Posts

Showing posts from 2014

Salamu na mambo ya kuzingatia mwaka 2015

Kwanza kabisa sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi ya kuendelea kuwepo kwa mwaka huu hadi kuiona krismas nyingine tena ya mwaka huu, wapo wengi waliotamani kuiona lakini hawajaifikia. Ila zote ni baraka za Mwenyezi Mungu. Tukirudi katika mada kuu nawatakieni heri ya Krismasi na Mwaka mpya wa 2015 wasomaji wangu wapendwa,wajasiriamali,wafanyabiashara na kila anaepitia na kusoma hapa, nawatakia sherehe njema na nnawaombea tufike wote mwaka 2015. Nimekuwa kimya kidogo nilikuwa na shughuli zimenibana kidogo lakini nafikiri kwa baadhi waliokuwa wanapata shida kunipata walikuwa wanatumia mawasiliano yangu ambayo yako kwenye ukurasa wa   huduma zetu na pia ukishusha chini kabisa kuna sehemu ya kutuma ujumbe ambapo zilikuwa zinanifikia na nilishughulikia changamoto zao haraka iwezekanavyo. Kwa mwaka 2015 nategemea zaidi kupata maswali ya nini mtahitaji niwe nakiongelea au kitu ambacho haujakielewa kwenye baadhi ya machapisho au kwenye biashara yako. Nitaruhusu kupokea m

Mabadiliko ya lazima kwa wafanyabiashara na wajasiriamali Tanzania

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa mwenendo wa biashara unavyoenda hapa nchini basi utakuwa umeshagundua kuna mabadiliko makubwa yanayoendelea ndani ya nchi hii, na sababu kubwa ya mabadiliko hayo ni kutokana na Tanzania imekuwa ikifanya biashara kienyeji kwa muda mrefu na sasa imeonekana  katika ramani ya dunia wawekezaji na makampuni mengi ya kigeni yanakuja kufungua matawi na kuanzishwa hapa nchini hivyo serikali yetu imeona ni bora ianze kuwatengeneza wafanyabiashara mapema kabla haijajaa wawekezaji mfano: Serikali haikuwazoesha wafanyabiashara kulipa kodi kwa EFD lakini imegundua kuna fedha nyingi zinapotea iwapo hawatatumia EFD ndio maana wakaamua kuwabana lakini kwa kuwa hawakuzoeshwa leo hii hadi Wahindi na Wachina ikiwa ni mgomo wa kufunga maduka nao wamo japokuwa kwao mtindo huu unatumika kitambo na biashara ni ushuru, lakini huku nao wako mstari wa mbele kufunga maduka. Baadhi ya mabadiliko haya yanatokea kwa kutangazwa na mengine hayatangazwi Mfano: Serikali iliona wimbi kubwa

Kabla ya kuanza kufanya marketing jiulize maswali yafuatayo

Marketing kwa maana moja mimi huwa naiita ni zao la Branding kwenye biashara ambalo linatakiwa litoke liende kuitangaza brand iliyojitengeneza.Hapa nchini biashara nyingi zinafanyika kwa mazoea na watu wanafanya bila kuelewa au kuwa na maana halisi ya kitu wanachokifanya, utakuta mtu ameona kampuni fulani wamefanya kitu fulani kwa ajili ya bidhaa, biashara au huduma kwa ajili ya kampuni yao, basi na yeye pia atataka kubadilisha jina tu kwenye hicho kitu kutoka jina  la biashara alioiona hadi jina la biashara yake, ila vingine ataviaacha kama vya mwenzake kwa vile tu amependa jinsi kile kitu kilivyo. Na wengine hufanya hivyo kwa mifano na kujaribu . Leo nitaelezea kidogo vitu vya kuzingatia kabla hujaanza kujitangaza au kufanya marketing,Tutaangalia vitu kama vitano(5) ambavyo unatakiwa kuviangalia kwenye biashara yako kabla ya kuanza kufanya marketing, vitu hivi mara zote huwa ni vitu vya kawaida na huonekana ni sio vya muhimu sana lakini nikupe siri ndugu yangu hakuna kitu ambac

Ushauri wangu kwa serikali kuhusu ujasiriamali na upungufu wa kazi kwa vijana.

Nchi yetu inaongozwa na sheria na moja kati ya sheria za nchi hii ni kila mtu ana uhuru na haki ya kutoa maoni yake , hivyo na mimi nimeamua kutoa maoni yangu binafsi kuhusu hili suala la ujasiriamali hapa nchini , kwanza pongezi  kwa serikali kuona njia mbadala ya kupunguza wimbi la vijana wasio na ajira ni kufanya ujasiriamali , lakini nilikaa na kuangalia baadhi ya mambo nikagundua kuna mapungufu mengi na mara nyingi tumezoea kutaja matatizo ili uliemwambia atafute suruhisho. Hapo unakuwa unakosea kama yeye hakuliona tatizo unapompa tatizo tu bila suruhisho unampa kazi ya kufanya ambacho hakijui hebu fikiria nimekutengenezea gari lako na kukuletea mimi sio mtengenezaji wa kwanza inamaanisha ntarekebisha ili liwe kama awali wewe ndio unaetumia gari yako nikitengeneza isipofika unapohitaji ni lazima utaniambia bado ilikuwa anafanya hivi na hivi na hivi tofauti kabisa na huku kuna tatizo la maji kijijini watu wanaeleza tu tunashida ya maji tufikiriwe hata kidogo na sisi tunatembea umb

Kwanini wajasiriamali wengi wanafeli?

Image
Kumekuwa na watu wengi ambao wamekuwa  wanahitaji kuwa wajasiriamali lakini asilimia kubwa wanakuwa ni wale ambao wanakuwa wamefeli mipango mikubwa au kuna kitu kimewasukuma ,vitu ambavyo unatakiwa usifanye kwa kudhani unatengeneza maisha utakuwa unapotea. Kuna kundi ambalo wao huanza ujasiriamali baada ya kuona umri unaenda au wanategemewa sasa na aidha famili a au kadahali Usifanye ujasiriamali kwa kuona umri umeenda upate kitu cha kujishikiza, hapo utafeli kumekuwa na watu wengi ambao hadi astaafu ndio anaanza ujasiriamali au baada ya kuona umri umeenda ndio anatafuta kitu cha kumpatia ujasiriamali hii ni mbaya na kufanikiwa kwake ni kugumu sana, ujasiriamali sio nyongeza ya ulichonacho ujasiriramali ni msingi wa ulichonacho kama hukutengeneza msingi mwanzo ujue hata uweke ukuta imara kiasi gani dhoruba ikija ni lazima nyumba itapata mtikisiko. Wapo wengine ambao wanafanya ujasiriamali  baada ya kukosa au kutuma sana maombi ya kazi ukifanya ujasiriamali

Jinsi ya kuanzisha biashara bila ya kuwa na mtaji wa pesa. (Sehemu ya pili)

Baada ya kuangalia sehemu ya kwanza wiki iliyopita ya jinsi ya kujiajiri bila kuwa na mtaji pesa leo tunaendelea na sehemu ya pili. Kama imetokea umeshindwa kugundua kipaji chako bado kuna uwezekano wa kuanzisha biashara yako bila ya kuwa na mtaji pesa haya kitu cha kwanza ni unatakiwa ujitambue wewe ni nani kati ya mfanyabiashara au mjasiriamali halafu ona aina ya biashara ambayo ndani ya uasili wako mwenyewe  ichague kwa umakini halafu andika chini vitu ambavyo unavihitaji ili biashara yako ifanikiwe au ionekane andika pembeni ( Sio mpango biashara)halafu  anza kufanya utafiti wa hivyo vituulivoandika kwa kutafutia mbadala wake sehemu zote ambazo zinahitaji pesa ziorodheshe pembeni halafu anza kutafuta mbinu mbadala kwa kila kimoja usikurupuke chukua muda ili ufanye maamuzi mazuri kama ulichochagua kikondani ya sehemu  yako ya kujitambua kupata njia mbadala sio kazi ngumu.( Safari ya mafanikio huanzia mbali sana hakuna tajiri ambae alianza huku akiwa tajiri au alianza na mtaji mku

Nukuu za Chuma

Image

Jinsi ya kuanzisha biashara bila ya kuwa na mtaji wa pesa.

Imekuwa ni kawaida kwa watu wengi kutambua pesa kama mtaji wa kila kitu katika biashara , lakini katika ulimwengu wa biashara iko tofauti pesa sio mtaji bali pesa ni kiasidizi cha mtaji . Leo nitakupa baadhi ya njia unazoweza kutumia kuanzisha biashara yako bila ya kuwa na mtaji pesa ila kwa kutumia mtaji mbinu na vinginevyo. Watu wengi  huruka sana sehemu ya kwanza ya mtaji ambayo ndio  chimbuko la mtaji  na kukimbilia kwenye  sehemu zinazofuata na kuendelea bila kujua muhimili wa nyumba ni msingi bila ya msingi mzuri nyumba inaanguka hivyo bila chimbuko zuri la mtaji wako hauwezi kufanikiwa, sasa basi chimbuko hilo ni nini ambalo watu huliruka na kukimbilia mengine. Kichwa/ akili mtaji wako mkubwa ni kichwa chako na hata wazo na kila kitu kinaratibiwa na kichwa chako mwenyewe ndani ya kichwa ndipo panatengeneza ndoto na ndipo panapofanya ndoto zitimie kwa kushirikiana na viungo vingine vya mwili lakini injini ya mwanadamu ni kichwa katika kufanya mambo ya maamuzi. Kichwa ndi

Vitu vinavyorudisha nyuma wajasiriamali/ wafanyabiashara (sehemu ya 2)

Toleo lililopita nilitoa maelezo kuhusu vitu ambavyo vinarudisha nyuma wajasiriamali wengi na wafanyabiashara, ambavyo ni vitu vya kawaida na vinafanyika na vingine hufanyika kimakosa bila hata kujua. Unapokuwa mjasiriamali / mfanyabiashara kufeli ni moja ya hatua za ukuaji wa biashara yako hivyo tegemea kufeli kila unapotaka kukuza biashara yako,na kama kuna kufeli ambako ni lazima upitie basi lazima kuwe na namna ya kukabiliana na kufeli huku inatakiwa kila mpango unaoutengeneza uwe na mpango msaidizi wa iwapo utafeli basi huu utachukua nafasi au iwapo mambo yataenda mrama kwa upande huu nitafanya hivi au vile sio kufanya tu huku unawaza na kusema MUNGU atasaidia. Na madhara yote hutegemea  vitu 4 ambavyo ndio vinakuongoza katika biashara yako Mipango biashara yako( Business plan) Baadhi ya vitu ambavyo huwa vinawafelisha wengi ni pamoja na jinsi ya  utengenezaji au ufanyaji wake , japokuwa mpango biashara ndio nguzo ya biashara wengi hufikiria ni ufujaji wa pesa  na h

Mambo yanayorudisha nyuma wajasiriamali/Wafanyabiashara

Kuna mambo mengi ambayo wajasiriamali wengi huyaangalia kama hayana nafasi sana   wanapoanza ujasiriamali lakini baada ya muda na mambo kugeuka ndipo hukumbuka umuhimu wake, na mengi kati ya hayo huwa yanakataliwa na misemo ya mitaani ambayo huwa inaathari za moja kwa moja au vinginevyo kwa mfano maranyingi unapoamua kufanya kitu huwa unafuta mawazo yote ya kufeli ingawa katika hali halisi kufeli kupo katika hilo hilo unalolifanya na wengi huwa wanatumia msemo wa " unapofanya jambo fanya kwa moyo wote usiwaze kufeli sababu utapunguza ari" uwezekano ni ukweli ukiwaza kufeli unapunguza ari ya kulifanya jambo lakini Je unalolifanya linakufeli au halina? Na je ukifikiria kufeli unapunguza ari kwa kuliogopa jambo au kwa kuchukua tahadhari iwapo utafeli? .vivyo hivyo na kwa wajasiriamali wengi pia huwa hawawazi kufeli katika wanachokifanya ni kushinda tu muda wote lakini ukiangalia ukweli ni kwamba hata katika maisha yao ya kawaida mipango yao sio yote inayofanikiwa. Utakuta baada

Vitu ambavyo vinatakiwa vionekane kwenye nembo yako

Iwe ya kipekee Watu wengi wamezoea kuwa wanatengeneza logo kwa kuigilizia ya sehemu fulani au kwa kufuatisha mfumo wa kampuni fulani , wengine hufanya kama logo nyingine kisa tu ni kwa vile imempendezea machoni kwake au ameipenda bila kujali ujumbe utakaotoka baada ya hapo, nembo yako mara zote inatakiwa  iwe ya kipekee na isifanane na nembo yoyote dunia nzima. Hasa katika soko ulilopo, unatakiwa kuifuata maana halisi ya nembo kama nembo ni utambulisho wako iweje uwe unafanana na utambulisho wa mwingine na iwapo umeigilizia kutoka kwa mwenzako inamaanisha tayari yeye brand yake ni kubwa kuliko yako hivyo ukitengeneza nembo inayofanana nayakwake ni kama vile unamsaidia kumkumbushia watu na kumtengenezea nafasi katika vichwa vya wateja wake. Mfano: leo hii ukipita sehemu ukaona nembo inayofanana na ile nembo ya brand ya cocacola utamkumbuka nini brand ya cocacola au brand ya yule aliyeitengeneza . Ukweli ni kwamba utaikumbuka cocacola na unaweza hata kuanza kujiuliza kama wa

Muendelezo wa umuhimu wa Logo katika biashara yako

Image
Kukutambulisha katika soko Logo yako ndio inayokutambulisha katika soko la ushindani ,soko la biashara  na hata kwa wateja hivyo logo yako inatakiwa iwe ambayo ni maalum kweli ili utambulisho wako usije kuwa na muonekano mbaya au usiovutia logo yako ndio ambayo inatathminiwa ndani ya soko mtu anapoiona logo yako ndio anakutambua. Logo ni muongozi wa biashara yako  kwa sababu unapokutana na mteja ananunua kitu kutokana na utambulisho na muendelezo wa logo ya bidhaa unayotengeneza siku sio nyingi nilipokea simu kutoka kwa mtu nisiemfahamu akawa anataka nimtengenezee logo kawaida yangu huwa ni kupata maelezo nikamuuliza ameipatia wapi namba yangu na aina ya logo anayotaka alishangaa kidogo kuona nakuwa na maswali kumzidi lakini alielewa na kitu alichokuja kunijibu ni aliona business card yangu kwa mtu akawa amependa logo yangu ikawa imemvutia kiasi kwamba akawa anataka nayeye  nimtengenezee nyingine lakini iwe jamii ya hiyo ya kwangu, hivyo logo yako ni muongozo wa bi

Logo/Nembo na Biashara yako

Image
Katika matoleo yangu ya nyuma nilielezea vitu vinavyotengeneza biashara yenye afya na moja kati ya vitu hivyo ilikuwa ni nembo (Logo) leo nitaelezea kwa undani kidogo maana yake katika nyanja ya biashara na kwanini biashara inahitaji logo. Logo/Nembo ni nini? Nembo ni alama maalum inayokutambulisha sehemu fulani katika jamii, hiyo ni maana ya nembo kwa ujumla lakini nembo ( logo) maana yake haitofautiani  sana na maana ya hapo juu,logo maana yake ni alama ya utambulisho wako katika biashara ambayo inatengenezwa kwa umakini na utaalamu maalum kwa ajili ya biashara yako. Logo/Nembo inamaana gani kwako Imekuwa kawaida kwa watu kutengeneza nembo mtu anapomiliki biashara basi anajua kitu cha kwanza ni nembo japo hajui inaumuhimu gani katika biashara nilishawahi kukutana na mmiliki wa biashara moja nikamuuliza kwanini ananembo katika biashara yake  majibu yake ilikuwa ni " kama biashara lazima na mimi niwe na logo, na unapomiliki biashara nembo ni lazima

Nukuu za Elisha

Image

Aina tatu za imani zitakazokurudisha nyuma katika biashara yako

Biashara haiangalii unaamini kupitia nini,  biashara haiangalii wewe ni mkristo,mpagani muislamu au mhindu,lakini kuna imani ambazo biashara inakutengenezea na inataka ufanikiwe kupitia hizo, hivyo ilikufanikiwa katika biashara yako unatakiwa upitie ukipishana nazo lazima matokeo yake hayatakuwa mazuri. 1.Naweza kufanya kila kitu mwenyewe.  Hii inakuja   pale mtu anapoanza kujiona yeye ni mzuri na mwelevu wa kila kazi katika biashara yake , lakini ukweli ni hauwezi kufanya kazi zote , ufagie , uhasibu,afisa utumisishi, afisa rasilimali watu na hata masoko wewe mwenyewe? Ukweli ni kwamba hauwezi ukawa mzuri wa hizo kazi zote ni lazima utakuwa na sehemu yako ambayo unaweza kufanya vizuri zaidi ya nyingine ,   na kama unataka biashara yako ifanikiwe fanya anbacho biashara inataka tumia au fanya ambacho unaweza kukifanya vizuri zaidi usilazimishe kwa kutaka kuonekana unajua sana au unaweza kufanya kuliko wengine ila fanya kwa kuangalia ni kipi unaweza kukifanya vizuri zaidi ya

Vitu vinavyotengeneza biashara yenye afya

Image
Kuna vitu vitatu ambayo hutumika sambamba   ili kutengeneza brand yenye afya Logo - Nembo Nembo   ni alama maalum ya kwako peke yako inayokutambulisha sokoni na alama hiyo ndio Itakuwa inasimama kwa niaba ya kampuni yako , japo nembo (logo) imekuwa ni kitu cha kawaida kwa watu na wengi wanatengenezea mazoea kwa vile kuna fulani katengeneza au kampuni fulani au ukiwa na biashara fulani ni lazima uwe na nembo lakini ukweli na umuhimu uliopo ndani ya nembo ni mkubwa na zaidi inahitajika nembo hiyo itengenezwe maalum kama ambavyo nimeeleza hapo juu utakuta mtu anatengeneza nembo kwa kukopi nembo nyingine hii sio sahihi tengeneza kitu ambacho kitakuwa ni chenyewe na kitakacho kutambulisha wewe mwenyewe katika soko. Branding- kulijengea jina utambulisho Branding ni kutengeneza uaminifu na ahadi ya bidhaa yako kwenye akili ya mteja unaemtegemea Ambapo brand huunganishwa na bidhaa kwa mteja inatakiwa ulijengee jina la biashara yako utambulisho ambao hata mto

Jinsi ya kujibrand wewe mwenyewe

Katika matoleo yaliyopita nilielezea maana na faida za branding lakini leo nitaelezea kuhusu brand kwa maana au kwa nafasi ya mtu hivi ni baadhi ya vitu vinavyoijenga na kuitengeneza brand yako.   Kusikiliza Tengeneza maneno ya kuongea kulingana na rika Toa maoni mara nyingi kwenye mitandao ya jamii Sikiliza na wengine kwenye   eneo lako la ushindani Sikiliza viongozi   wa maeneo mengine na angalia ni vipi mawazo yao unaweza kuyatumia Usisahau podcast   Tovuti Unatakiwa uwe na blogu au tovuti Iwe na muonekano mzuri Ukurasa wa "about us" unatakiwa iwe ni wewe pamoja na biashara yako Isajili tovuti yako na sehemu zinazoshughulika na kutafuta url(top sites)   Pasipoti Fungua akaunti kwenye mitandao ya kijamii   Outpost( Muonekano wako kwenye mitandao ya kijamii) Hakikisha mtandao wako   unaotumia umeandikwa kwenye profile yako (linkeldin) Hakikisha kila mtandao wa kijamii uliojiu

Kuongeza uelewa

Habari za Jumatatu baada ya kutoa maelezo ya njia na baadhi ya hatua  za kufanya katika biashara wiki hii nitakuwa ninapokea maswali kuhusiana na mada zangu nilizoandika hapo awali kama kuna sehemu umepata utata unaruhusiwa kuuliza kwa kutumia comment chini ya huu uzi au kwa kutuma email moja kwa moja kwangu kupitia elishachuma@gmail.com. Huduma hii itakuwa ni ya wiki 1 ( siku 7)

Tofauti kati ya Branding na Marketing ( Masoko)

Kumekuwa na Mkanganyiko wa matumizi pia ya hivi vitu viwili Branding na Marketing ( Masoko) na imekuwa ni tatizo kugundulika ipi inayotakiwa ianze kati na ipi ni kubwa zaidi ya mwenzake . kwa upande wa Branding tayari nilikwisha elezea kwenye toleo za nyuma  Branding . Leo nitaelezea kidogo maana ya masoko na tofauti yake na Branding Masoko (Marketing)   ni kila mkutaniko wa kampuni yako na mtu au kitu chochote duniani Maana ya marketing ( Masoko) inajumuisha; Jina la biashara,mgawanyo wa aidha unatoa huduma au bidhaa,njia za utengenezaji au utoaji huduma,rangi,saizi na umbo la bidhaa yako,upakiaji,eneo la biashara,kujitangaza,mahusiano na jamii, tovuti,Branding,email,sahihi yako kwenye majarida na chochote unachokitoa ,ujumbe wa sauti,matamasha ya mauzo,simu,mafunzo ya uuzaji,jinsi ya kutatua matatizo, mipango endelevu ,watu wanaokuwakilisha,wewe,unavyofuatilia Lakini pia kwa upande mwingine marketing(Masoko) inajumuisha,wazo kuu la brand yako,huduma yako,mueleke