Salamu na mambo ya kuzingatia mwaka 2015

Kwanza kabisa sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi ya kuendelea kuwepo kwa mwaka huu hadi kuiona krismas nyingine tena ya mwaka huu, wapo wengi waliotamani kuiona lakini hawajaifikia. Ila zote ni baraka za Mwenyezi Mungu.

Tukirudi katika mada kuu nawatakieni heri ya Krismasi na Mwaka mpya wa 2015 wasomaji wangu wapendwa,wajasiriamali,wafanyabiashara na kila anaepitia na kusoma hapa, nawatakia sherehe njema na nnawaombea tufike wote mwaka 2015.

Nimekuwa kimya kidogo nilikuwa na shughuli zimenibana kidogo lakini nafikiri kwa baadhi waliokuwa wanapata shida kunipata walikuwa wanatumia mawasiliano yangu ambayo yako kwenye ukurasa wa  huduma zetu na pia ukishusha chini kabisa kuna sehemu ya kutuma ujumbe ambapo zilikuwa zinanifikia na nilishughulikia changamoto zao haraka iwezekanavyo.

Kwa mwaka 2015 nategemea zaidi kupata maswali ya nini mtahitaji niwe nakiongelea au kitu ambacho haujakielewa kwenye baadhi ya machapisho au kwenye biashara yako. Nitaruhusu kupokea maswali na nitayajibu kupitia hapa hapa ili elimu ya changamoto hiyo iwafikie wengi zaidi.

Unaweza kutuma swali lako sasa kupitia barua pepe yangu( elishachuma@gmail.com) au kwa kushusha chini kabisa ya blogu kuna sehemu ya kutuma maoni au unaweza kuandika kama komenti kwenye andiko hili asante.

NAWATAKIA SIKUKUU NJEMA!!!!

Elisha Chuma

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango