ENEO LA BIASHARA



Kumekuwa na changamoto kubwa kuhusiana na lipi ni eneo sahihi la kuiweka biashara yako,watu wamekuwa  na kasumba na kujifanyia hadi imefikia hatua hawajui athari zimeletwa na nini.

Na hii inachangiwa mara nyingi na kufanya vitu bila kufuata weledi ama kuonana na washauri wa masuala hayo,mara nyingi biashara zinapoanza mwenye biashara hutafuta kuwa na sehemu tu ya kumfanya aonekane na yeye ana sehemu ya uelekezi (Physical  address) lakini inapokuja suala la kwanini amechukua eneo hilo huwa hana majibu ya moja kwa moja kama inamfaa ama haimfai kwa kulingana na biashara yake.

Hili limekuwa tatizo kubwa sana na madhara yake yanaweza kuwa hayako moja kwa moja ila yanakutafuna mfano: ukiwa kwenye location sio unaweza kuwa unapata wateja wa mwisho na wa kwanza wanaishia kwa mwenzako,hii itasababisha biashara kuwa na mauzo ya kawaida na kutokukua ,ikichelewa kukua inamaanisha malengo yatapishana na mipango ambapo kufeli kwake kunakuwa mlangoni lakini chanzo cha yote ni kukosea eneo la kuweka biashara yako.Na kwa vile halitakuwa kwenye mawazo yako unaweza kuongeza nguvu kwenye masoko na mauzo kwa kuhisi kwamba unakosea huko hivyo inaweza kukugharimu pia na kujikuta unafeli bila kugundua kama unafeli sababu unauza/unatoa huduma lakini haifikii kiwango kinachotakiwa.

Sasa baadhi ya madhara unayoweza kupata baada ya kukosea eneo la biashara :-
  1. Kukosa wateja wa kutosha
  2. Kutumia nguvu kubwa kubrand
  3. Mauzo kuwa chini
  4. Biashara kushindwa kukua
  5. Msongo wa mawazo - Afya ya akili ( Presha,Maamuzi mabovu,Hasira, Uchovu na mengineyo.


Ushauri: Usichague eneo la kuweka biashara yako kwa kufuata mihemko,tumia washauri na wataalam ili upate ushauri stahiki.

Changamoto ya Biashara aina moja Frem 10 eneo moja.

Hili pia ni moja kati ya changamoto zinazowakumba wafanyabiashara, na imekuwa kama kasumba  kuona mtaa wa bidhaa moja , mara nyingi hii imetokea sababu ya maamuzi yasiyokuwa na tafiti ama kuhesabu faida kuliko gharama ,na pia kufanya biashara kwa kufuata stori ama mihemko.

Lakini pia unatakiwa kutambua biashara ni eneo la kusahihisha makosa ya mshindani,hivyo inawezekana kukawa na makosa ambayo yanaendelea kurekebishwa na washindani wako.

Ukiwa kama mfanyabiashara haijalishi unaenda kuweka eneo gani
  1. hakikisha eneo  unapoipeleka biashara yako lina sababu ya wewe kuwepo hapo.
  2. Tambua asili ya eneo husika usiige kuwafata wenzako, ( Commercial na Residental)
  3. Eneo ambalo wateja wako watafika kirahisi ( Haimaanishi kwenda kubanana na wenzako hapo hapo)
  4. Biashara inabebwa na
    1. Mbinu - Kuwashinda wapinzani wako
    2. Mipango - Kufikia malengo
    3. Utatuzi - unatatua tatizo gani na huduma yako.
  1. Usichague location kwa kufuata historia ( Eneo hili steshenari inalipa)
  2. Fanya utafiti na linganisha na hali yako ndio uingie kwenye hilo eneo.

Kwenye mbinu za biashara inaruhusiwa kabisa kujazana eneo moja ili kumsaidia mteja wenu kuchagua kile kilichobora pale pale.na hapo ndio huwa mbivu na mbichi huonekana mwenye uwezo wa kupata wateja na asiekuwa na uwezo.

Kuwa katika ushindani kama huo kusikukatishe tamaa, kama ni eneo lako sahihi na ndio sehemu ambayo unaamini itakutoa na utapata zaidi kile ambacho unafikiria basi usiogope japo inagharama kwenye ushindani kama huo.

Na kinachofanya ushindani kuwa hivyo ni wanaweza kuanza wachache ila nguvu ya ushindani ikawashinda wakafeli  wakakaa na kuangaliana then anakuja mwingine anaekwapua fursa nae anajiunga na kundi hivyo wanajikuta wanajisomba hata 10 bila kuona tofauti yao sababu ushindani wa hivyo unafaa ka biashara inayotoka haraka yaani iliyoko kwenye mzunguko wa kutosha wote mpate na muendeleze.

Katika dunia hii kila kitu kina faida na hasara zake.

Faida .
  1. Ushindani huongezeka
  2. Wateja wengi watafika eneo hilo
  3. Chachu ya kuongeza thamani na huduma bora kwa wateja
  4. Mteja atakuwa na uhuru wa kuchagua bidhaa
  5. Mfumuko wa bei unaweza kudhibitika

Hasara:
  1. Gharama za ushindani ( kila siku kutafuta makosa ya mwenzako)
  2. Biashara nyingi hufeli sababu siku zote huwa kuna mshindi
  3. Kugawana wateja
  4. Changamoto nyingi amabazo hupelekea ufanyaji kazi hafifu.

leo nitaishia hapa ili kuendelea kupata machapisho yangu bonyeza kitufe cha (follow) upande wa kushoto chini na kila nitakapotoa uzi utapata taarifa ama kwa wale walioko katika mtandao wa facebook unaweza kulike page yangu Elisha Chuma, Pia unaweza kuungana nami kwa kundi la whatsapp kwa kutuma namba yako kwenda 0684047323.

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango