Umuhimu wa Broshua katika biashara yako

Broshua haina tofauti sana na Kipeperushi lakini yenyewe inakuwa imedizainiwa na kuprintiwa pande zote na kukunjwa ,lakini kipeperushi chenyewe  hakina kukunjwa na huprintiwa pande moja tu.

Broshua hazitolewi kama kipeperushi mara nyingi broshua hugawiwa na mtu wa masoko baada ya kuona mteja amevutiwa na kitu fulani au anahitaji maelezo zaidi ya kitu ambacho maelezo ya kina yapo kwenye broshua hiyo au amevutiwa na kitu fulani, Broshua ni lazima iwe ni nzuri na nadhifu.

Sababu za kutoa Broshua ni pamoja na
  • Kufuatilia maelezo zaidi kuhusu mawasiliano ya mauzo
  • Kutoa maelezo ya kina na mengi zaidi kuhusiana na biashara,bidhaa au promosheni
  • Kupata muitikio wa mteja mtarajiwa kwa kuonyesha uwezo,gharama na mategemeo



Watu wengi wamekuwa wanaacha kujitangaza au kutengeneza vitu vya kujitangaza kwa vile tu pale mauzo yanapoongezeka ni makosa kusimamisha promosheni kwa ajili tu unapata faida inatakiwa kila siku kuwe na promosheni inayoendelea ndani ya biashara yako na inatakiwa iwe inafanyiwa matangazo.

Chapisho lijalo nitaelezea utangulizi  wa Branding 

Pia kwa wale watakaohitaji professional email za branding .co. tz kwa ajili ya biashara zao,tafadhali wasiliana nami kwa mawasiliano hapo chini

Bado mnakaribishwa kujiunga na kundi la Whatsapp Branding kwa kuandika namba yako katika sehemu ya comment chini ya uzi huu ili uunganishwe, Asante. Kauli mbiu ya mwaka huu ni Mabadiliko lazima.


Pia karibu utangaze nasi na biashara yako ifikie watu wengi zaidi nje na ndani ya nchi kupitia blogu hii maelezo zaidi kuhusu kutangaza piga simu nama 0713603699.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango