JENGA MAZOEA YA KUANDIKA MAWAZO YAKO.


Akili zetu zimeumbwa kuwa na maboresho ya mawazo kulingana na msimu ama uhitaji husika, hii imekuwa ni changamoto kwa watu wengi sana wanapofikiria kuanzisha ama kukamilisha malengo yao, wanapoanza wazo linakuwa jingine na wanapoendelea pia wazo linakuwa jingine hii inapelekea kupoteza nguvu katika kusimamia misingi ya wazo la kwanza.

Sasa basi jitahidi sana uwe unaandika mawazo yako ili unapoyafanyia kazi uwe na sehemu ya kumbukumbu ambayo utaitumia kwa ajili ya kukuongoza katika yale ambayo unafikiria kuyafanya, kuandika inaweza kuonekana kama ni kitu kidogo sana katika utendaji lakini ni kitu kikubwa sana kisaikolojia na pia hata kimalengo.

Nijulishe hapa chini, na wewe ni mtu wa kuandika malengo yako au unakiamini kichwa chako kwamba siku zote utakumbuka na kulisimamia lengo mama.

Bado kitabu cha Saikolojia ya mahusiano kinapatikana, ni kitabu maalum kwa ajili ya kuinua na kurudisha uelewa bora wa mahusiano kuanzia yale ya mzazi na mtoto hadi yale ya kimapenzi, saikolojia yake isipotambulika tunafeli sehemu kubwa ndio maana sasa hivi mahusiano yamekuwa ya kikatili sana kwa pande zote, tujifunze ili tuweze kuokoa kizazi chetu lakini pia na msingi bora wa kizazi cha baadae.

Kitabu kinapatikana katika nakala aina 3 ( nakala ngumu, nakala ya sauti na nakala digitali) unaweza kuagiza ama kuwasiliana nami nachi kitakufikia kwa uhakika kabisa
0745108010.

#echumaarifa #timizamalengo #maarifabora #UJASILIAMALI #biashara #elishachuma #maishanihayahaya #wakubadilikaniwewe






 

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango