Ushauri wangu kwa serikali kuhusu ujasiriamali na upungufu wa kazi kwa vijana.

Nchi yetu inaongozwa na sheria na moja kati ya sheria za nchi hii ni kila mtu ana uhuru na haki ya kutoa maoni yake , hivyo na mimi nimeamua kutoa maoni yangu binafsi kuhusu hili suala la ujasiriamali hapa nchini , kwanza pongezi  kwa serikali kuona njia mbadala ya kupunguza wimbi la vijana wasio na ajira ni kufanya ujasiriamali , lakini nilikaa na kuangalia baadhi ya mambo nikagundua kuna mapungufu mengi na mara nyingi tumezoea kutaja matatizo ili uliemwambia atafute suruhisho. Hapo unakuwa unakosea kama yeye hakuliona tatizo unapompa tatizo tu bila suruhisho unampa kazi ya kufanya ambacho hakijui hebu fikiria nimekutengenezea gari lako na kukuletea mimi sio mtengenezaji wa kwanza inamaanisha ntarekebisha ili liwe kama awali wewe ndio unaetumia gari yako nikitengeneza isipofika unapohitaji ni lazima utaniambia bado ilikuwa anafanya hivi na hivi na hivi tofauti kabisa na huku kuna tatizo la maji kijijini watu wanaeleza tu tunashida ya maji tufikiriwe hata kidogo na sisi tunatembea umbali mrefu kuyapata . Je suruhisho lako ni nini kupitisha bomba,kutengeneza bwawa au kuchimba kisima nk. Tuyaache hayo tuendelee na hili la ujasiriamali

  1. Kwanza hakuna mfumo mzuri wa kumtengeneza mjasiriamali au mfanyabiashara ila kuna mfumo mzuri wa kumkata kodi, haujamfundisha kuitafuta kodi lakini unamkata kodi, wafanyabiashara wakubwa na makampuni makubwa wanamisamaha ya kodi lakini tofauti na kwa mlalahoi ambae anaingiza pesa ya kula tu kwa siku kwake kila kitu ni kodi. Hii sio nzuri inatakiwa utengenezwe mfumo wa (freemind) fikra huru tangia mtu akiwa mdogo ili kama fikra zake zimemuelekeza sehemu fulani basi aende akafanye kwa moyo mmoja sio mfumo wa sasa unaruhusiwa kuwa na fikra huru unapomaliza chuo au elimu ya kidato cha sita ni miaka mingapi mtu anapoteza akiwa amefungwa na  elimu ya kumpacheti peke yake.uwekwe utaratibu wa kuwafundisha watoto mashuleni kuhusu ujasiriamali na biashara ili mtoto anapokua huku anatambua na tena inabidi masomo hayo yatumie mifano hai ya wajasiriamali na wafanyabiashara wazawa ili kutoa motisha ya kusoma na mazingira rafiki ya chaguzi zake.

  1. Pia hakuna matabaka ya wajasiriamali muuza nyanya na mmiliki kampuni wote wanakuwa katika sehemu moja hiyo ni mbaya kwa sababu mawazo ya mwenye kampuni na muuza nyanya ni tofauti japo wanahitaji kukutana lakini sio kwa kukaa eneo moja unatakiwa uwekwe mfumo pia wa kuwatambua wajasiriamali na ngazi zao ili kuwafanya wakae katika ngazi sawa ili wapeane changamoto na mbinu kulingana na ngazi zao, pia hii italeta changamoto katika utendaji wa kazi alieko chini atahitaji kupanda juu hivyo ataongeza ufanisi wa kazi ili afike huko juu.

  1. Kwa kuwa sasa hivi tayari tumechelewa kuanzisha hiyo mifumo kwetu na kizazi cha wanetu basi kwa sasa tutengenze mipango biashara ambayo inakuwa inaonyesha faida na hasara za kila ujasiriamali unaofanyika hasa kwa wajasiriamali wadogo wengi wao wanashindwa na kufeli sababu ya kulichukulia soko kikawaida sana inakuwa kama vile anajiona yeye ndio wa kwanza kuleta bidhaa sokoni kumbe tayari kuna wengine lakini hii yote inakuja sababu ya kutamanishwa bila kuambiwa changamoto tunahitaji kuondokana na wimbi la vijana wasio na ajira lakini suruhu yake sio kujitengenezea mwenyewe ili uondoke kwenye hilo kundi usipo msaidia kijana mwenzako leo kesho atakuiibia lakini ukimsaidia kesho atakusifia.Wanaotengeneza fursa na kuziweka hadharani nafikiri ni vizuri zaid iwapo vitu kama jinsi ya kufanya,changamoto,faida na hata hasara zake ziwe zinaainishwa ili kusaidia kuokoa muda wa wengi.

  1. Ujasiriamali isiwe ni kitu cha kukurupuka na kila mtu anakuwa mjasiriamali kwa vile ndio inataka kuonekana uti wa mgongo wa aliefeli kuwe na sehemu maalum za kutoa elimu ya ujasiriamali ambapo kila anaetaka kuwa mjasiriamali basi anapitia hapo atapewa elimu ya ujasiriamali kabla ya kuwa mjasiriamali na pia atakuwa na cheti cha kumtambulisha kama yeye ni mjasiriamali.

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango