Jinsi ya kujitangaza na ujumbe kumfikia mteja unaemtaka

Biashara nyingi zimekuwa zinafeli kufikia malengo ama kufanikiwa kwa sababu ya kutokutambua ni nani na aina gani ya ujumbe/ wateja ambao  ujumbe unatakiwa uwafikie.

Kwa mjasiriamali kutambua uwanja wako wa kujitangaza ni jambo la muhimu sana, kama hujui utakuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa acheze ujumbe utatoka lakini hautawafikia walengwa hivyo utakuwa hauna matokeo chanya yoyote sababu waliouona hauwahusu, sababu kutambua uwanja wako ndicho kitu cha kwanza ambacho hukupa muelekeo na maandalizi safi ya kampeni na promosheni zako.

Kwanini ni muhimu biashara kutambua aina ya uwanja na watu inaowataka? ili kufanya tangazo lako liwe na mashiko ni lazima lionekane kwa mtu sahihi, na ukishatambua ndipo hapo unaweza kutengeneza ujumbe na muonekano utakaoendana na malengo ya uwanja wako.

Ili kujua aina na mteja wako unaetakiwa kumfikishia ujumbe ni lazima utambue na kuzifuata hatua zifuatazo.

1. Chagua aina( Kifaa cha mawasiliano)
Unatakiwa kuwalisiliana na watu na hii itakuwa kwa aina uliochagua(uso kwa uso, simu, mitandao ya kijamii, tovuti n.k), kitu cha muhimu hapa ni kuchagua kifaa sahihi ambacho kitakuwa rahisi kwako na kwa mteja wako kufanya mawasiliano.

2.Fanya utafiti.
Utafiti ni moja kati ya njia nzuri ambazo zitakufikisha mapema kwenye kumtambua mteja wako, kwa utafiti huo utaongeza maarifa kuhusu masoko mengine na washindani wako pia. Kikubwa hapa angalia jinsi ambavyo washindani wako wanafanya kazi na wateja wao na pia kwa njia gani pamoja na utafiti pia unaweza kutumia mitandao kusoma na kutambua njia,mbinu na aina ya wateja wako.

3.Tafuta mtandao ambao wateja wako wapo.
Hii haihusiani na kutumia mitandao ya kijamii ambayo inafahamika sana au inatumiwa na watu wengi hii inamaanisha ukishajua aina ya wateja wako pia utajua sehemu sahihi wanakopatikana , huko ndiko unakotakiwa kuupeleka ujumbe wako sio kung'ang'ania mtandao kisa tu unawatu wengi.

4.Tengeneza mahusiano imara( Mtandao)
Tengeneza mtandao imara kupitia muonekano wako ili popote mtu atakapo ona kitu kinachoendana na kada yako akuchague, usiwe mtu wa kubadilika badilika tu, hii itafanya wateja wako wasikutambue mapema na inaondoa uaminifu, leo unanembo ya kijani kesho nyekundu keshokutwa ya bluu. Tengeneza muonekano sahihi ambao utausimamia.

5. Usiondoke sokoni
Hii inamaanisha usiwe kwenye ushindani kwa kujaribu,unakuwepo na kuondoka, unatakiwa uwepo katika ushindani siku zote ili soko liendelee kukupa nafasi, na mteja aendelee kukuchagua hii ni zaidi ya kujitangaza na kuendesha kampeni na promosheni,hapa inahusisha na kuonekana kwenye semina, matamasha, kushiriki shughuli za kijamii na kadhalika.

Ukivifanya hivyo vyote kwa ufasaha utaweza kugundua na kupeleka ujumbe sahihi kwa yule anaetakiwa afikishiwe ujumbe.

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango