Aina za washindani katika biashara
Katika kila biashara
lazima kuwe na washindani, biashara isiyokuwa na washindani hiyo sio
biashara na katika biashara Ushindani ni wa
muhimu kwa ajili ya maendeleo ya biashara yoyote na moja kati ya faida za washindani ni kuongeza
changamoto za ufanisi wa kazi,kuna aina kuu
tatu za washindani
- Washindani wa moja kwa moja
Hawa
ni washindani ambao unawafahamu na mnashabihiana biashara,mnafanya biashara ya
aina moja,kwa mfano kama biashara yako ni fundi cherehani basi mafundi
cherehani wengine ndio washindani wako
wa moja kwa moja.
- Washindani wasiokuwa wa moja kwa moja
Hawa
ni washindani ambao wanatengeneza bidhaa au shughuli mbadala ya za kwako,
wanatengeneza aina ya bidhaa ambazo kama
mteja asipotumia za kwako basi atatumia za kwao. Mfano: kama wewe ni fundi
cherehani washindani wako ambao sio wa moja kwa moja ni wale ambao wanauza nguo
madukani za spesho na mitumba hao ni washindani wako pia.
- Washindani dhahania
Hawa
ni aina ya washindani ambao hawapo kwenye hyo biashara sasa ila wanafikiria
kuanzisha biashara aidha kama ya kwako au mbadala wa biashara yako hawa pia ni
washindani wako.
Kati ya washindani
wote watatu mshindani ambae ni hatari zaidi ni mshindani asiokuwa wa moja kwa
moja, huyu ni hatari kwa biashara yako na mara nyingi huleta madhara katika
biashara yako na ugumu unakuja pale unapotaka kushindana nae yeye sio mshindani
wako wa moja kwa moja.
Comments
Post a Comment