Jinsi ya kuanzisha biashara bila ya kuwa na mtaji wa pesa.
Imekuwa ni kawaida
kwa watu wengi kutambua pesa kama mtaji wa kila kitu katika biashara , lakini
katika ulimwengu wa biashara iko tofauti pesa sio mtaji bali pesa ni kiasidizi
cha mtaji . Leo nitakupa baadhi ya njia unazoweza kutumia kuanzisha biashara yako
bila ya kuwa na mtaji pesa ila kwa kutumia mtaji mbinu na vinginevyo.
Watu wengi huruka sana sehemu ya kwanza ya mtaji ambayo
ndio chimbuko la mtaji na kukimbilia kwenye sehemu zinazofuata na kuendelea bila kujua
muhimili wa nyumba ni msingi bila ya msingi mzuri nyumba inaanguka hivyo bila
chimbuko zuri la mtaji wako hauwezi kufanikiwa, sasa basi chimbuko hilo ni nini
ambalo watu huliruka na kukimbilia mengine.
Kichwa/ akili mtaji
wako mkubwa ni kichwa chako na hata wazo na kila kitu kinaratibiwa na kichwa
chako mwenyewe ndani ya kichwa ndipo panatengeneza ndoto na ndipo panapofanya
ndoto zitimie kwa kushirikiana na viungo vingine vya mwili lakini injini ya mwanadamu
ni kichwa katika kufanya mambo ya maamuzi. Kichwa ndio chimbuko la mtaji wako
na kila mwanadamu amebarikiwa kupewa kipaji au uwezo wa kufanya kitu fulani
ambacho anaweza kufanya bila kufundishwa na mtu, na kupitia hicho kipaji au
uwezo unaweza kufanikiwa sana tatizo ni wengi hupuuzia vipaji na uwezo wao
binafsi na kuabudu uwezo wa wengine na wengine huona kama vile uwezo wao
hautoshi au haujafikia uwezo wa kuanzisha kitu cha kumsaidia.Kipaji chako
haufundishwi unazaliwa nacho kuna vipaji ambavyo ni vya wote na kila mtu
anakuwa nacho ila asilimia kubwa huwa tunahisi ni lazima uwe hivyo. Huwezi
kwenda kutafuta kipaji chako shuleni unaenda shule kuendeleleza kipaji chako.
(Mfano wa kipaji cha wote ni kula, kila mtu anapozaliwa huwa anakipaji cha kuchukua
mkono kupeleka mdomoni hakuna anaefundishwa hilo ila unaweza kwenda shule
kusomea namna ya kula vizuri,kistaarabu na vitu kama hivyo lakini sio kwenda
kufundishwa namna ya kula.) nisikutoe sana kwenye mada jitambue unakipaji
ambacho kinaweza kuwa mtaji tosha iwapo utakionyesha na watu wakakiona.
Kitu cha muhimu
ambacho unatakiwa ukifahamu kwanza ujitambue ili uweze kufuata njia yako na
katika lugha za kibiashara kuna kujitambua kwa aina mbili aidha ni mfanyabiasha
au mjasiriamali hapoa sasa unatakiwa kujua wewe ni nani na kati ya hivyo viwili
unaweza kuegemea sehemu ipi na ukapambana na changamoto zake ukiwa unafurahi
kuna msemo fulani husema " Watu masikini huomba matatizo yasiwakute ilhali
matajiri huomba matatizo yawakute " hapo wengi mtaanza kujiuliza ni kwa
njia gani unaweza kuomba hivyo masikini huchukulia matatizo kama shida hivyo
hujitahidi kuyakimbia ili yasimharibie mipango yake ya sasa lakini tajiri
huomba matatizo yaje ambapo yeye huona matatizo ni sawa na changamoto hivyo
huomba changamoto zimfike ili ajifunze hata itakapokuja kumtokea tena atakuwa
anauzoefu tofauti na mwanzo lilipotokea.hivyo ukijitambua wewe ni nani utapita
katika changamoto zake huku ukiona njia nyingi za kutokea ni wewe mwenyewe
utumie ipi ambapo ni tofauti iwapo umechagua sehemu ambayo sio hapo ili
ufanikiwe itakubidi umtafute mtu ambae yeye ndio sehemu yake ili akupe njia na
mbinu za kutokea hapo uwezo wako utakuwa umefunikwa na kumuelekea yule
anaekusaidia.
Ona kipaji chako
kinaruhusu ufanye nini na tumia kipaji chako kama mtaji wa kukuanzishia
biashara yako au ujasiriamali wako ambao ndio kipaji chako kitu cha msingi ni
kutambua unahitaji watu gani na unawafikia vipi tumia kichwa chako vizuri na
akili zako asilimia kubwa ya waliofanikiwa sana au wenye maendeleo makubwa
walitumia vipaji vyao kwa umakini ndio wakatengeneza ajira kwa wengine.
itaendelea toleo lijalo......
Comments
Post a Comment