Wazo la 3

Vijana wengi na watu wengi wamekuwa na shida ya ajira sasa hivi ambapo imefikia hatua inabidi aajiriwe katika sekta isiyokuwa na weledi wake na wengine kukosa kabisa,wengine wanapesa za mitaji lakini hawana wazo bora la biashara waanzishe kitu gani ili kiwe na mafanikio kwao.
Leo hii tutaenda kuangalia wazo jingine la biashara ambalo litawahusu sana akina mama na akina dada,katika mzunguko wa maisha wote tunatakiwa kutambua Mungu ni kiongozi na katika uumbaji wake hakuna alieumbwa kwa bahati mbaya na ndani ya kila mtu kuna kitu cha ziada ambacho Mungu amemuwekea kulingana na utashi wake..Leo nitawapa mbinu ya kujiajiri kwa madada ambao wanasema hawana ajira kabisa.
Kuna baadhi ya kazi ambazo kama mdada ama mwanamke ukifanya kwa uhakika zinakutoa na hazihitaji chuo wala cheti ni kipaji na baraka tu baadhi ya kazi hizo ni pamoja na ususi,kutengeneza vitafunwa(bites),kufanya usafi na kadhalika,kama wewe unajijua unakitu unachoweza kukifanya kwa ufasaha kwa moyo wote bila kushurtishwa basi usiseme huna ajira.
Nitaongelea upande wa ususi,anza kwa kufanya na majirani zako muite jirani ambae anabadilisha mara kwa mara mtindo wa nywele zake anza nae kwa kumsuka vizuri na kisha kumwambia afanye kazi ya kukutangaza tu kila atakae muuliza amesuka wapi akutaje na hata akiweza atoe namba, kisha taratibu anza kusuka na walioko karibu na wewe kwa bei pungufu huku ukiwapa punguzo kama ukileta wateja 5 basi ntakusuka kwa nusu bei, wanawake wanapenda sana urembo hivyo kama ukiamua kuifanya kibiashara itakutoa kwa watu kusafiri na kukufata nyumbani hadi baadae kuwa na eneo lako maalum.
Hakuna biashara ambayo inakua kwa siku moja na iwe na mafanikio ya muda mrefu hivyo hata kwa hii pia inahitaji muda kujitolea,juhudi ,uwezo na maarifa kwa ajili ya kuifanikisha usijihisi unaweza kusuka na kuifanya ipime kwanza kama inaendana na wewe kisha ndio uifanye.
Kupata na kuendelea kupata mawazo na ushauri wa biashara endelea kuwa karibu na mimi kupitia Instagram na Facebook : Elisha Chuma, Blogu: www.elishachuma.blogspot.com,Barua pepe : elishachuma@gmail.com. Pia tuungane kwenye maisha mseto ya Times fm(100.5) kila siku ya jumatatu hadi ijumaa saa 12:45 alfajir - saa 1 :00 asubuhi na Kila siku ya Alhamis kipindi Hatua 3 saa 5:30 asubuhi - saa 6:00 mchana radio Times Fm(100.5)

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango