Muonekano wako ndio biashara yako

Biashara nyingi zimefeli sokoni sababu ya kutengeneza muonekano hafifu ama unaokinzana na aina ya asili ya biashara husika na bahati mbaya matokeo ya makosa ya branding huwa hayaonekani moja kwa moja kama ilivyo branding (chapa) yenyewe, chapa inatengenezwa ndani ya kichwa cha mtu hivyo kufeli na kufaulu kwake ni ndani kwa ndani ndio maana mara nyingi hufanywa kwa kufuata saikolojia ya mawazo ya mtu.

Sasa basi imekuwa ni ndoto ya watu wengi sana kuwa ama kuanzisha biashara zao,lakini na wengine tayari wameshaanzisha baadhi ya vitu ambavyo hutiliwa maanani sana kwa wengi ni upande wa bidhaa/huduma pamoja na eneo la huduma kwa sababu wazo la biashara haliji na muonekano hivyo huweka juhudi kwenye vitu ambavyo huhisi ama kuona ni vya muhimu sana,lakini sehemu ambayo huchukuliwa kawaida ni sehemu ya muonekano bila kujua biashara inalindwa na kusimamiwa na muonekano kwanza ndio vingine vinafuata,unapokosea kutengeneza muonekano ama chapa yako vizuri unakuwa kwenye hatihati ya kupoteza nguvu ya ushindani lakini pia wateja na hadhi ya biashara yako ama brand.

Asilimia kubwa ya wamiliki ama waanzishaji wabiashara hufanya kazi wenyewe pale wanapoanzisha biashara zao na pia hata sehemu ya muonekano huchukua jukumu la aidha kusimamia ama kutengeneza kwa muonekano anaoufikiria yeye kichwani ama kuona kwa jirani nakadhalika,wala sio makosa kabisa kufanya hivyo lakini ikiwa umefanya hivyo unatakiwa kwenda kwa mtengeneza muonekano ambae anaweledi na anatambua madhara na faida ya kazi yake kwenye biashara yako na soko lako pia lakini iwapo utakutana na wale wanaofanya kazi kusukuma siku ziende utakuwa ni mwanzo wa kuia biashara yako,nitakupa mfano : utengenezaji wa nembo/logo sio wa kujisikia na hamu unaenda kwa kufuata sheria zake kila soko ama kada inasheria za aina gani ya nembo ndio maana ukiona nembo unasema ile ni ya hospitali,kanisa,duka la dawa,nguo n,k hii ni kutokana na kufuata asili ama aina sahihi ya nembo na soko husika,lakini hapo hapo unaweza kukutana na nembo ikiwa na muonekano ama alama isiyokuwa ya kwake na ukaweza kugundua kama nembo hii imefana na nembo ya kitu kingine ambacho sio sawa na hiki,sasa basi unapotengeneza nembo ni lazima uzingatie rangi (zinamaana zake),aina,soko,trend na motto hivi ni vitu muhimu sana ambavyo unatakiwa kuvifuatilia unapofikiria kutengeneza nembo usipovifuatilia inamaanisha nembo yako haitaendana na soko lako,sasa basi iwapo utaenda kufanya kazi na mtengeneza nembo ambae hana weledi wa kutosha asipofuatilia vitu hivyi inamaanisha anakuwa tayari ameshakuweka kwenye hatari ya kutokufanikiwa kwa biashara yako na asilimia kubwa huwa hawana bei sababu kazi zao na malengo yao ni kufanya kazi nyingi ili wapate vingi waendelee ambapo shida huja kutokea baadae sana ambapo nembo imeshaingia sokoni inapoenda kwenye ushindani haina muonekano wa kutosha kuleta ushindani matokeo yake ni kufeli ama kutumia nguvu na gharama kubwa ili kufanya watu waizoee tofauti na ile ambayo inaendana na soko lako.

Hivyo unapofikiria kutengeneza muonekano wako unatakiwa kuwa makini sana na eneo hili,mteja anakutana kwanza na muonekano wako kabla ya bidhaa,inamaana ukikosea jinsi ya kuonekana hautampata kirahisi na kumbuka biashara ni ushindani ambapo ukienda kwenye ushindani kwa kutumia nguvu ya bidhaa wenzako wakiwa na nguvu ya muonekano ( nitakuja kufundisha hili aina za ushindani na washindani) utahitaji nguvu ya ziada kubwa sana ambayo inaweza kukufanya ufeli sababu ya gharama ni kubwa,aliekufelisha ni mtu wa mwanzo bila kujua sababu ulifanya ama mlifanya muonekano wa kuwapendeza ama kukupendezea wewe biashara ni kuhusu wateja sio wewe chochote unachokifanya kiwe kinahusu mteja,ukijifurahisha tu unakuwa umejitoa kwa wateja wako usikimbilie gharama kidogo ili uwe na kitu,kinaweza kukugharimu gharama kubwa zaidi pale ambapo unakitumia.madhara ya kutokuwa na muonekano sadifu ni makubwa kuliko gharama ya kutengeneza muonekano stahiki na watu wenye weledi na uelewa wa kutosha,biashara ni uwanja wa makosa,kosa lako leo ni mbinu ya mshindani wako ya kesho.

Tumia washauri wa masuala yabiashara na uchumi kupanga na kutambua ni kitu gani na aina gani ya muonekano utakao sadifu biashara yako,ili hata wewe uwe na wazo kamili la aina gani ya soko na muonekano unauhitaji,lakini pia tumia watengeneza muonekano wenye weledi kwa kuwatambua utendaji kazi wao wa kazi mwenye kuijua kazi yake lazima atakupitia kwenye hatua zote za kutengeneza muonekano stahiki lakini kwa yule mwenye kujali kiasi atakutengenezea kwa kufuata ulichosema bila kuchuja wala kushauri,ni suala la msingi sana kutambua ni wapi unatakiwa kufanya na muonekano bora usisimamiwe na watu wengi chagua sehemu moja tengenezea hapo hapo ukisambaza mikono ya watengenezaji utakosa ule utofauti wa mwanzo kwenye muonekano wako.

tumia washauri na watengeneza muonekano(image,brand) wenye weledi na kazi zao,madhara yake ni makubwa baada ya kutokea na hautayaona moja kwa moja kama yameletwa na hatua ya kwanza ya utengenezaji wa biashara ama brand yako.

Elisha Chuma
Mshauri wa Branding,Biashara na Ujasilimali
0765912609

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango