Eneo sahihi la kuweka biashara yako.

Tunapoelekea kuumaliza mwaka kila mtu anatakiwa kujichuja na kujitathmini ni sehemu gani ametelza ama amefanikisha kwa ufasaha na kuna wengine wanajitahidi mwaka usianze bila biashara zako kupata eneo la kuwekw sasa basi kumekuwa na changamoto kubwa kuhusiana na lipi ni eneo sahihi la kuiweka biashara yako,watu wamekuwa  na kasumba na kujifanyia hadi imefikia hatua hawajui athari zimeletwa na nini.

Na hii inachangiwa mara nyingi na kufanya vitu bila kufuata weledi ama kuonana na washauri wa masuala hayo,mara nyingi biashara zinapoanza mwenye biashara hutafuta kuwa na sehemu tu ya kumfanya aonekane na yeye ana sehemu ya uelekezi (Physical  address) lakini inapokuja suala la kwanini amechukua eneo hilo huwa hana majibu ya moja kwa moja kama inamfaa ama haimfai kwa kulingana na biashara yake.

Hili limekuwa tatizo kubwa sana na madhara yake yanaweza kuwa hayako moja kwa moja ila yanakutafuna mfano: ukiwa kwenye location sio unaweza kuwa unapata wateja wa mwisho na wa kwanza wanaishia kwa mwenzako,hii itasababisha biashara kuwa na mauzo ya kawaida na kutokukua ,ikichelewa kukua inamaanisha malengo yatapishana na mipango ambapo kufeli kwake kunakuwa mlangoni lakini chanzo cha yote ni kukosea eneo la kuweka biashara yako.Na kwa vile halitakuwa kwenye mawazo yako unaweza kuongeza nguvu kwenye masoko na mauzo kwa kuhisi kwamba unakosea huko hivyo inaweza kukugharimu pia na kujikuta unafeli bila kugundua kama unafeli sababu unauza/unatoa huduma lakini haifikii kiwango kinachotakiwa.

Sasa baadhi ya madhara unayoweza kupata baada ya kukosea eneo la biashara :-
  1. Kukosa wateja wa kutosha
  2. Kutumia nguvu kubwa kubrand
  3. Mauzo kuwa chini
  4. Biashara kushindwa kukua
  5. Msongo wa mawazo - Afya ya akili ( Presha,Maamuzi mabovu,Hasira, Uchovu na mengineyo.



Ushauri: Usichague eneo la kuweka biashara yako kwa kufuata mihemko,tumia washauri na wataalam ili upate ushauri stahiki.

Kwa huduma ya ushauri na maelezo zaidi usisite kuwasiliana nami kwa simu 0684047323. Kumbuka ili ufanikiwe ni lazima uwe na muongozo thabiti na ushauri stahiki kwa unachokifanya.


Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango