Posts

Showing posts from April, 2015

Kwanini usiache kuendelea kujitangaza na kutafuta masoko hata kama biashara yako inafanikiwa.

Nimekuwa nikiulizwa hili swali mara nyingi sana kuhusu mafanikio ya biashara na muendelezo wa matangazo, na asilimia kubwa ya wanaouliza swali hili ni wale ambao biashara zao zimefanikiwa au malengo waliyokuwa wameyaweka yamefikia au yamekaribia sana. Mara zote jibu langu huwa ni moja tu. Msingi wa biashara yako uko kwenye kujitangaza hivyo ukisimama kujitangaza basi na biashara itasimama kuingiza mauzo. Leo nimeona niweke hapa chini baadhi ya sababu ambazo zinakufanya kama mfanyabiashara au mjasiriamali usiache kuendelea kujitangaza. 1. Ushindani haukomi katika ulimwengu wa biashara mafanikio au kushindwa kunaletwa na ushindani,biashara isiyokuwa na ushindani haiwezi kujijua kama inashinda au inafeli sababu hakutakuwa na mwingine wa kuikumbusha kufanya ambavyo inatakiwa kufanya. Hivyo kama biashara yako iko sokoni na inafanya kazi kujitangaza hakukomi sababu mshindani wako kila siku anafikiria njia na namna ya kukushinda kibisahara mteja aliekuja kwako leo kesho awe ni mteja wake

Kazi na Aina za Branding

Karibu katika muendelezo wa somo la Branding na leo nimekuletea kazi na  aina za Branding katika maisha ya biashara zetu, watu wanafikiri Branding ni kitu kigeni katika ulimwengu wa biashara La Hasha! Branding sio kitu kigeni na kila mtu kila siku anafanya Branding.Hapa chini ni baadhi tu ya kazi za Branding katika biashara yako. Branding ndio muongozo au chanzo cha mauzo yako, iwapo utajibrand vibaya mauzo yako yatakuwa mabaya na iwapo utajibrand vizuri mauzo yako yatakuwa mazuri,Kazi ya masoko ni kuipeleka Branding nje ya ofisi ambapo kama ahadi na muonekano ulioweka kwenye brand yako utakuwa mzuri na wenye kumvutia mteja basi huyo atakuwa mteja wako ila ikiwa tofauti na hapo utakuwa umemkosa mteja. Kazi za Branding Brand   hutambulisha muonekano ,ubora   wa kuaminika kwa watu, huku bidhaa za generic (kawaida)   hazijulikani   na haziaminiki ,hata hivyo brand ni ghali na inahitaji mipango ya muda mrefu Brand hutofautisha bidhaa na hufanya bidhaa kutambulika mapem