Kwanini wajasiriamali wengi wanafeli?
Kumekuwa na watu
wengi ambao wamekuwa wanahitaji kuwa
wajasiriamali lakini asilimia kubwa wanakuwa ni wale ambao wanakuwa wamefeli
mipango mikubwa au kuna kitu kimewasukuma ,vitu ambavyo unatakiwa usifanye kwa
kudhani unatengeneza maisha utakuwa unapotea.
- Kuna kundi ambalo wao huanza ujasiriamali baada ya kuona umri unaenda au wanategemewa sasa na aidha famili a au kadahali Usifanye ujasiriamali kwa kuona umri umeenda upate kitu cha kujishikiza, hapo utafeli kumekuwa na watu wengi ambao hadi astaafu ndio anaanza ujasiriamali au baada ya kuona umri umeenda ndio anatafuta kitu cha kumpatia ujasiriamali hii ni mbaya na kufanikiwa kwake ni kugumu sana, ujasiriamali sio nyongeza ya ulichonacho ujasiriramali ni msingi wa ulichonacho kama hukutengeneza msingi mwanzo ujue hata uweke ukuta imara kiasi gani dhoruba ikija ni lazima nyumba itapata mtikisiko.
- Wapo wengine ambao wanafanya ujasiriamali baada ya kukosa au kutuma sana maombi ya kazi ukifanya ujasiriamali wa aina hiyo utakuwa unakosea pia ujasiriamali sio njia mbadala wa kazi yako na tatizo kubwa linakuja kujitokeza mtu anapotaka matokeo ya ujasiriamali yawe sawa na ya kazi aliokuwa amepanga kuifanya .
- Asilimia kubwa ya wanaofeli ni wale ambao hata elimu ya kujitambua mwenyewe hana, unaweza kuja kumpa wazo la biashara leo kesho yeye akaanza nalo hata bila kuangalia kwa undani kama linaendana nayeye pia bila hata kulinganisha hiyo biashara na yeye wala kufanya utafiti matokeo yake mara nyingi ni kufeli.
Comments
Post a Comment