Matumizi sahihi ya elimu yako.

Kwanza kabisa ni jambo la msingi kutambua na kuiondoa dhana ya kuwa mjinga ni tusi,ama kushushwa hadhi HAPANA.

Mjinga ni mtu asiekuwa na uelewa wa kitu ama jambo fulani,hivyo ifike mahala izoeleke tu kuwa wewe ni mjinga wa kitu fulani  na isiwe ni tusi ama udharirishaji kwako.

Lakini dhima ya bandiko hili iko kwenye muktadha wa matumizi ya elimu zetu kwa manufaa ya baadae,tumepita kwenye kipindi ambacho dhana kuu ya elimu ilikuwa ni kusema umesoma chuo ama sehemu fulani na uko na vyeti vingi,kipindi hiki kimetuathiri kwa kiasi fulani kwani kimetengeneza wahitimu wengi wenye vyeti lakini hawana uwezo sokoni.

Lilipokuwa tatizo tena wakaanza kulalamika wazee wameshikilia nafasi za ajira zao hivyo hawawezi kuajiriwa, lakini swali ambalo hawakujiuliza ni kwanini hadi leo bado hawana kazi lakini wana elimu, na Je ni kweli kuwa bila kuajiriwa elimu yako haina kazi?.

Watu wengi tunajisahau sana na kuacha kutumia elimu ila tunakimbilia makaratasi,mabadiliko ya kipato yanaanza na mbadiliko ya ndani mwili,akili na uthubutu unatengenezewa ndani kwanza.

Jambo la msingi zaidi kutambua akili sio kitu cha kutengenezwa kila mtu anazaliwa akiwa nazo pamoja na utambuzi, unapoenda shule ni kwenda kuongeza eulewa juu ya kile unachotamani kukifanya kuondoa tatizo kiwe msaada kwa wengine na ww upokee shukrani ya kujikimu na kuishi vyema, hivyo dhana ya elimu sio makaratasi ni uelewa unaotakiwa kuungana na ufahamu ulionao tayari pamoja na maarifa ili utatue tatizo,badilisha mawazo leo tumia elimu yako sio makaratasi.

Kwa huduma ya ushauri , machapisho na vitangu vyangu.

0745108010



Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango