Elisha Chuma : Maana ya mawasiliano


Watu wengi wanapowasiliana mawazo yao ama fikra zao huwapeleka kwenye kujibu kabla ya kuelewa kwanza na ndipo hujitokeza ile dhana uanongea na mtu unahisi anakuelewa halafu baada ya muda ndio anakufata anakwambia "kwa hiyo kumbe pale ulimaanish hivi" hii ni dalili moja wapo kwamba  mtu huyu hakukusikiliza ili akuelewe ila akujibu kwanza,mimi na wewe ni mashahidi wa vitendo hivi mara nyingi na kulingana na mazingira tumejikuta tumesahau kurekebisha tabia hii ambayo imekuwa na madhara makubwa kwa watu wengi.

Kwenye usaili sasa hivi kampuni nyingi zinatumia mbinu ya kupima uwezo wa mtu kuelewa kama kigezo moja wapo cha kumuajiri  mtu,maswali utakayoulizwa asilimia kubwa ni ya kukupima kiwango chako cha uelewa hii yote ili kuhakikisha ni mtu sahihi nje ya weledi alionao,unaweza kuwa na ujuzi ama uwezo mkubwa wa kufanya kazi ila kama hautakuwa mtu wa kuwasiliana kwa kuelewa inamaanisha ile dhana ya "team work" inakuwa inapotea sababu hautaweza kufanya kazi vizuri na wenzako sababu ya mawasiliano mabovu.

hata kwenye mahusiano pia kufanya mawasiliano kwa kujibu badala ya kuelewa ni tatizo kubwa, mahusiano mengi yanaharibika sababu ya mawasiliano mabovu ambayo hupelekea uaminifu kushuka na mwisho ni hisia kupotea kabisa, lakini asilimia kubwa inakuwa imesababishwa na mawasiliano mabovu.mfano: mko kwenye mahusiano huangalii kwanini mwenzako kakutumia sms ama kakupigia simu,kwenye mahusiano mawasiliano yanakuwa yamebeba ndani yake hisia,mapenzi,ahadi ,mipango na vitu kadha wa kadha,hivyo inapotokea ( hasa mwanamke) anapoanzisha mawasiliano tambua sio maneno unayoyasikia ama vitu unavyoviona ndani yake vina maana kubwa ,sasa utakuta mtu katumiwa sms saa 4 na imeonyesha imefika inakuja kujibiwa saa 9 napo majibu yanakuja makavu hayana bashasha wala hisia ndani yake,kwa mtumaji tayari ni doa kwa mawasiliano yenu ,zile hisia za kutuma sms zinakuwa zimeumizwa na muitikio wake,lakini huenda mtumiwaji kweli alikuwa amebanwa kipindi sms inafika lakini jibu lako ndio linanafasi ya kuziponya ama kuziumiza zaidi hisia zake, hivyo mawasiliano kwa kuelewa ni jambo la msingi sana kwenye maisha yako, kumbuka unapowasiliana sehemu yoyote ile kumbuka kuwasiliana kwa kuelewa sio kujibu na mawasiliano sio kuongea na sms tu,mwili wako unatoa mawasiliano ndio maana kuna lugha ya mwili na lugha za alama pia.


Ukiwasiliana kwa kujibu unaondoa mambo mengi mazuri ambayo yanakuwa yamefichwa ndani ya mawasiliano kabla ya kufika mwisho, hata wewe ni shahidi mapokeo ya mawasiliano yameshakufikisha mahala ukaahirisha kufanya ama kusema ulilohitaji kusema,na hii imetengeneza mazoea hadi kwenye salamu kuna muda tunahisi ni kawaida lakini matokeo yake sio mazuri, mfano  unaenda kumtembelea mgonjwa ukimsalimia "habari yako" wengi na asilimia kubwa atajibu "nzuri" ambapo kiuhalisia unamuona hali yake sio nzuri, "umeamkaje" atajibu "salama ila hatujalala leo" hii yote imetengenezwa na mazoea ya kuwasiliana kwa kujibu ila sio kwa kuelewa.

Anza kufanyia kazi mfumo wako wa mawasiliano leo,unapowasiliana na mtu usifanye kwa kujibu ila wasiliana nae kwa kumuelewa jiulize baadhi ya maswali kabla ya kujibu,kwanini kasema hivi,yuko kwenye wakati gani?,tuko wapi?, anataka kufahamu nini kupitia anachouliza/wasiliana,nina ufahamu kiasi gani kuhusu hili ndio unaweza sasa kumjibu mtu utaona vitu vingi vinaanzia hapo hata hekima na heshima inajengwa nna jinsi unavyowasiliana.

hata kwenye biashara matamshi yako na majibu yako ndio yanakupa biashara  ama yanaua biashara yako,lakini pia kwenye mahusiano jinsi unavyowasiliana ni aidha unajenga ama unabomoa ,kwenye kazi vivyo hivyo,kwenye maisha tunawasiliana na kila anaetuhusu na kuelewa ni jambo la msingi sana kutambua tofauti na kuanza kufanya kwa usahihi wake

Kuwasiliana ni kuelewana sio kujibizana.

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango