Hatua za kufuata unapofikiria kuanza ujasiriamali
Ujasiriamali sio
kitu kidogo kama wengi wanavyofikiria na wengi hufikiria kupokea hasara ni kama
vile umefungua duka hujauza vitu hadi muda wake wa kutumika umeisha ndio unakuwa umepata hasara lakini kwa maana
ya ujasiriamali maana iko tofauti kidogo maana ya kukubali hasara kwa upande wa
ujasiriamali ni ile hali ya kukubali kutumia nguvu na gharama nyingi kwa ajili
ya matokeo ya baadae ,ambapo matokeo hayo yanaweza kuchukua muda mrefu hadi
yaonekane. Mjasiriamali ni mfanyabiashara pia na hakuna mfanyabiashara
anaefanya biashara kwa hasara kila kinachofanyika katika biashara kinategemewa
kulipa hata kama sio sasa, hivyo hata mjasiriamali pia hakubali hasara ila kwa
malengo.
Hivyo unapoamua kuwa
mjasiriamali usikurupuke kwa vile unajiona unaweza kwanza kabla ya yote
jitambue kwanza (tofauti kati ya
ujasiriamali na biashara),ukishakuwa na uhakika na hilo sasa unaweza kuanza kufata hatua
zifuatazo,nb: usifanye kwa kuwa unataka kujilazimisha kuwa mjasiriamali fanya
kwa kufuata origin yako.
- Kutambua investment unayoiweka
Unapokuwa
mjasiriamali ni sawa unakuwa
unatengeneza mpango wa kifo chako au maisha yako ,ujasiriamali au unachokifanya
kwa ujasiriamali kinatakiwe kiwe ndani yako,kiwe kinaongoza maisha yako,hivyo
unatakiwa utambue kwamba unachotengeneza kwa muda huo ni maisha yako ni kifo
chako na ni inestment yako pia.
- Baada ya kutambua hilo unatakiwa uyaone mafanikio ya investment kwa kipindi cha muda mrefu usitengeneze mafanikio ya muda mfupi,ujasiriamali wako unatakiwa usikuonyeshe chochote kila ukijaribu kupata picha ya muda mfupi ila ukipiga picha ya muda mrefu unayaona mafanikio hiyo ndiyo aina ya ujasiriamali unayotakiwa kuwa nayo.
- Ili kukamailisha mipango ya ujasiriamali wako tengeneza vyanzo shirikishi vya biashara ambavyo vitakuwa na kazi ya kukusaidia kuyafikia malengo makubwa ya ujasiriamali wako. vyanzo hivyo vifanyie utaratibu kama uliotangulia kwenye uzi wa.
http://elishachuma.blogspot.com/2013/11/hatua-za-kufuata-unapofikiria-kuanza.html
Comments
Post a Comment