Elisha Chuma : Kujiamini

Je wewe unajiamini,unatambua faida  za kujiamini na hasara za kutokujiamini hebu pitia somo hili ujione uko sehemu gani.


Kujiamini naweza kusema ni uwezo wa kuwa na uthubutu juu ya mambo pasipo kuwa na hofu wala uoga bila kutegemea msukumo kutoka nje.

Kujiamini sio kitu cha kufanyiwa na mtu mwingine ila ni maamuzi binafsi ambayo yana hatua zake ukitaka kuyafikia ili ufikie hatua ya kujiamini vitu vinavyochangia ama vinavyoweka chachu na hamasa ya wewe kujiamini ni pamoja na 
   1. Kujitambua
   2. Maamuzi binafsi
   3. Imani yako
   4. Uelewa
   5. Makuzi na
  6. Mazingira 
Hivyo ndio vitu ambavyo unapofikiria kujiamini vinakupa chachu na hamasa wewe kufanya jambo bila msukumo wa nje bali msukumo wa ndani yako mwenyewe.

Vitu vinavyoweza kukusaidia kujiamini katika maisha yako.
1. Jifunze kujithamini ( usijione huna thamani hata siku moja)
2. Jisamehe na kuwa mkweli kwa nafsi yako mwenyewe
3. Jilinde na pambana na hofu yako (Kisaikolojia)
4. Fanya vitu unavyoviogopa ( visivyo na madhara ya muda mrefu)
5. Kubali kushindwa na kujifunza
6. Jisimamie (kimawazo,kiimani na kimatendo bila ujeuri)
7. Jipongeze
8. Jifunze kushughulika na  hisia zako (furaha,huzuni,hasira...n.k)

Ukiwa na dalili hizi tambua kiwango chako cha kujiamini kiko chini
1. Kugusika kirahisi kihisia
2. kuwategemea watu wengine kuthibitisha
3. kujilinganisha  katika kufanya mambo au thamani
4. Kujishusha ama kujipandisha thamani kuliko wengine
5. Kuwafurahisha wengine kwa gharama/hasara zako 
6. Kukimbia majukumu na kutupa lawama
7. kutumia nguvu nyingi kuilinda hadhi ya uongo
8. Kuogopa sana kukosolewa  na kupenda kukosoa
9. Aibu za ziada kushindwa kutazama watu usoni
10. kutawaliwa na majuto ya jana na hofu za kesho

Hasara za kutokujiamini
1. kukosa usalama kuhusu wewe na kukosa imani dhidi yako mwenyewe (Hujiamini)
2. Kushindwa kuwa wazi na kushindwa kuwaamini wengine
3. Kushindwa kufanya maamuzi 
4. Kukosa amani na utulivu (wasiwasi)
5. Ugumu wa mahusiano na wengine
6. Kushindwa kudhibiti mihemko na hisia
7. Kuogopa kukataliwa na kutojaliwa hivyo unakuwa mtumwa wa mtu/watu
8. Kutokuwa na kiasi cha ya ndani
9. Kujifungia kwenye tabia kwa njia ya usugu (pombe etc...)
10. kuwa na wivu mkali muda wote
11. Kuikosa furaha na kuhisi kutojitosha
12. Kukimbia uhalisia  ili kukandamiza
13. Maisha ya kufake huku unahitaji msaada
14. Kushuka utendaji kazi kazini

Katika maisha unatakiwa kujiamini kwa kila hali,ili ufanikishe malengo yako ni lazima ujiamini,ndoto nyingi zimefeli sababu ya kutokujiamini na malengo mengi hayafikiwi sababu ya kutokujiamini unavitu vingi mkononi mwako lakini hujiamini navyo unafursa nyingi mbele yako huzioni sababu hujiamini,unawazo bora ndani yako hulifanyi sababu hujiamini. Badilisha mtazamo wako anza kuwaza chanya na chanya itakujia.

Hili pia lianzie kwa wazazi mfundishe mwanao kujiamini tangu akiwa mdogo ili makuzi yake yampe uthubutu mapema usimfanye awe ni wa kuogopa na kukuogopa kila siku saikolojia yake unaiharibu kwa maisha ya baadae,samaki tumkunje angali mbichi mtoto wa leo ni kijana wa kesho bila kumpa msingi imara hataweza kuwa na uthubutu kwa yeye mwenyewe lakini pia hata kwa vitu vinavyomzunguka.

Jiamini maisha ni wewe na wewe ni maisha changamoto ni ukuaji zipokee zikubali jifunze,jiamini ulipoanguka hujafa amka unaweza kutembea tena na tena.

Elisha Chuma
Mwalimu/Mshauri 
+255 745 108010
www.elishachuma.blogspot.com

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango