Kazi na Aina za Branding

Karibu katika muendelezo wa somo la Branding na leo nimekuletea kazi na 
aina za Branding katika maisha ya biashara zetu, watu wanafikiri Branding ni kitu kigeni katika ulimwengu wa biashara La Hasha! Branding sio kitu kigeni na kila mtu kila siku anafanya Branding.Hapa chini ni baadhi tu ya kazi za Branding katika biashara yako.

Branding ndio muongozo au chanzo cha mauzo yako, iwapo utajibrand vibaya mauzo yako yatakuwa mabaya na iwapo utajibrand vizuri mauzo yako yatakuwa mazuri,Kazi ya masoko ni kuipeleka Branding nje ya ofisi ambapo kama ahadi na muonekano ulioweka kwenye brand yako utakuwa mzuri na wenye kumvutia mteja basi huyo atakuwa mteja wako ila ikiwa tofauti na hapo utakuwa umemkosa mteja.

Kazi za Branding


Brand  hutambulisha muonekano ,ubora  wa kuaminika kwa watu, huku bidhaa za generic (kawaida)  hazijulikani  na haziaminiki ,hata hivyo brand ni ghali na inahitaji mipango ya muda mrefu

Brand hutofautisha bidhaa na hufanya bidhaa kutambulika mapema

Brand inaruhusu mtumiaji kutengeneza maamuzi na matumizi ya bidhaa

Brand hutengeneza thamani halisi kwenye macho ya washirika wa kibiashara na hupenyeza thamani ndani ya macho ya mtumiaji

Branding hutengeneza trademark ambayo huongeza thamani ya bidhaa. 

Aina za branding. 

 

  1. Brand kama bidhaa
Hufanya kazi ya ubora na thamani ya brand.

Katika mkusanyiko wa matangazo ya bidhaa nyingi, mtumiaji huhitaji kujua jinsi ya kuchagua bidhaa moja juu ya nyingine, hivyo kwa kulinganisha udhania wake pale anapoamua kufanya hivyo huwa hana muda mwingi wa kulinganisha ,huamua kuchagua bidhaa ambayo inakidhi haja zake kutokana na brand.

  1. Brand kama mfumo/kampuni
Hutengeneza muonekano chanya wa brand na huonyesha nyuma ya brand kuna mfumo

Uwezo wa ushawishi wa kampuni hufanya bidhaa kuongeza thamani

  1. Brand kama mtu
Hii hujishughulisha na uhusiano na wateja , hutengeneza kukutana kati ya mtu na brand

Ni ngumu kuongeza soko kama hakuna mahusiano mazuri na wateja wako.

  1. Brand kama alama
Hutoa muendelezo wa utambulisho wa brand

Brand inayochukua akili yako hupata tabia , na brand inayochukua moyo wako hupata kujiapiza kwanzo.


Karibu katika Semina ya Branding online sehemu ya pili itakayofanyika kupitia mtandao wa Whatsapp kuanzia tarehe 1/05/2015. Jiandikishe kwa kutuma Namba na jina lako kwenda simu namba 0684 047323.ili ujiandikishe sasa. Elimu ya Branding ni ufunguo wa mafanikio ya biashara yako.

Kwa huduma ya ushauri na kufanya Branding ya biashara yako piga namba 0684047323 na utapata maelezo zaidi. ASANTE

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango