Elimu inayokosekana
Elimu inayokosekana
na inayowapoteza wengi katika maisha
Katika mfumo wetu wa
elimu kuna elimu muhimu inayokosekana na
hakuna sehemu ya kuipata hadi
Ujitambue mwenyewe
ambapo elimu hiyo ni elimu ya
kujitambua,
Tatizo lililopo
katika elimu yetu ni kwamba tunasoma kwa kufuata taratibu za watu fulani, mfumo
wa elimu tunaotumia
Ni wa mzungu , ili
ujikomboe unatakiwa ujitambue, mzungu alileta elimu lakini haikuwa elimu ya
kutufanya tujitegemee
Elimu tunayoipata
kwenye shule zetu kuanzia ngazi ya chekechea hadi ngazi ya sekondari ni elimu
ya lugha na kusoma na kuandika, kama ni hivyo kwa nini basi tuendelee kupoteza
muda wingi kusumbukia kusoma na kuandika?.
Wanafunzi wanachukua
hadi masomo 14 yote ayafanyie mtihani na anatakiwa kufaulu ni uwezo wa hali ya
juu unaotumika kwa wanafunzi wanaofaulu, na hicho hakikuwa kizazi cha dot.com
ambacho kila kitu wanafunzi wanatumia
Mbadala wa google
kutafuta.hata kufeli sana kwa wanafunzi wetu kumesababishwa na mabadiliko ya
hali ya utandawazi
Nchini zamani
ilikuwa ili ufaulu unajitahidi kujisomea sana na kujisomea kwenyewe ni kwa makatasi ya mitihani iliyopita na vitabu
lakini sasa hivi hali ni tofauti hadi wanafunzi
wa shule za msingi wameshakuwa watumwa wa kompyuta kila kitu wanajua
kinawezekana hata wanaoshindwa wanajua google itawasaidia lakini. Waliofanya na
kusoma kabla ya google walifaulu vipi?
Serikali imekazania
sana masomo ya sayansi na hakuna sayansi wanayoisoma tofauti na historia ya
sayansi, maabara zenyewe sio za kutosha lakini katika mtihani unatakiwa ufanye
nadhalia na vitendo ni jambo gumu kwa wanafunzi wetu na katika hilo bado serikali
inataka mtu ajitegemee atajitegemea kwa kitu gani iwapo mmeshamfanya awe
tegemezi.
Mfano: Mwanafunzi
akiwa msingi kapata elimu ya kusoma na kuandika hadi akamliza huku somo moja tu
ndio anafundishiwa lugha ya kigeni, kaingia sekondari lugha inabadilika sasa ni
somo moja tu ambalo anafundishiwa lugha ya nyumbani ( hapo tayari umeshamchanganya
ni sawa na umemrudisha kuanza msingi wakati yuko sekondari) tena anachukua
masomo 14 masomo yote hayo anatakiwa ayaweke kichwani mwake aidha yanamsaidia
au hayamsaidii katika maisha ( wakati maana ya kusoma ni kupata elimu amabayo
itakuja kukusaidia mbeleni katika maisha yako, kuna umuhimu gani kusoma masomo
yasiyo kusaidia ).bila kumuandaa au kumpa machaguzi kulingana na atakachosoma (
mfano: CBG,PCB - Haya kwa upande wa sekta ya afya ,hkl,hgl - haya kwa upande wa
lugha ) mwanafunzi anaanza kujichagulia bila kuwa na uchaguzi hivyo uchaguzi
wake utafuata ashauri wa marafiki au kundi fulani , aatachukua
Hayo masomo na
ataendelea nayo hadi chuo , lakini kutokana na kuwa hayakuwa katika mipangilio
yake ya maisha ya baadae ndio unakuta mtu anadegree ya sheria ila anaomba kazi
ya kuwa administrator.
Serikali haiwaandai
wanafunzi kutambua tofauti iliyopo pale ambapo mtu akiwa shule, akiwa chuo,
akiajiriwa na anapo jiajiri mwenyewe, hakuna elimu hiyo lakini baada ya kuona
vijana wengi wanapotea sasa hivi vijana wanashauriwa wajiajiri watajiajiri vipi
wakati hawana hata hiyo elimu ya ujasiriamali?.
Inatakiwa watu
wajitambue ilhali wakiwa bado wanauwezo wa kukunjika sio tayari
wameshanyongorota ndio mnaanza kuwaambia wajinyooshe, elimu ya kujitambua
inatakiwe itambulike kwa kila mtu kuanzia mtoto hadi mtu mzima ikiwa unajitambua hauwezi kukaa mtaani
miaka nenda rudi bila kupata kitu cha kufanya kutokana na elimu uliyoipata
lakini kwa sababu hajafundishwa kujitambua, muda wa yeye kujitambua anakuwa
tayari anamajukumu mengine tayari hiloni tatizo .
Ushauri wangu.
Yafaa serikali
kuanzisha masomo au kuwe na vipindi maalum katika mtaala wa elimu kufundisha
elimu ya biashara na ujasiriamali kwa wanafunzi wetu ili wanapohitimu tayari
wanakuwa wameshajitambua wako upande gani. Pia ushauri wangu serikali ipunguze
masomo yasiyokuwa na umuhimu kwa mwanafunzi anapoteza muda mwingi kufanya
yasiyo na manufaa katika maisha yake.
Comments
Post a Comment