Kwanini unatakiwa kumuweka ndani mtoto mchanga siku 40 baada ya kuzaliwa.
Muda na wakati unatupa mkono sana katika kuijua kweli na hii inasababishwa na vitu vingi mabadiliko ya uchumi,hali ya hewa,mitindo ya maisha,kuiga na vichocheo vingi vinatufanya tunabadilisha ile kweli kuwa kawaida, leo nitaongelea suala la kwanini mtoto anapozaliwa anatakiwa kuwekwa ndani kwa siku 40 ni kitu ambacho tumekikuta tumekirithi lakini tunakiacha, Je vizazi vyetu ama kizazi chako cha 4 kitafahamu kama kulikuwa na kuweka 40 kama kuanzia kwako haujaweka 40?.
Historia,zama na ukweli vinatupeleka mbali sana lakini hii dhana ya 40 haijatumika kwa mtoto tu vipo vingi leo tutaangalia kwanini mtoto.
Sasa basi katika mwili wa binadamu kuna kitu kinaitwa Aura hiki hauwezi kukishika wala kukigusa ni kama tabaka lililopo juu ya mwili wako ambalo linakusaidia na kukukinga na nguvu za nje,mfano unaweza kutembea ukahisi mwili umesisimka ghafla tambua hapo aura yako imefanya kazi,ama umepima na unaumwa lakini hujanywa dawa na unajiona mzim tambua aura imekuponyesha vipo vingi kuhusiana na hili nisiende ndani sana,mtoto anapozaliwa aura yake inakuwa haijajitengeneza hivyo zile siku 40 huwa za kuitengeneza aura na kuifanya ikomae iwe na uwezo wa kupambana na nguvu za walimwengu,mzunguko huu hutumia siku 40 ndipo inakuwa imekomaa ukimtoa ama ukimkutanisha na walimwengu kabla ya muda wake inamaana aura yake inaweza kuathirika sababu itajitengeneza tayari ikiwa na madhaifu, mfano: mtoto akiwa mchanga kabla ya siku 40 ukimtoa akakutana na watu wa aina mbalimbali wote hawawezi kuwa sawa kiafya,kiusafi,kimatendo,hata kiimani hivyo ni rahisi kwa mtu anaembeba mwanao kupenyeza ama kumuambukiza kitu ambacho hawezi kukikataa sababu aura yake haijakomaa.
Sasa wazazi wa siku hizi akimaliza tu kujifungua mtoto yuko kwenye mtandao,tambua ile ni nafsi changa bado haijawa ana uwezo wa kupambana kabla ya kukomaa tayari unaipeleka kwenye mapambano na kuna nguvu nyingi zisizo onekana zinazotafuta nafsi changa kuziharibu, unaweza kutoa nafasi ya kuharibu maisha yote ya mwanao kwa picha moja uliopandisha akiwa mchanga sababu ya mahaba yako na ulimwengu kutambua kama umejifungua,mtoto anaweza kupandikizwa magonjwa aura inakua na magonjwa ambayo sio ya asili ama kupandikizwa kusudi lisilokuwa la kwake mtoto anakuwa tofauti kabisa na matarajio kila siku unalalamika afya yake mbovu kumbe imeletwa na kuiruhusu dunia kukutana na mtoto akiwa bado hajakomaa.
Hakuna mama aisiependa mwanae hivyo siwezi kuwakumbusha kuwapenda,ila tukumbuke sio kila tamaduni tunazoziiga zinamanufaa na zina madhara ya moja kwa moja madhara yanaweza kuwa yasiyoonekana mara moja akakua nayo na ukayazoea ukahisi ndivyo alivyo kumbe sababu ilikuwa ni kosa la mwanzo.Kuna vitu vingi ambavyo vinahusisha 40,kama mtu akifariki watu hukutana tena baada ya 40,Yesu alifunga siku 40,Musa alifunga siku 40,wana wa israel miaka 40,Kuumbwa kwa mwanadamu ni Marhala ya siku 40,Nabiyallah Yunus Alayhi ssalam amekaa tumboni kwa siku 40 na vingine vingi.tulizingatie hili siku 40 sio nyingi mpe nafasi mwanao kuwa na afya,nguvu,akili,upeo na kusudi imara aliloandaliwa.MPENDE ZAIDI MWANAO WALIMWENGU WAPO TU.
mtumie ama mtag mama kijacho kwa faida na mafanikio ya kizazi na vizazi vijavyo.
Elisha Chuma.
Instagram:@elishachuma

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango