Baadhi ya sehemu ambapo watu wengi wanafeli na kunyanyuka kwao kunakuwa kugumu  ni kati ya muumganiko wa kile anachokiwaza na uhalisia,na hii inachangiwa sana na kutengeneza mipango isiyokuwa na uhalisia wa maisha ama mzunguko wako wa maisha yako ya kila siku.Usitegemee kuja kufanikiwa kwa mpango ambao utaubadilisha zaidi ya asilimia 40 ya maisha yako ya kila siku,hakikisha mpango wako unazingatia uhalisia wa mzunguko wa maisha na uwezo wa kuufanya uwe hai.Simamia kuunganishwa kwake.

Kitu kingine kinachowa rudisha nyuma watu wengi ni kuishi maisha ya wenzie,hata umempata roll model wako kamwe usitake kuishi kama anavyoishi yeye sasa hivi ukitaka uwe kama roll model wako anza kwanza kufatilia alifanya nini kabla ya kuwa kama alivyo usimuige kama alivyo sasa ila mfatishe alivyofanya hadi akawa kama alivyo sasa hivi.Kwenye akili unabeba ndoto kubwa ili uendane na roll model wako matokeo yake unafeli nakumfaidisha yeye.

Pia kingine na kikubwa zaidi unatakiwa kujitambua ili mawazo yako yaendane na uhalisia wako, ukijitambua utakuwa na uwezo wa kujiamini na kuiamini njia yako watu wengi wanafeli sababu hawajiamini,hii inafikia hata wazo la biasahara anatafuta kwa mtu mwingine ili afanikiwe yeye,hilo ni kosa kubwa haitakiwi kuomba wazo bora la biashara kwa mtu unalo mwenyewe ila unalipuuzia,ukimuomba mtu atakupa lakini atatoa kwa mzunguko wake wa maisha ambao hauendani na wako UTAFELI mapema.Jitambue na ujiamini ili uweze kuunganisha mawazo ya akili yako na uhalisia wako. UTAFANIKIWA.

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango