia au mbinu muongozo za kufuata unapotaka kuanza biashara yako. Wazo la biashara. Kitu cha kwanza unachotakiwa utafute ni wazo la biashara,hii itategemea na eneo pamoja na asili ya kazi yako (kwa muongozo wa jinsi ya kupata wazo la biashara.angal

Tahadhari kwa wafanyabiashara na wajasiriamali

Taa ya hatari imeanza   kuwaka kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wa Tanzania Asilimia kubwa ya wafanyabiashara, ( wakubwa na wadogo) wanafanya biashara Kienyeji na kikubahatisha wanafanya biashara kama mchezo wa bahati nasibu kupata Kukosa   lakini siku sio nyingi mambo na hali itabadilika na kubadili mfumo wote wa kibiashara Hapa Tanzania. Kwa kuanza kwa sasa watanzaia wengi wanapata hamasa na hamu ya kuwa wafanyabiashara Au wajasiriamali kwa inspiration kutoka nchi za nje, kutoka kwa wajasiriamali wakubwa , kutoka Kutoka katika vitabu vya waandishi wa nje ambao huelezea hali ya biashara au ujasiriamali kwa Kiwango na uwezo wa sehemu walipo na kwa mjasiriamali   wa kawaida akisoma au kutumi mbinu zile Zinaweza msaidia sababu kwa kipindi hicho vitu alivyovisoma sehemu anakovitumia havijulikani hivyo Hata akikosea au kipatia hakuna atakaetambua,hiyo ndiyo hali iliyokuwepo kwa Tanzania ya zamani lakini Kwa sasa hali inabadilika tena sana . Pili Kwa sasa

Vitu vitano vinavyosimamia biashara yako

Biashara pia inavitu ambavyo kila mtu anatakiwa avifuatilie ili uweze kuimanage, biashara nyingi zinafeli   iwapo moja kati ya vitu hivyo vinapopungua au kukosekana hivyo basi kabla ya kuanzisha au kuanza biashara yako jiaminishe unaweza kusimamia vitu vifuatavyo. 1.Branding Branding ni muonekano wa biashara yako kwa mteja unaemkusudia, hii ikiwa inamaanisha lazima ujue mteja wako anataka akuonea katika hali gani ili akuamini , mteja wako unataka apate kitu gani kichwani mwake mara tu akiiona alama yako nakadhalika,kuijua elimu hii kutakusaidia sana katika uendeshaji wa biashara yako kwa sababu itakuwa ni rahisi kwako kujua saikolojia ya mteja wako na kuepusha kufanya yasiyo sawa katika biashara   na pia ukiiifahamu branding itakufundisha pia   njia za   kupambana na wateja na mbinu za kiushindani. 2.Masoko ( Marketing) Masoko ni sehemu ambayo inahitaji umakini mkubwa baada ya kufanya brand ya biashara yako kitu kinachofuata ni kutengeneza na kutafuta masoko ya brand hi

Makosa yanayofanywa na wanaotoa elimu ya ujasiriamali

Kuna kitu ambacho wananchi wanakuwa wanapotea bila kujua kumekuwa na wimbi kubwa la watu wanaohamasisha na kutoa elimu kuhusu ujasiriamali, Sio wote Watu hao wanawasaidia watu,lakini wanaruka sehemu kubwa ambayo inawaumiza sana Watu wanaoamua kutumia elimu yao kwa manufaa yao,mfano kuna wale wanaotoa elimu kuhusu Kutengeneza vitu kama sabuni,shampoo na vinginevyo,hao hutoa tangazo la kuwafundisha watu mbinu Za kuwa mjasiriamali, wao hufundisha namna ya kutengeneza hadi unaelewa halafu wanakuacha.hilo Ni kosa kubwa sana kwa wao kumfundisha mtu kutengeneza kitu kinachofanywa na makampuni makubwa kama kazi yao halafu ukamfundisha yeye kwa shilingi elfu 30, bila kujua atatoka hapo atatafuta fedha ya mtaji na mtaji wa kwanza unaweza kuwa ni 50,000 tu hapo ameshapigia hesabu akiuza anauhakika wa kutengeneza fedha nyingi halafu inakuwa tofauti. Kumekuwa na wimbi kubwa la watu wanaoitwa walimu wa ujasiriamali   wanaofundisha mbinu za ujasiriamali siwapingi wala sikidhani na

Elimu inayokosekana

Elimu inayokosekana na inayowapoteza wengi katika maisha Katika mfumo wetu wa elimu kuna elimu muhimu inayokosekana   na hakuna sehemu ya kuipata hadi Ujitambue mwenyewe ambapo   elimu hiyo ni elimu ya kujitambua, Tatizo lililopo katika elimu yetu ni kwamba tunasoma kwa kufuata taratibu za watu fulani, mfumo wa elimu tunaotumia Ni wa mzungu , ili ujikomboe unatakiwa ujitambue, mzungu alileta elimu lakini haikuwa elimu ya kutufanya tujitegemee Elimu tunayoipata kwenye shule zetu kuanzia ngazi ya chekechea hadi ngazi ya sekondari ni elimu ya lugha na kusoma na kuandika, kama ni hivyo kwa nini basi tuendelee kupoteza muda wingi kusumbukia kusoma na kuandika?. Wanafunzi wanachukua hadi masomo 14 yote ayafanyie mtihani na anatakiwa kufaulu ni uwezo wa hali ya juu unaotumika kwa wanafunzi wanaofaulu, na hicho hakikuwa kizazi cha dot.com ambacho kila kitu wanafunzi wanatumia Mbadala wa google kutafuta.hata kufeli sana kwa wanafunzi wetu kumesababishwa na mabadiliko ya

Maana ya Branding kwa mfanyabiashara na Mjasiriamali

                                           Maana ya branding kwa mfanyabiashara Branding ni muonekano wa biashara yako kwa mteja unaemtarajia   kwa maana hiyo brand Inahusika na inanafasi kubwa katika ukuzaji wa biashara yako na   maendeleo yake kila   jina ni Brand lakini sio kila brand ni jina hivyo ili jina liwe brand linahitaji   vitu fulani fulani ili kuwa hivyo Mfano: Naseeb Abdul ni jina lakini Diamond ni brand. Ikiwa inamaana ya kwamba ili uwe na kitu au Uonekane katika kipengele au sehemu yako ya ushindani ni lazima uwe na brand na sio jina.Ukiwa kama mfanyabiashara ambaye unafanya biashara sio kwa majaribio brand ni lazima katika  biashara yako , Brand inatakiwa kuanza kutengenezwa tangia mwanzo wa biashara   ili kuipa nguvu ya kuwepo sokoni kwa muda mrefu na pia kutengeneza kitu ndani ya vichwa vya wateja wako na wateja unao wategemea Mfano: Serikali ilipoamua kuhama kutoka analojia kwenda dijitali   kampuni nyingi zilikuwa                  hazi

Matumizi ya blogu hii

Blogu hii ni kwa ajili ya kukuza na kuelimisha kuhusu biashara na ujasiliamali blogu hii inasimamiwa na kuendeshwa na Elisha Chuma mwenyewe . Kwa wenye maswali yoyote kuhusiana na biashara , ujasiliamali au kitu chochote ambacho kiko katika mzunguko wa branding,biashara na ujasiliamali unakaribishwa sana. Jinsi ya kushikiriki fungua user name yako na weka swali lako au maoni yako kwenye post itakayokuwepo juu au tuma swali lako kupitia elishachuma@gmail.com na nitalitoa na kuliandikia majibu yake haraka iwezekanavyo kulingana na idadi ya maswali. Asanteni sana na karibu katika ulimwengu wa kuelimishana Elisha Chuma

Tofauti kati ya mfanyabiashara na mjasiriamali (Jitambue)

Tofauti kati ya ujasiriamali na ufanyabiashara Ujasiriamali unaweza kuipata maana yake halisi kwenye Jina lenyewe ujasiriamali ( ujasiri kwenye mali) hivyo ili Kuwa mjasiriamali lazima uwe jasili na   mwenye uwezo Wa kukubali matatizo na changamoto, uwe tayari kupoteza Sasa hivi kwa ajili ya mafanikio ya baadae. Ukiwa mjasiriamali faida za muda mfupi kwako huwa sio za muhimu sana na lengo Kubwa huwa ni kufikia malengo uliyoyapanga na kukamilisha ulichokifikiria Watu wengi hujiona ni wajasiriamali kwa vile tu huwa na uwezo wa kutatua matatizo Ya biashara yake kwa kutumia njia nyingine . Mfano: utakuta mtu anafanya kazi ameamua kuanzisha biashara yake pembeni ya kazi Anayoifanya ambapo inafikia hatua anapata hasara au bashara hailipi kwa muda husika Anachoamua kufanya ni anachukua fedha kutoka sehemu anakofanyia kazi anaziba pengo Lililopo kisha anaendelea na biashara, huyu anaweza kujiona ni mjasiriamali lakini sio Huyu ni mfanyabiashara .

vitu vya kutambua baada ya kuwa mfanyabiashara au mjasiriamali

biashara au ujasiriamali ni ndoto za watu wengi lakini asilimia kubwa husahau vikwazo na vizingiti ambavyo hutokea kabla na baada ya kuwa mjasiriamali au mfanyabiashara  toleo lililopita nilielezea vitu unavyotakiwa kufanya kabla ya kuwa mjasiriamali, leo nitaelezea vitu unavyotakiwa kuvifanya baada ya kuwa mjasiriamali . kuna vitu na mambo mengi ambayo unatakiwa kuyafata ili ufanikiwe katika kila hatua ya biashara au ujasiriamali wako baadhi ya vitu hivyo ni pamoja na                                     Baada ya kuwa mjasiriamali au mfanyabiashara                           1. Biashara ni ushindani, na nafasi ya makosa   Moja kati ya vitu ambavyo unatakiwa kutambua ni biashara ni ushindani ili biashara Iendelee lazima ipate ushindani wa kutosha ndipo biashara itakuwa biashara   ila kama Hakuna ushindani hautakuwa unafanya biashara bali unatoa huduma,mfano kwa kampuni kama Tanesco wao hawafanyi biashara wanatoa huduma kwa sababu hawana mshindani wa m

Vitu vya kutambua kabla ya kuwa mfanyabiashara au mjasiriamali

Vitu   vya kutambua kabla  ya kuwa mfanyabiashara au mjasiriamali   Ujasiriamali  imekuwa ni ndoto ya watu wengi sasa hivi, kila anaepata nafasi au wazo la biashara huanza kujiita mjasiriamali lakini kuna maana na mambo mengi ambayo mtu anatakiwa ayajue kabla ya kuanza biashara na anatakiwa achague kati ya ujasiriamali au ufanyabiashara. leo nitaelezea mambo kadhaa ambayo unatakiwa kuyafahamu kabla ya kuwa aidha mjasiriamali au mfanyabiashara na baadhi ni mambo ya kawaida na tunakutana nayo kwenye maisha yetu ya kila siku lakini ni sawa na ukiona sululu bila kuambiwa ni sululu na inafanya kazi gani utakuwa unaona iko kama uma lakini unaweza kupatia  au kukosea matumizi yake kwa kuiona tu, vivyo hivyo hata kwenye ujasiriamali pia kuna vitu ambavyo unatakiwa kuvifahamu.unaweza kuvifanya bila kuambiwa na ukawa sawa ila ukiambiwa utaweza kujiamini na unachokifanya zaidi ya mwanzo. Kabla ya kuanza biashara 1. Kukubaliana na hali     Katika vitu  vikubwa ambavyo wafanyabia

Vitu vya kuzingatia unapofanya Branding

Kuna vitu vitatu ambayo hutumika sambamba   ili kutengeneza 244  yenye afya Logo - Nembo Nembo   ni alama maalum ya kwako peke yako inayokutambulisha sokoni na alama hiyo ndio Itakuwa inasimama kwa niaba ya kampuni yako Branding- kulijengea jina utambulisho Branding ni kutengeneza uaminifu na ahadi ya bidhaa yako kwenye akili ya mteja unaemtegemea Ambapo brand huunganishwa na bidhaa kwa mteja . Identity - utambulisho ( marketing,advertising,publication,sales) Hii inamaanisha aina ya utambulisho utakaotumia kujitambulisha, unaweza kujitambulisha kama expert Kujitambulisha kama mzoefu kujitambulisha kwa aina ambayo wewe itakupa ahueni na upenyo kwenye soko ulilopo

Maswali 12 kuhusu Branding

Maswali ya Msingi unayotakiwa kuyafahamu kabla ya kuanza kubrand. 1. Brand ni nini? Brand kwa maana moja tunaweza kusema ni muonekano wa biashara yako, branding ni muonekano wako Kuhusu biashara yako na jinsi gani biashara yako inajitofautisha na washindani wenzako, 2. Kazi za Brand. Brand hutambulisha muonekano ,ubora wa kuaminika kwa watu, huku bidhaa za generic(kawaida) hazijulikani na haziaminiki ,hata hivyo brand ni ghali na inahitaji mipango ya muda mrefu. Brand hutofautisha bidhaa na hufanya bidhaa kutambulika mapema Brand inaruhusu mtumiaji kutengeneza maamuzi na matumizi ya bidhaa Brand hutengeneza thamani halisi kwenye macho ya washirika wa kibiashara na hupenyeza thamani ndani ya macho ya mtumiaji. Branding hutengeneza trademark ambayo huongeza thamani ya bidhaa. 3. Kwanini ufanye brand     Unafanya brand kwa sababu unataka kutambulika na kuongeza mauzo , pia ni kutaka     kujitofautisha na washindani wako 4. Faida gani unayoipata ukibrand      Brand hukutambuli