Tofauti za mipango katika biashara

 Katika biashara lazima kuwe na mipango ambayo itaisaidia biashara yako kusonga mbele, kila biashara imara lazima iwe na mipango ili kuifanya na kuisaidia kusonga mbele kwa wakati husika na baadae pia. Mipango hii ndio  msingi mkubwa wa kila biashara ,Mipango imegawanyika katika pande kuu mbili kuna mipango ya Muda mrefu na mipango ya muda mfupi, mipango ya muda mrefu ni ile ambayo inakuwa biashara  inafany ili iifikie , mipango ya muda mfupi ni ile mipango mifupi mifupi ya kusaidia biashara ifikie mipango ya muda mrefu bila kutoka nje ya muda mrefu

Mipango ya muda mrefu ni ile ambayo Biashara inayaweka kwa ajili ya kuyafikia baada ya kipindi cha muda mrefu kuanzia miezi 12 nakuendelea.

Mipango ya muda mfupi ni ile ambayo inakuwa ya muda mfupi inayotengenezwa kwa ajili ya kuifanikisha mipango ya muda mrefu bila kutoka nje ya lengo la mipango mirefu

Mfano: unapofanya biashara unatakiwa uwe na malengo na maono hivyo hayo ndio malengo ya mbali ,lakini ili uyafikie ni lazima uwe na mipango mifupi mifupi ambayo inaweza kuwa na ukomo au inayoweza kuendelea bila kutoka nje ya lengo kuu.unabiashara ya kusafirisha mizigo malengo makuu ni baada ya miaka mitano uwe unasafirisha mizigo hadi nje ya nchi lakini umeanza na gari ndogo ambazo haziwezi kuhimili hiyo mikiki ya kusafirisha hadi nje ya nchi unatengeneza mipango mifupi mifupi ya kufanikisha kununua magari,ukaanza kuwa unaangalia mikoa ambayo kuna uhaba wa usafiri wa mizigo ndiko ukaegemea zaidi baada ya mwaka  ukafanikiwa kupata hilo gari moja ukabadilisha mpango kwa hili gari kubwa lenyewe likawa linazunguka mikoa yote kwa kupeleka mzigo kutoka mkoa mmoja na kwenda mwingine huku zile ndogo zinaendeleza mpango ule ule ule wa mwanzo .baada ya miaka 3 tayari unaweza kuanza safari za nje ya nchi na kwa kuwa umeshafahamika kwa kupeleka mizigo mikoa yote hata wateja wa kupeleka nje utawapata kwa urahisi mwaka wa tano unafika ukiwa umeyafikia malengo yako.

Watu wengi hudhania mipango ya muda mrefu na muda mfupi hutakiwa kuwa sawa hivyo hufanya mipango ya aina moja tu na kuacha lakini baada ya muda hujikuta kuna kitu kinapungua katika mipango yao, unapoamua kutengeneza mipango ya biashara kwanza unatakiwa uwe umeshatambua nafasi yako katika soko  na una chachu kiasi gani katika soko je?  ni msindikizaji au ni mshindani,ukishajitambua hapo ndio unaweza kutengeneza mipango yako ambayo utaiweka na kuisimamia pamoja na mipango ya muda mfupi


Ili mipango ya muda mrefu ifanikiwe basi ni lazima kuwe na mipango ya muda mfupi imara na pia tujifunze kuyafikia malengo na mipango madhubuti na imara na mafanikio ya mipango ya muda mrefu hayaonekani kwa macho ya kawaida haya ni aina ya mafanikio ambayo yanagundulika na wachache, wafanyabiashara wengi hufikiri mafanikio ni kuwa na pesa nyingi au kutengeneza ofisi ndio ni mafanikio lakini sio ambayo biashara inayahitaji  hayo ni mafanikio yako ya kimapato mafanikio ya biashara yanaenda sambamba na wateja hivyo mafanikio yao yako mikononi mwa wateja wako na washindani wako.

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango