Muongozo wa kuanzisha biashara

Biashara imekuwa ni ndoto ya watu wengi wake kwa waume,vijana kwa wazee na katika mizunguko zunguko yangu nikaona leo ngoja niongelee hili suala ambalo linabeba ndoto za watu wengi,mafanikio na ajira za watu wengi.

Kwanza kitu cha kwanza ambacho unatakiwa ukitambue ni kwamba mafanikio au kufeli kwa biashara yako kunategemeana sana na vitu vifuatavyo


  1. Ujuzi wa kazi
  2. Hamasa
  3. Nguvu 
  4. Maono na
  5. Uwezo wa mfanyabiashara au mjasiriamali huyo.

Hivyo kwa kuanza tu leo nitakupa vitu vitakavyokupeleka katika mafanikio ya biashara yako tangu inapoanza hadi ukuaji wake.
  1. Tambua uwezo wako
  2. unapoamua kuanzisha biashara shirikisha na upendo ulionao kwenye hiyo kazi na mvuto ulionao kweye biashara hiyo
  3. Fikiria kupitia biashara yako unaisaidia dunia
  4. Siku zote fikiria kuhusu mteja wako sababu biashara yako ni kuhusu wateja wako
  5. Tambua kwamba biashara ni utatuzi wa matatizo ya wateja
  6. Hakikisha unambinu zilizokamilika
Hayo ni mambo makuu ambayo ukiyatambua unapoanzisha biashara basi biashara yako itakua na itaendelea,chini hapa pia nimeorodhesha aina za mawazo ya biashara ili utambue wazo lako pia liko katika nafasi gani.

  1. Mawazo ya kiubinifu/uvumbuzi
  2. Mawazo ya bidhaa
  3. Mawazo ya mseto (ujumla)

Hivyo jitambue mapema umepata wazo gani na utakabiliana na changamoto zipi ili ujue namna ya kuzikabili muda utakapofika.


Karibu ujiunge na Branding group la Whatsapp huko utapata update za blog, Semina na Promosheni mbali mbali kutoka kwa wahisani,Jinsi ya kujiunga ni andika Nambari yako ya simu chini ya chapisho sehemu ya comment au tuma sms ya jina na namba yako kwenda namba 0684047323

Karibu sasa Kauli mbiu mabadiliko lazima

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango