Mabadiliko ya lazima kwa wafanyabiashara na wajasiriamali Tanzania

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa mwenendo wa biashara unavyoenda hapa nchini basi utakuwa umeshagundua kuna mabadiliko makubwa yanayoendelea ndani ya nchi hii, na sababu kubwa ya mabadiliko hayo ni kutokana na Tanzania imekuwa ikifanya biashara kienyeji kwa muda mrefu na sasa imeonekana  katika ramani ya dunia wawekezaji na makampuni mengi ya kigeni yanakuja kufungua matawi na kuanzishwa hapa nchini hivyo serikali yetu imeona ni bora ianze kuwatengeneza wafanyabiashara mapema kabla haijajaa wawekezaji mfano: Serikali haikuwazoesha wafanyabiashara kulipa kodi kwa EFD lakini imegundua kuna fedha nyingi zinapotea iwapo hawatatumia EFD ndio maana wakaamua kuwabana lakini kwa kuwa hawakuzoeshwa leo hii hadi Wahindi na Wachina ikiwa ni mgomo wa kufunga maduka nao wamo japokuwa kwao mtindo huu unatumika kitambo na biashara ni ushuru, lakini huku nao wako mstari wa mbele kufunga maduka.

Baadhi ya mabadiliko haya yanatokea kwa kutangazwa na mengine hayatangazwi Mfano: Serikali iliona wimbi kubwa la vijana na rika mbalimbali zikikaa kijiweni bila ajira wakahamasisha na kutoa mianya ya wazi kwa watu kuwa wajasiriamali, na watu walijitokeza wakafuatilia mafunzo na mwisho wakaamua kujikwamua kupitia hiyo kutengeneza Mafuta,kutengeneza Batiki, Shampoo,Sabuni na wengine waliamua kufanya kazi hiyo kuwa ndio mhimili wa maisha yao baada ya muda serikali ikaongeza mianya kwa kuwaruhusu kupeleka bidhaa zao kwenye supermarket kubwa na ndogo na watu walifanya hivyo lakini baada ya muda tena wakagundua wanakosa mapato kupitia kwao wakatoa tangazo mwananchi usinunue bidhaa yoyote isiyokuwa na nembo ya TBS, hapo tayari kwa wafanyabiashara wadogo ikawarudisha nyuma hasa ambao wanajua kutengeneza tu.

Sasa basi kwa mifano michache hapo juu unaweza kupata picha ni kipi ambacho kinabadilika na kwa mtindo gani chini hapa nimeorodhesha baadhi ya vitu ambavyo ni vinabadilishwa kulingana na mabadiliko haya ya biashara,asilimia kubwa ya mabadiliko haya yanaletwa na ongezeko la makampuni makubwa kutoka nje ambayo yanatumia mifumo hii ambayo kwetu tulikuwa tunaiongelea bila kuitumia.

Mfano: Brela, zamani ilikuwa ukitaka kusajili kampuni ni unaenda na jina unalotaka unatafutiwa kama lipo utapewa majibu baada ya hapo unapeleka memorandum na mengine yanafuata lakini kwa sasa inakoelekea na baada ya kutoa hili tangazo la kuhakiki makampuni mpango wao ni kufuta makampuni hewa ambayo hayafanyi kazi,lakini itakuwa kwa sasa ili kusajili kampuni yako itatakiwa pia uwe na business plan yaani unapopeleka maombi ya kufungua unakuwa tayari na business plan yako ambayo inaonyesha uwezekano wa uhai wa kampuni.

Mfano mwingine wa badiliko la lazima ni TRA kwa wafanyabiashara zamani ilikuwa ukihitaji TIN namba ni bure na haichukui hata siku nyingi lakini kwa sasa upatikanaji TIN namba ya biashara unakuwa mlolongo mrefu,utatakiwa kuleta mkataba wa pango,thamani ya vitu ulivyonavyo na mengine mengi ili tu kuhakikisha biashara yako ipo na itafanya kazi.

Ipo mifano mingi lakini yote ni kuhusiana na mpango mpya wa kutengeneza makampuni ambayo yanaliongezea pato taifa,hivyo kama mfanyabiashara katika hayo yote unatakiwa usisahau Branding, kufanya branding ya kampuni yako ni sawa na kujitengenezea maisha marefu ya uhai wako katika soko sababu vyote nilivyoorodhesha hapo  juu ni ni vya kukuhalalisha lakini kinachokuweka katika soko ni Brand yako hivyo zingatia sana vitu hivi kwa mfanyabiashara ambae anafikiria kuanza biashara ihalalishe biashara yako mapema tunakoelekea hakutakuwa na biashara za vichochoroni na kwa mfanyabiashara ambae tayari umeisha ihalalishe biashara yako zingatia Branding.


Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango