Jifunze kufanikiwa kwa kiwango ulichopo

Kila biashara hutegemea kufanikiwa katika eneo lake la ushindani lakini asilimia kubwa hufeli kwa vile hazitambui mafanikio yanahitaji vitu gani,chache ambazo hutambua uhitaji wa mafanikio hufanya ushindani na kujitengenezea nafasi katika soko, leo nitatoa siri 7 za vitu ambavyo vitakutengenezea mafanikio kwa sehemu na kiwango ulicho nacho kwa sasa:-

1.IBRAND BIASHARA YAKO.

Branding sio neno geni na nimeshalitaja na kulielezea sana hivyo itengenezee muonekano wa tofauti katika soko lako, utofauti wako kwenye soko utakao kupa nafasi katika soko lako la ushindani na mafanikio ni matokeo ya ushindani.

2.UTAFITI

Usifanye vitu kwa mihemko au kukurupuka  fanya utafiti wa kutosha kuhusu biashara yako  kuanzia vitu kama Eneo,Asili ya biashara, wateja wako,ushindani na aina zote za washindani, Mbinu shirikishi na vingine vingi, mafanikio hayawezi kuja iwapo hautajua uko katika kiwango gani na unakutana na ushindani aina gani,hilo unaweza kulielewa kwa kufanya utafiti tu hivyo tafiti ni msingi wa mafanikio yako.

3.MBINU (MIPANGO)

Tengeneza Mipango ya mizuri ya mbinu za kupambana na kujitangaza katika soko lako ambazo utakuwa unazitumia kulingana na muitikio wa wateja wako, sio unakuwa na mbinu moja tu kwa ajili ya biashara  ikifeli basi ni kama biashara pia imefeli  lakini kwa zile ambazo zimetengeneza mara zote huongeza mapato kwani inakuwa inapata nafasi katika masikio na macho ya wateja kwa mabadiliko yote ambayo yanakuwa yanafanyika Mfano:" Kampuni ya vinywaji baridi ya cocacola hubadili mipango mbinu kwa kila kipindi cha miezi mitatu na kuna kipindi hata chini ya hapo kulingana na aina ya mbinu tumika hiyo yote hufuata utaratibu maalum uliopangwa kulingana na soko lao la vinywaji" hivyo ili kufanikiwa inakupasa kutengeneza mpango mbinu wa biashara yako kulingana na soko lako.


4.SIMAMIA LENGO KUU.

Biashara nyingi zinayumba na nyingine kufeli kutokana na sababu ya kutokushikiria lengo mama (Kuu), wamiliki wa biashara huwa na tamaa fedha kuliko kutatua tatizo, usiwe na tamaa ya pesa kuliko asili ya biashara yenyewe, ambayo ni kutatua tatizo la mteja hivyo unatakiwa kumfikria zaidi mteja kuliko pesa, ambapo yenyewe inakuja kama zawadi ya kutatua tatizo la mteja wako, hivyo zingatia sana wateja kuliko faida au pesa, hivyo kila biashara inalipa ni kuisimamia tu kwa ari na lengo lake mama,  wazo lako la mwanzo lilikusukuma hadi ukafungua hiyo biashara ndio la kulisimamia haya yanayokuja baadae ni ya kuliboresha tu lakini yasilibadilishe hata kidogo. Mfano" Utakuta mfanyabiashara anaduka la mahitaji ya nyumbani baada ya muda anapata wazo au faida ya kumtosha anaamua kuongeza biashara anaanza kuuza na vinywaji, ile biashara ya vinywaji ikimlipa anaanza na kuhamisha mtaji anauweka zaidi kwenye vinywaji baada ya muda,kikifika kipindi cha mauzo kuwa chini biashara inayumba na kwa vile yeye haikuwa ya kwanza itamsumbua hivyo anaweza kufunga au kurudi kwenye biashara ya awali ambapo kama kulikuwa na washindani wengi watakuwa wamegawana wateja wake hivyo biashara itayumba au hata kufeli kabisa. hiyo yote ni sababu ya kutokusimamia lengo kuu.Kila biashara inalipa.

5.AHADI YAKO IENDANE NA UTENDAJI KAZI

Hili pia ni tatizo lingine katika biashara unapofanya branding unatengeneza neno na picha ya biashara yako katika vichwa vya wateja wako lakini utakuta kuna baadhi ya biashara zinakinzana na ahadi zilizoweka zenyewe Mfano" Bisahara imeweka meme au ahadi ya "haraka na ufanisi" lakini ukifika eneo la biashara vitu havifanyiki katika kasi ya uharaka na ufanisi ni mdogo, hii inapunguza sana wateja hivyo jitahidi sana kuendana na ahadi uanyoweka ndani ya vichwa vya wateja wako.

6.HUDUMA KWA WATEJA

Huduma kwa wateja ni sekta nyeti sana katika biashara ni moja kati ya uchawi wa biashara lugha, mapokezi, huduma na kauli nzuri hivyo ni baadhi ya vitu vinavyopatikana katika huduma kwa wateja, lakini sehemu nyingi hutolewa chini ya kiwango ambapo humuachi mteja nafasi ya kutokurudi katika biashara hiyo, jitahidi sana kuboresha huduma kwa wateja katika biashara yako mapokezi na ukarimu kwa mteja ni dawa ya kumrudisha kesho na kesho kutwa.


7. JITANGAZE KWA KIWANGO CHAKO

Tumia vitu vyote unavyohisi vinaweza kuisaidia biashara yako kufika kwa mteja mtarajiwa, kwa sasa kulingana na kukua kwa teknolojia sehemu nzuri zaidi kujitangaza ni katika mitandao, tumia mitandao kwa ajili ya biashara yako na itakuletea mafanikio, tengeneza tovuti, fungua kurasa katika mitandao ya kijamii, Blogu, Podcast na vingine vingi....Kujitangaza kupitia mtandao kwa kiwango cha chini ni nafuu kuliko kujitangaza kwa njia nyingine.



Hivyo ni baadhi ya vitu vitakavyokusaidia kufikia mafanikio ya biashara yako kulingana na hatua na kiwango ulichopo,Kila biashara inalipa ndio maana yule anaefanya biashara ya vitumbua na yule anaefanya biashara ya madini wote wanafamilia na familia zinaishi na kupata mahitaji kupitia biashara hizo hizo.


Kwa huduma ya kufanyiwa Branding na ushauri kitaalamu kwa biashara yako wasiliana nami kwa mawasiliano 0684047323. Karibu.Pia unaweza kutembelea kurasa yangu ya facebook  www.facebook.com/chumaelisha.

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango