Kwanini usiache kuendelea kujitangaza na kutafuta masoko hata kama biashara yako inafanikiwa.

Nimekuwa nikiulizwa hili swali mara nyingi sana kuhusu mafanikio ya biashara na muendelezo wa matangazo, na asilimia kubwa ya wanaouliza swali hili ni wale ambao biashara zao zimefanikiwa au malengo waliyokuwa wameyaweka yamefikia au yamekaribia sana. Mara zote jibu langu huwa ni moja tu. Msingi wa biashara yako uko kwenye kujitangaza hivyo ukisimama kujitangaza basi na biashara itasimama kuingiza mauzo.

Leo nimeona niweke hapa chini baadhi ya sababu ambazo zinakufanya kama mfanyabiashara au mjasiriamali usiache kuendelea kujitangaza.

1. Ushindani haukomi
katika ulimwengu wa biashara mafanikio au kushindwa kunaletwa na ushindani,biashara isiyokuwa na ushindani haiwezi kujijua kama inashinda au inafeli sababu hakutakuwa na mwingine wa kuikumbusha kufanya ambavyo inatakiwa kufanya. Hivyo kama biashara yako iko sokoni na inafanya kazi kujitangaza hakukomi sababu mshindani wako kila siku anafikiria njia na namna ya kukushinda kibisahara mteja aliekuja kwako leo kesho awe ni mteja wake, hivyo unatakiwa kila siku kuwa kwenye ushindani, biashara ikifanikiwa ujue umekubalika lakini tambua ukiona unafanikiwa ujue kuna mwenzako amefeli na marekebisho ya chochote hufanya baada ya kufeli, hivyo aliefeli akirudi lazima atajipanga zaidi.Usikome kujitangaza au kutafuta masoko ushindani haukomi.

2. Biashara yoyote ili ikue inahitaji kuwa na matangazo, hivyo iwapo utasimamisha kujitangaza inamaana unasimamisha ukuaji wa biashara yako kitu ambacho hata kama umefanikiwa na umekua kwa kiasi gani iwapo matangazo yako yakipotea sokoni basi ujue na brand yako pia inapotea kichwani mwa wateja wako. Brand na muonekano wako unasimamiwa na branding, ambapo biashara kila siku inajibrand hivyo ukisimamisha kujitangaza umesimamisha ukuaji wa biashara.

3.Mauzo yako yanategemea sana matangazo yako hata hadhi yako sokoni inategemeana na hadhi ya matangazo yako na uwezo unaoutangaza hivyo mauzo yako yanategemea sana matangazo yako, kila siku mipango yako iwe ni ya kujitangaza na kuongeza masoko hata kama biashara inaendelea vizuri hauna sababu ya kuacha kufanya matangazo au kujitangaza kwa sababu mauzo yako ni matangazo yako.

4. Mteja wako anahitaji kukuona kila siku unaweka fedha kwa ajili ya kumtafuta hata kama umeshampata.hivyo iwapo utasitisha kutangaza unakuwa unaihatarisha biashara yako kupoteza wateja. Kila mtu ni mteja wa mtu fulani hakuna mtu anaefanya kila kitu katika maisha yake na hakuna kitu kizuri kama kumuona unaemwamini kama mtoa huduma au bidhaa akiwa imara na anajitangaza kwanza huongeza morali hata kwako na pia hukufanya kuwa mteja wa kudumu.USIACHE KUJITANGAZA, USIACHE KUJIBRAND.


Karibu katika Semina ya Branding online sehemu ya pili itakayofanyika kupitia mtandao wa Whatsapp kuanzia tarehe 1/05/2015. Jiandikishe kwa kutuma Namba na jina lako kwenda simu namba 0684 047323.ili ujiandikishe sasa. Elimu ya Branding ni ufunguo wa mafanikio ya biashara yako.

Kwa huduma ya ushauri na kufanya Branding ya biashara yako piga namba 0684047323 na utapata maelezo zaidi. ASANTE

Comments

Popular posts from this blog

Baadhi ya vitu vinavyosababisha biashara nyingi kufungwa.

Umuhimu na maana ya Logo( Nembo) katika biashara yako.

Aina za malengo na mipango