Jinsi ya kutengeneza mpango biashara ( Business plan)
Katika dunia ya sasa
utengenezaji wa mpango wa biashara
umekuwa ni lazima na kwa biashara yoyote unayoifanya bila kuitengenezea mipango
haiwezi kufanikiwa, leo nimeamua kuanza na baadhi ya mambo ambayo unatakiwa kuyafahamu
unapotaka kutengeneza mpango wa biashara .
Hapa chini
vifuatavyo ni vitu muhimu unavyotakiwa kuvizingatia katika utengenezaji wa
mpango biashara wako, andika kwa umakini kiini cha wazo lako la biashara na
lijumuishe vitu kama.
1/ Jina
2/ Aina ya biashara
3/ Historia ya
biashara na maendeleo yake
4/ Huduma /bidhaa
5/ Tathmini
ya Soko
6/ Ushindani
7/ Masoko
8./Ufanyaji kazi
9/ Usimamizi na
utawala
10/ Uwezo wa
wafanyakazi
11/Matatizo na
utatuzi
12/ Maelezo ya
kifedha
Jina na aina ya biashara
Kipengele cha kwanza
na cha pili ni kama vinashabihiana kwanza ni inatakiwa uandike jina la biashara
unayotegemea kufanya ( hapa sio aina ya biashara) ni jina linalokutambulisha
wewe katika biashara , Pia hapa napo kuna tatizo majina ya biashara pia ni ishu
haitakiwi kujichagulia tu ilimradi jina lako unaitwa Musa basi jina la biashara
litakuwa Musa Genereal Enterprises uchaguzi wa jina la biashara nao unanafasi
yake katika kuvuta wateja kwenye biashara yako. Ukimaliza hapo unaainisha sasa na aina ya biashara unayofanya je? Ni
kutoa huduma au bidhaa kwa maelezo ya kujitosheleza.
Historia ya Biashara na maendeleo yake.
Sababu ya kuelezea
hii ni kuangalia utungaji na nafasi yako katika soko pia maendeleo ya hiyo
biashara, hapa unatakiwa utoe maelezo ya Taarifa za kuanzisha,uzoefu na uwezo
wa mmiliki, Eneo, Matatizo na utatuzi wa matatizo yanayoendelea, uwekezaji
wake, Mipango na Malengo ya baadae,
Taarifa na muonekano wa soko, Washindani wakubwa na faida ya Bidhaa /huduma yako.
Huduma au bidhaa
Unatakiwa kueleza au
kutoa maana ya bidhaa au huduma ambazo zinavutia kwa biashara yako.kwa
kuzingatia maelezo ya utofauti wako,uwiano wa soko,Hatua ya uboreshaji wa
huduma/bidhaa, uzalishaji, vitendea kazi( wafanyakazi na rasilimali ), fedha
inayohitajika, Mzunguko wa uhai wa huduma/biashara na ukuaji wa baade.
Tathmini ya Soko.
Kuangalia bidhaa/
huduma na uhusiano wake na mtumiaji, vitu unavyotakiwa kuvielezea ni
Soko unalolikusudia, watumiaji wake tabia zao,vitu vinavyotakiwa kwa
huduma /bidhaa yako, majibu ya mtumiaji baada ya kutumia,sababu za kimasoko na
msimamo wake, upenyo katika soko, Kuchangia soko,utafiti na kusoma,gharama na
mpango wa mauzo.
Ushindani
Unatakiwa uanishe na
kuelezea washindani wako na wewe mwenyewe ili mbinu zako ziwe imara baadi ya
maelezo unayotakiwa uyatoe kwenye mpango biashara wako ni pamoja na Kujua
washindani wako,taarifa za washindani, uwiano wa bidhaa /huduma, uwezo na
udhaifu wa bidhaa /huduma, maendeleo ya baadae ya huduma/bidhaa na
kinachohitajika sokoni.
Comments
Post a Comment