Hali za kimaisha za vijana zisitumike kama mtaji wa kisiasa kwa vyama na wanasiasa.
Kwanza kabisa nitoe shukrani zangu za dhati kwa wewe ambae
umeendelea kunitumia ujumbe mfupi ,kunipigia simu na kunitumia barua pepe kwa
ajili ya shughuli hii,siwezi kuwataja wote kwa majina lakini ninautambua
mchango wenu bila kusahau wapenzi wa blogu hii ambao huendelea kutembelea blogu
hii hata kama sijaweka uzi upya niwashukuru kwa namna ya kipekee kabisa.
Baada ya kupita kimya kidogo cha kutokuwa na uzi nimeonelea
kwanza leo tuzungumze kidogo na vijana wa taifa hili maana hakuna familia
isiyokuwa na kijana au vijana katika nchi hii, hata kama hatakuwepo kijana basi
kutakuwa na kijana mtarajiwa.Tuko katika kipindi cha uchaguzi hivi sasa na watu
wengi wanajitahidi kupata nafasi au sehemu ya kujishikiza kwa kipindi hichi ili
angalau na wao wapate japo kidogo kitu katika mzunguko huu wa kampeni na
mchakato wa uchaguzi kama mlivyoona kwa sasa kuna kampeni na zoezi la
uandikishaji wapiga kura ambapo zinatumika mashine za BVR asilimia kubwa ya
waandikishaji ni vijana hivyo katika kipindi hiki vijana watapata sana ajira za
muda mfupi kwa ajili ya uchaguzi.
Lakini dhumuni langu kutoa uzi huu ni kuwakumbusha tu vijana
wasitumike kama mtaji wa kisiasa aidha kwa chama au kwa mwanasiasa, tuko katika
kipindi cha uchaguzi mkuu wa serikali asilimia kubwa ya watendaji wakuu wa
serikali wanaenda kubadilika kupitia uchaguzi huu hivyo asilimia kubwa ya
mipango mipya na ahadi za zamani zinakuwa zimefikia kikomo kwa sasa labda tu
kukamilisha utaratibu wa zile zilizoanza kabla,lakini kumekuwa na wimbi kubwa
la misaada na mipango chanya kwa ajili ya vijana na wajasiriamali wadogo kwa
ajili ya kuwasaidia kuwainua kiuchumi.
Nnawaasa vijana kuwa makini na fursa hizi kwani nyingine ni
kwa ajili tu ya uchaguzi na kampeni hivyo wanaweza kupoteza malengo yao ya muda
mrefu ambayo wamejiwekea kwa kujiingiza katika kitu
cha muda mfupi ambacho kitakugharimu muda mrefu baadae,
Ushauri kwa serikali.
Serikali inajua takwimu za vijana wanaobaki na wanaoingia
kazini kwa mwaka
Takwimu zinaonyesha kila mwaka wanahitimu vijana kati ya
800,000 –1,000,000 lakini nafasi za kazi zinazotakiwa ni kati ya 400,000 hadi
600,000 hivyo hadi hapo tayari inaonyesha kila mwaka tunaidadi kubwa ya vijana
ambao wamesoma lakini hawana ajira kila mwaka.Serikali itafute au itengeneze
mfumo thabiti ambao utasaidia nchi kuwa na usawa na uhalali katika suala la elimu na sio kushusha viwango vya ufaulu ili tupate
wahitimu butu kwa ajili ya kazi zenye makali,
Nafikiri serikali iongeze makali katika viwango vya ufaulu
na wanafaulu pia wafaulu kihalali na wanaofeli pia wafeli kihalali lakini
itambulike tu hakuna mtu asiekuwa na msaada kwa mwenzake leo hii dunia nzima
waliosoma wanafanya kazi kwa wasiosoma hivyo,serikali inaweza kutengeneza hata
vyuo vidogo vidogo kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi waliofeli na kuwapa masomo
na maandalizi ya jinsi ya kuishi na ujuzi wa vitu nje ya shule na nyumbani
ambapo kama kijana akipewa elimu sahihi akitoka hatakwenda kujibweteka tena na
kusubiri second selection au kwenda kusubiri aliesoma amalize ili amsaidie
sababu atakuwa na chachu na mafunzo thabiti ya nini cha kufanya sehemu aliopo,
ambapo na alisoma akimaliza atakuta sokoni kazi za weledi wake zinamsubiri
hivyo ataingia moja kwa moja kazini
tofauti na sasa mwenye weledi wa dokta anafanya kazi ya udreva.
Comments
Post a Comment