Jinsi ya kutengeneza Brand yako online
Utengenezaji wa
brand umebadilika sana kulinganisha na
hali ilivyokuwa zamani,na hii inachangiwa na ukuaji wa teknolojia na ufanyikaji
wa dunia kuwa kijiji hivyo hali hii imepelekea
hadi mfumo wa biashara nao kuhamia huko, mauzo yanayofanyika nje ya
mitandao asilimia kubwa kwa sasa ni
matokeo ya ushawishi ama kujitangaza vizuri kupitia mitandao ya kijamii .
Japokuwa tumekuwa
tukiyaona na kuyashuhudia mabadiliko haya , bado hatujaweka mkazo mkubwa katika
soko hili la kujitangaza online, mfano serikali inasema kuboresha vifungashio
na muonekano wake hii inamaanisha lazima na soko la online( Mtandaoni) Uliangalie
kama unataka biashara yako itoke sababu mtandao unafanya kazi dunia nzima na
hicho ndicho kilichoufanya upate mwamko na kasi kubwa sababu unapokuwa kwenye
mtandao unauwezo wa kujitangaza na dunia nzima ikakuona sasa ishu tuliyokuwa
nayo ni kwamba kila kitu tunatengeneza chini ya kiwango lakini tunahitaji tuuze
kwa kiwango cha juu.
Mfano: Huwa
mara nyingi nasema kufanikiwa ama kufeli
kwa biashara yako kunachangiwa ama kunatengenezwa na uwezo wa brand yako,
taarifa ilionyesha tumepunguza mapato ya nje kwa billion kama 3 hivi ile
ilikuwa ni kutokana na brand kuwa chini ya kiwango kama unatengeneza vizuri na
umejitangaza vizuri huwezi kushusha mauzo kwa kiwango hicho hata kama
kodi,makato yakiongezeka ukiwa umejibrand vizuri unauwezo wa kulifanya soko
likufate, mfano kama wewe ni muuza maandazi mzuri na unauza kila siku maandazi
sh.100 unauwezo kuwaambia wateja wako unga wa ngano umepanda maandazi sasa hivi ni 150 na watu wakakubali
bila shida lakini kama wewe sio kiongozi ukipandisha inamaana watu watakuhama
tu sababu wewe sio kiongozi na brand yako haina huo uwezo.
Kwa hiyo mtandao kwa
sasa unanguvu kubwa sana katika mauzo ya biashara yoyote watanzania milioni 20,
wanatumia mtandao hivyo inamaanishau ukitumia mbinu na njia sahihi za
kujitangaza basi unaweza kuwafikia watu milioni 20 wanaotumia mtandao,sasa ishu
inakuja haya mambo huku tunayapokea na hakuna mtu wa kutuongoza hivyo watu
wanajifanyia fanyia tu bila kuwa na muongozo sahihi wa jinsi ya kufanya na hii
ni tatizo kubwa sana, utakuta brand inauwezo wa kuwa kubwa na kuwafikia vizuri
watu wake lakini haitumii ipasavyo mtandao husika ama maudhui tofauti na kile
inachokifanya hii inapelekea wateja wengi
kuishia njiani na kutokufikia kwenye ununuzi.
Twende mbele turudi
nyuma mteja haumpati kwa kumlazimisha, ishu ambayo huwa wafanyabiasharana
wajasiriamali wanasahau ni kuwa mteja haumlazimishi kununua kwako ila
unamshawishi tu, wewe utatumia weledi na nguvu ili kumpata ila yeye atatumia
uasili wake tu aidha kukukubali ama kukukataa.kwa hiyo ushawishi wako wote
unapoufanya ni lazima uufanye ukitambua unaitafuta asili ya mteja, hili
limekuwa tatizo kwa biashara nyingi sababu wamekuwa wakitumia komand( Ulazima)
hadi kwa wateja wao yaani wanaweza wakafanya hata tangazo ambalo halina
uhalisia ilimradi tu wao wanataka bidhaa zao zieleweke lakini matangazo
mengi yenye mvuto na yanayopenda ama
kusikilizwa huwa ni yale yaliyoingiza uhalisia ndani yake sasa hapo ndio inakuja
kujitathmini tangazo langu lina uhalisia ndani yake ama nnalazimisha watu
kutumia bidhaa/huduma yangu.
(Tangazo hadi mtoto
analikariri sio kama ni mteja wako ila lina uhalisia na anaweza kuwa balozi
mzuri kukumbusha kuhusu tangazo lako mara nyingi awezavyo)
Sasa basi ni lazima
kaka mfanyabiashara ama mjasiriamali kuitambua nguvu ya mtandao katika
kujitangaza na usifanye kama ni kitu cha kupita ama kujifurahisha unapotaka
kufanikisha hilo kwa ufasaha ni lazima uifanye kama sehemu ya masoko kwako na
biashara yako.
Baadhi ya vitu
ambavyo unatakiwa utambue kama mfanyabiashara ama mjasiriamali.
- Mtandao ni sehemu ya kutafuta masoko
- Tengeneza jina halisi
Lisiwe
jina gumu,liwe rahisi kuandikwa ,kutamkwa na pia kupatikana
- Muda
- Ongeza shea za masoko
- Panua soko lako
- Miliki aina.
Kitu
ambacho unatakiwa kutambua kila sehemu kumekuwa na makanjanja hivyo unapoamua
kutafuta watu ama sehemu za kujitangaza hakikisha ni sehemu ambazo zinaaminika
pia process ya kutengeneza brand sio ya siku moja ama wiki hivyo tumia mda
mwingi kufuata kanuni zake
- Muonekano
- Picha ( Image)
- Maudhui
- Tengeneza line/ Focus
Muda
:
Muda mzuri wa kutuma
matangazo yako kupitia mitandao ya kijamii nitakuandikia baadhi tu.
- Faceboo = 7 mchana - 10 mchana
- Linkeldin = 11 - 12 jioni
- Instagram 11 - 12 jioni ( 10 alfajir)
- Pinterest - 2- 5 usiku
- Google+ = 3 - 5 usiku
Umenena vzr sana nimeongeza kitu juu ya kile nilichokuwa naelewa
ReplyDeleteSafi sana ndugu.
ReplyDeleteNice Bro now nimeelewa nianzie wapi na nimalizie wapi
ReplyDelete