Jinsi ya kuanzisha biashara bila ya kuwa na mtaji wa pesa. (Sehemu ya pili)
Baada ya kuangalia sehemu ya kwanza wiki iliyopita ya jinsi ya kujiajiri bila kuwa na mtaji pesa leo tunaendelea na sehemu ya pili.
Kama imetokea
umeshindwa kugundua kipaji chako bado kuna uwezekano wa kuanzisha biashara yako
bila ya kuwa na mtaji pesa haya kitu cha kwanza ni unatakiwa ujitambue wewe ni
nani kati ya mfanyabiashara au mjasiriamali halafu ona aina ya biashara ambayo
ndani ya uasili wako mwenyewe ichague
kwa umakini halafu andika chini vitu ambavyo unavihitaji ili biashara yako
ifanikiwe au ionekane andika pembeni ( Sio mpango biashara)halafu anza kufanya utafiti wa hivyo vituulivoandika
kwa kutafutia mbadala wake sehemu zote ambazo zinahitaji pesa ziorodheshe
pembeni halafu anza kutafuta mbinu mbadala kwa kila kimoja usikurupuke chukua
muda ili ufanye maamuzi mazuri kama ulichochagua kikondani ya sehemu yako ya kujitambua kupata njia mbadala sio
kazi ngumu.( Safari ya mafanikio huanzia mbali sana hakuna tajiri ambae alianza
huku akiwa tajiri au alianza na mtaji mkubwa )anza kufanya na kushughulikia
biashara yako kwa ngazi yako usilazimishe ianzie juu. Kama ulichochagua kweli
kiko kwenye damu yako kufeli ni kugumu
mfano: Asili ya kabila la wachaga ni biashara hivyo kwa mchaga kuwa
mfanyabiashara ni kitu rahisi kuliko msukuma, Mmasai asili yake ni ufugaji (
Mjasiriamali) hivyo kwa huyu kufanya ujasiriamali ni kitu ambacho kiko ndani ya
damu yake hivyo ni rahisi kupata mbadala wa changamoto.
Baada ya kupata
mbadala wa kila sehemu ya fedha anzisha biashara yako kwa kutumia mibadala hiyo
ambayo itakusaidia wewe kukamilisha malengo yako bila ya kugusa pesa yako.
Katika biashara kuna mafanikio aina mbili , yanayoonekana na yasiyoonekana watu wengi huangalia mafaniko yanayoonekana
tofauti na yasiyoonekana mafanikio yasiyoonekana ndio mafanikio ya kweli kwani
mafanikio ya kuonekana ni matokeo ya mafanikio yasiyoonekana. Na mara nyingi
unapoanza biashara yako mafanikio yasiyoonekana ndio mengi kuliko mafanikio
yanayoonekana watu wengi huishia hapa pia sababu tu yeye anataka mafanikio
yakuonekana au watu alionao wanahitaji mafanikio hayo basi anaamua kuachana na
hiyo biashara kwa kuona haina matokeo chanya japo yapo hayo matokeo chanya
katika maisha yake mwenyewe. Kama unachokifanya unakifanya kwa moyo mmoja
mafanikio yake utayaona kwanza wewe ndio wengine watakuja kuyaona lakini wewe kwanza. Pia tatizo kubwa wengi
wanahitaji kuwa mabilionea ndani ya miaka au muda mchache . Asilimia kubwa ya
matajiri ni wajasiriamali ambao waliwekeza katika biashara, biashara ya
ujasiriamali ikikubalika sokoni mafanikio yake ni makubwa .
Usiwe na papara ya
mafanikio wakati hauna hata mtaji angalia vitu gani unavyoweza vifanya kwa
hatua na uwezo wako kwanza acha kufikiria kama waliofanikiwa wakati hata
haujafanikiwa bado.chini hapa ni mfano wa mtu mwenye asili ya ufugaji.
Anavyoweza kufanya ufugaji bila ya kutumia pesa ila akili na uwezo.
Mfano: Umejiangalia
ukagundua ujasiriamali wako ni kufuga kuku, hauna pesa ya banda wala ya
kuhudumia hao kuku achilia mbali kuwanunua
kuku wenyewe , kitu cha kufanya kama nilivyosema hapo juu andika vitu
vinavyohitaji pesa
- Banda 2. Matunzo 3. Kuwanunua kuku wenyewe n.k, ondoka nenda sehemu ambapo wanafuga kuku tengeneza
Tengeneza mazoea na
mwenye banda, ongea nae kuhusu mpango wako wa kuwa mfugaji pia na mwambie
tatizo lako ni mtaji lakini unataka uingie nae makubaliano halafu atakusaidia.
Mwambie utamletea au utamuuzia aidha kuku au mayai trei au kiasi fulani cha
kuku na ukifikisha wateja kiasi fulani atakupatia kuku na jogoo mmoja , nenda
katafute soko na uza kama mlivyokubaliana na ukishafikisha utapewa hapo tayari
mtakuwa mmeshazoeana utamuomba waendelee kukaa hapo kwake hadi
utakapowatengenezea banda, akikubali subiri hadi kuku atakapototoa chukua yale
mayai baadhi yaache mengine toa kwa kuuza kwa vile tayari unawateja unaweza
kupeleka na kuuza ukapata kiasi fulani cha pesa hicho kiasi kitunze kama ni
kidogo na anza kutengeneza banda dogo la muda subiri kuku wako atotoe tena
fanya vivyo hivyo hadi utakaporidhika unaweza kuwahamisha watoe wapeleke kwenye
banda lako na sasa utakuwa tayari unasoko na sehemu ya kuwatunzia matunzo yake
pia yatatoka katika mayai na utakao amua kuwauza.
UKIWA UNAFANYA KITU
KWA MOYO WOTE HUWEZI KUKOSA MBADALA WA CHANGAMOTO.
Fanyia kazi utambuzi
wako na biashara ya moyo wako.UTAFANIKIWA tatizo kubwa kwa sasa ni uwezo wa
kutambua ipi ndio njia sahihi ya moyo wako sababu wengi wanatamani vingi .
Comments
Post a Comment