Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.


Leo nimepata nafasi ya kuandika waraka huu kwa ajili ya kuwakumbusha kidogo wafanyabiashara wenzangu na wajasiriamali wenzangu kuhusu dhana moja ya muhimu sana iliyopo katikati ya mauzo na kujitangaza.

Biashara nyingi sana sijajua kama ni kwa sababu ya kutokujua misingi ya biashara ama kutokuwa na uelewa wa kutosha na biashara zinafanya mambo kinyume na vile ambavyo inatakiwa na kujikuta zinatumia gharama kubwa kutengeneza mauzo kuliko ambavyo ingapaswa kuwa.

Mara zote huwa nikipita na nikiwa kwenye semina huwa nawakaumbusha wafanyabiashara wenzangu na wajasiriamali kwamba siku zote usiwekeze kwenye kutafuta mauzo tu, kumbuka na kulijenga jina ama picha ya biashara, kuna faida nyingi sana za kujenga jina /picha katika kichwa cha mteja wako,lakini biashara nyingi hazifikirii sana kuhusu hilo bali wanawaza kuongeza mauzo tu.

Siku zote mauzo ni mazuri lakini mauzo bila ya kuwa na jina ni gharama,nimeshakutana na wateja wengi sana wenye kutumia kauli hii " Mimi ninabidhaa nzuri lakini mpinzani wangu ananishinda sababu yeye anajina, watu wengi wanaenda dukani kuulizia bidhaa kwa jina lake, mimi wanatumia kwa matumizi yake ambapo inaniwia vigumu kushindana nae"

Mfano huu na mingine mingi ya kufanana na hii ni mifano hai ambayo ni kilio cha biashara nyingi sana, ambapo hujikuta zinatumia gharama kubwa kujitangaza ama kuitangaza bidhaa bila kujenga jina.Mauzo bila ya kuwa na jina (Brand) ni gharama sana.

Unapouza ama unapotangaza biashara yako ili inunuliwe peke yake maana yake ni kwamba utakuwa unaitangaza kila siku ili upate wateja, na pia hautafahamika kwa wateja wako zaidi ya bidhaa tu, lakini ukiwa unajenga jina unakuwa na nafasi kubwa ya kuwa mshindani sokoni hata kipindi ambapo haujaweka nguvu nyingi katika kujitangaza jina lako litakupa nafasi kwenye soko lako.

Faida za jina ni pamoja na, kuwa na uwezo wa kuwa mshindani sokoni,kuwa na uwezo wa kupanga bei,kuwa na uwezo wa kuigwa ,kukaa ndani ya vichwa vya watu,kuwekwa kumbukumbu muda wote ambao unajitangaza hata ule ambao haujitangazi.Makampuni makubwa yanatumia muda mwingi kutengeneza picha ndani ya kichwa cha mteja wake, kuliko mauzo kwa kuwa yanaamini kuwa mteja akishapata picha na ikatunzwa ndani ya kichwa chake, yatakuwa na kazi ya kuwakumbusha tu sio tena kujieleza kama ukiwa hujajenga picha.

Umeshawahi kujiuliza kwanini matangazo mengi barabarani huwa hayana maelezo mengi tofauti na picha ama nembo za kampuni husika?, wakati ni gharama kuyaweka hapo barabarani? Hiyo nafasi ungeipata wewe ungesema tena barabarani ujaze bidhaa zako zote na uandike kila unachofikiria ili kuhakikisha unatangaza kila kitu kupitia hapo.Lakini ni kwanini basi haiko hivyo?

Maana ya kufanya hivyo ni kwa sababu wanahitaji kumkumbusha mteja kuhusu nembo ama picha yao tu na mteja atakumbuka bidhaa zao, mathalani tufanye ni mtandao wa simu, ukiona tangazo barabarani kwenye zile nguzo za taa limechorwa nembo ama picha tu wewe kichwani kwako zitakuja huduma zote za kampuni hiyo…( Kurusha fedha,Kutuma sms,kutumia data, kumtafuta mtu wa mtandao huo,kumpigia mtu wa mtandao huo, yaani utakumbuka kila kitu ambacho kinahusiana na mtandao huo ) lakini kama wangeandika mfano ni promosheni ya vocha utakumbuka kuhusu vocha tu na kulinganisha na mtandao mwingine basi ukawa umemaliza kuwafikiria.Lakini yote hayo yanatengenezwa na kujenga picha/jina ndani ya kichwa cha mteja husika.

Sasa basi biashara nyingi zinafungwa kwa sababu gharama za kujitangaza ni kubwa sana kuliko mauzo ama zinachukua nafasi kubwa ya faida, hivyo inakuja kuingilia na matumizi, biashara inajikuta inafeli kuendelea na kufungwa,usitumie nguvu nyingi sana  kwa ajili ya kupata mauzo tengeneza mauzo yako kupitia kujulikana kwako na jina lako,itapunguza sana kiwango cha gharama ya kujitangaza kwa nguvu kama mwanzo.Lakini tatizo kubwa la wafanyabiashara huwa wanataka kila tangazo liwe ni la kuleta mauzo bila kujenga jina .Na hatua ya kujenga jina sio hatua ya siku ama mwezi hivyo wengi huona kama wanapata wateja  sio shida hivyo kuendelea tu ila muda wa kutumia jina ama brand ukifika wanajikuta hawana tena uwezo wa kufanya hivyo ,biashara inafungwa kwa sababu inategemea mauzo peke yake.

Hivyo badilisha namna ya kujitangaza kwako,namna ya kuhudumia wateja wako na hata namna ya kutengeneza mpango chapa wako,ijenge brand yako ikujenge.ila tambua kujenga brand sio shughuli ya siku 1 ama 10 inachukua muda lakini matokeo yake ni makubwa.kwa biashara yenye malengo ambayo inatakiwa kukua na kusimama kwa muda mrefu ni lazima itumie mbinu za kuwepo sokoni muda mrefu.

Amka leo usiendelee kuiweka biashara yako katika hatari ya kufeli sababu ya kufikiria mauzo peke yake,tengeneza jina huku unajenga mauzo mwisho utakuja kuona faida yake biashara inayodumu sokoni  ni ile inayojijenga sio inayojitangaza tu,tengeneza brand ya biashara yako leo Ili upate nafasi sokoni .


Mauzo ni mazuri lakini mauzo bila kujenga jina ni gharama sana,na hiyo gharama ni ngumu kuisimamia kwa biashara zinazoanza na zinazoendelea kukua.

Comments

  1. Da ii post nimechelewa kuiona labda nlikuw mdogo sema jamaa umetoa elim ambayo inaishi kwa kizazi hiki nimeelewa napafanyia kazi

    ReplyDelete
  2. 1xbet | 1xbet | Bet with a Bonus - RMC | Riders Casino
    1XBet allows you to 출장마사지 bet on 1xbet korean any favourite horse https://septcasino.com/review/merit-casino/ races or any other herzamanindir.com/ sporting event. ✓ Get up casinosites.one to £300 + 200 Free Spins No Deposit

    ReplyDelete
  3. Uko vizuri sana kaka mkubwa

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango